Serikali ya CCM haifurahi ukiwa na kiasi kikubwa cha fedha benki, unafilisiwa kwa kupewa kesi ya Uhujumu Uchumi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Salaam Wakuu,

Nmeanza kuelewa kwanini Matajiri wengi wa Tanzania wanaficha fedha zao nje ya Nchi. Siwalaumu tena. Na kama hii hali ikiendelea, Benki nyingi zitatikisika kiuchumi kwani watu watasusa kupeleka hela.

Zamani Watanzania wengi walikuwa hawapeleki fedha zao benki. Walikuwa wanazichimbia mashambani na wengine kuzilalia kwenye Vitanda vya Kamba. Hii walikuwa wanafanya kwa kuhofia kunyang'anywa fedha zao na Serikali. Mabenki yalifanya Kampeni kubwa kuwabembeleza watu wapeleke fedha benki na Wakafanikiwa.

Hii hali sasa imerudi kwa kasi hivi Karibuni. Nini kinafanyika?

1. Wanafuatilia benki una kiasi gani, Wakikuta hela ni nyingi Wanazizuia, Ukienda kutoa hazitoki wanakuambia zinafanyiwa Uchunguzi.

2. Wanabuni mbinu watazipataje hizo hela, hivyo ramani inachorwa ya kuzipata kwa kuangalia makando kando yako. eidha unaweza ambiwa:
i) Unamiliki fedha zisizoendana na Kipato chako
ii) Hujalipia kodi, au umepata kwa Udanganyifu.

3. Utakamatwa na kufunguliwa kesi isiyo na dhamana;;Uhujumu Uchumi.
i) Utakatishaji fedha
ii) Kuongoza genge la Uharifu
iii) Kukwepa kodi nk

4. Unalazimishwa uongee nao mfanye Makubaliano ni kiasi gani cha fedha utawapa ili Uachiliwe huru

5. Unalazimishwa ukiri kosa halafu Unapigwa faini na fedha zako zinachukuliwa. Faini haizidi fedha ulizo nazo, wanazijua hivyo wanajua utalipa tu.

Baada ya hapo Wanakuachia huru unaendelea na kazi zako. Unaanza upya kujitafutia kipato, kikiongezeka Mzunguko unaanza tena hapo kwenye maelezo namba moja.

Hakika adui wa Mtanzania ni Mtanzania.

Hapa chini naweka Mifano Michache ya Watu waliochezewa hii style ya kunyang'anya watu fedha zao ukiachilia mbali Tariq Machibya maarufu Mr Kuku.

1. Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Ndugu Erick Kabendera

2. Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika

3. Wafanyabiashara saba wa mafuta wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya SHIN UP Tanzania limited Zhang Zhi XIN, LINCOLN

4. Mkurugenzi mkuu wa Benki M Tanzania, Sanjeev Kumar

5. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura

6. Astery Ndege aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers

7. Mfanyabiashara Daniel Chizua aliyedaiwa kukutwa na Kobe Wawili

8. Raia wa China, Liang Hu aliyedaiwa kuua Tembo 511

9. Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet

10. Wafanyabiashara Noah Mmasanga, Richard Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo na wengine wengi.

Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.

Je, ni lini Tutapata Mabilionea Wapya sababu Waliopo Wanazidi kuaga dunia.

Nashauri wachunguzi wa mambo wafanyie kazi Vifo vya hawa Matajiri wa Kitanzania ambao wamekufa kwa kufuatana . Isijekuwa ni hela zao zimewatoa roho. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi Subhash Patel, Mr Reginald Mengi, Dr Rajni Kanabar, Ali Mufuruki, Salim Hassan Turky, Mr Salum Shamte nk.

 
Tutaanza kuzichimbia ndani Tena chumbani, tunachimba shimo chumbani chini ya uvungu wa kitanda na kuweka cement na chuma hafu tunapiga kufuli. Hakuna atakaye jua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usifikiri ni utani.

Leo hii ukipata tu hela nyingi, fikiria mara mbili kabla hujapeleka bank.

Kuna wakati nililkuwa nalipwa mshahara wa dola 9,000 kwa mwezi. Nilikuwa nimeajiriwa nje ya nchi lakini niliomba mshahara wangu ulipwe kwenye akaunti yangu ya nyumbani hapa Tanzania.

Niliporudi likizo, kutaka kuchukua hela, nikaambiwa nikamwone manager wa branch. Baadaye nilifanikiwa lakini baada ya kupeleka documents za mkataba, work permit, nakala ya dicuments za kodi za nchi nilikokuwa nafanya kazi, n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama naiona nchi ya Kenya ikienda kunufaika na mapesa ya watanzania yatakayoanza kumiminika kwenye mabank yao.

Maana hawa majiniwatu wakishamalizana na wenye million 100 and above watashuka mpaka na wenye < tsh milioni 1.

Nchi imevamiwa hii, mtawala kichaa anataka watu wawe mafukara ili awahonge chumvi na vijikanga wakati wa kampeni lakini akae akitambua dunia imebadilika sana hawezi kutufirisi huku tukimuangalia tu.

Kinachompa kiburi ni hirizi na matambiko anayojifanyia kila mwezi sijui anafikiri yeye ndie anaeujua uchawi kuliko akina Mobutu na the like.

TRA na Huyo waziri wao wa fedha wakae wakijua sasa dunia inaendeshwa na teknolojia soon mwakani kutakuwa na digital yuan,digital Euro,digital ksh nk amabazo zitahifadhiwa kwenye software wallets na ukumbuke hizi zitakuwa ni borderless kwahiyo hata sisi tutaweza kuzitumia

Kama naiona shilingi ya Tanzania ikenda sifuri mud mfupi ujao maana siku hizi hakuna anaetaka ujinga na ujuha kama wa hili liserikali la kiuwendawazimu na kishetani

#ni muda tu
#ni muda tu
#ni muda tu
#ni muda tu
 
Back
Top Bottom