Nafasi ya mikopo 'kausha damu' katika ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja

SONDR

JF-Expert Member
Apr 18, 2019
271
643
Mkopo unatokana na kitenzi kukopa, Kukopa ni umiliki wa pesa kutoka kwa Mtu binafsi au Shirika au Taasisi za kifedha kwa makubaliano ya kurejesha kiasi kilichokopwa.

Mikopo kausha damu ni mikopo kutoka kwa Mtu binafsi au Shirika au Taasisi za kifedha yenye riba kubwa.

Mikopo kausha damu inapatikana kwa urahisi, unaweza kwenda leo na ukarudi na fedha zako kwa hiyo inaweza kuwa fursa kwa mtu mwenye shida ya haraka bila kujali madhara ya mkopo huo.

Masharti ya mikopo hiyo imewafanya baadhi ya wananchi kuathirika kisaikolojia kutokana na upetevu wa mali zao walizoweka dhamana.

Mara nyingi mikopo hiyo ambayo huchukuliwa kwenye taasisi za kifedha zisizotambulika kisheria imekuwa na riba kubwa ambayo huwapelekea wananchi wengi kushindwa kuwasilisha marejesho na hivyo kupelekea kuuzwa kwa nyumba au vitu vya thamani wanavyo vimiliki na kupeleka wanufaika wa mikopo kutumbukia katika lindi la umasikini.

Hata hivyo sheria ya biashaya ya kifedha " The microfinance act" ya mwaka 2018 inatoa katazo ya kufanya biashara ya kifedha kwa kutoza riba bilaya kuwa na leseni.

Ongezeko la taasisi zinazotoa mikopo yenye riba kubwa imegeuka kuwa machungu kwa wakopaji, imekuwa chanzo cha msongo wa mawazo, kufariki kwa shinikizo la damu na kutumbukia katika lindi la umasikini kutokana na upotevu wa mali zao.

Je, ni ipi nafasi ya mikopo hii katika ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja?
 
Je, ni ipi nafasi ya mikopo hii katika ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja?

Haina maana kwa sababu muda mwingine inachangia kuzorotesha maendeleo ya mtu mmoja mmoja hasa pale unapowaza marejesho..stress tupu
 
Haina maana kwa sababu muda mwingine inachangia kuzorotesha maendeleo ya mtu mmoja mmoja hasa pale unapowaza marejesho..stress tupu
Nawengi wanaokopa miko kausha damu wanauelewa mdogo sana kuhusiana na pesa na uchumi
 
Back
Top Bottom