Luhaga Mpina: Mwigulu Nchemba, Mbarawa, Mkurugezi wa TRC na wote waliohusika wakamatwe na kushtakiwa kwa makosa ya Uhujumu Uchumi

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Mpina akiwa anachangia hoja amesema kamati imekiri suala la kutumia mzabuni mmoja lilikataliwa na PPRA ambaye ndio msimamizi mkuu wa manunuzi nchini, lilikataliwa na bodi ya manunuzi, na walikataa sababu sheria za nchi za manunuzi ilikuwa inatekelezwa wakayti huo haziruhusu mambo hayo, lakini pia walikataa sababu ulikuwa huwezi kupata thamani ya pesa kwa njia hiyo iliyotumika.


Akaendelea kuwa waziri wa fedha aliandika barua kupitia kwa katibu wake mkuu kutaka mkataba usainiwe ambayo hiyo pia ni muendelezo wa kuvunja sheria za nchi.

Lakini pia wamesema tulilazimika kutumia njia ya single source ili tupate mkopo wa standard chattered, lakini Mkopo wowote nchini unachukuliwa kwa mujibu wa sheria, na kwamba hauwezi kuchukua mkopo kwa kuvunja sheria za nchi.


Akasema kuwa amejiridhisha suala la kutumia mzabuni mmoja ni wizi rushwa na ufisadi, na hivyo anapendekeza kamati ya PAC kuvunja mkataba wa TRC kati ya Yapi Merkezi Rot 1 & 3 na kuitangaza upya.


2. Mwigulu, Mbarawa, Mkurugenzi wa TRC, Mkugenzi wa Yapi Merkezi na wengine wote waliohusika wakamatwe, washtakiwe kwa makosa ya Uhujumu Uchumi.
 
Mpina akiwa anachangia hoja amesema kamati imekiri suala la kutumia mzabuni mmoja lilikataliwa na PPRA ambaye ndio msimamizi mkuu wa manunuzi nchini,...
Akasema kuwa amejiridhisha suala la kutumia mzabuni mmoja ni wizi rushwa na ufisadi, na hivyo anapendekeza kamati ya PAC kuvunja mkataba wa TRC kati ya Yapi Merkezi Rot 1 & 3 na kuitangaza upya

2. Mwigulu, Mbarawa, Mkurugenzi wa TRC, Mkugenzi wa Yapi Merkezi na wengine wote waliohusika wakamatwe, washtakiwe kwa makosa ya Uhujumu Uchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akaendelea kuwa waziri wa fedha aliandika barua kupitia kwa katibu wake mkuu kutaka mkataba usainiwe ambayo hiyo pia ni muendelezo wa kuvunja sheria za nchi.

Lakini pia wamesema tulilazimika kutumia njia ya single source ili tupate mkopo wa standard chattered, lakini Mkopo wowote nchini unachukuliwa kwa mujibu wa sheria, na kwamba hauwezi kuchukua mkopo kwa kuvunja sheria za nchi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa lazima wajumbe walikate jina lake 2025,kwani chama chake hakija zoea kuambiwa ukweli. Hapo husishangae siku wakimwita na kumuonya kwa kuongea ukweli.

Sometimes naona hatupo tayari kuzifanyia kazi ripoti za CAG, kama inawezekana CAG ofisi yake ivunjwe tufanye mambo mengine. Maana wausika wanatajwa na CAG ila hawa chukuliwi hatua.
 
Mpina akiwa anachangia hoja amesema kamati imekiri suala la kutumia mzabuni mmoja...
https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/2154472/Mjadala unaoendelea bungeni kuhusu ripoti ya CAG hasa kwa siku ya jana ni wazi kuwa kuna ubadhilifu mkubwa sana umefanywa kwenye sekta ya nishati, mafuta, uchukuzi na maji.

Ni wazi waziri mwizi na mla rushwa kama January Makamba, waziri mzembe Profesa Mbarawa, Aweso na watu kama Dokta Andilile kule EWURA ,Kadogosa kule TRL wanatakiwa wawe jela muda huu au wameshajiuzulu nafasi zao au kufukuzwa kabisa.

Wizi na ulaji rushwa uliofanywa na January Makamba ni wa kihistoria ndani ya wizara ya nishati na ushahidi uko wazi kwa jinsi alivyounda mtandao wa ulaji rushwa na wizi kwenye mfumo wa kuagiza mafuta.

Ni wazi na ushahidi upo jinsi January Makamba alivyotoa vibali vya kuagiza mafuta kwa yule tu anayempa rushwa ya $300,000 na amefanya hivyo mpaka kufikia TAOMAC (chama cha waagizaji mafuta nchini) wakalazimika kuwasilisha malalamiko serikalini.

January Makamba hakuishia kufanya wizi huko tu bali alikwenda mbali zaidi na kuvuruga kabisa utendaji wa REA (wakala wa umeme vijijini) ambako CAG alibainisha wakandarasi kunyimwa kazi bila sababu za maana na wana uwezo lakini ukweli ni kuwa waliokataa kutoa rushwa wote kwa January kupitia mwizi mwenzake Maharage Chande walimfuta kazi na kumnyima tenda na ushahidi uko kwenye ripoti ya CAG.

January Makamba waziri mwizi na mla rushwa mkubwa kuwahi kutokea alihusika kununua mita za LUKU zenye thamani ya 105bn TZS bila kufuata sheria ya manunuzi na hazina kiwango na haijulikani zimetengenezwa wapi na supplier ni nani lakini tunaambiwa ni kazi amefanya yeye na ndugu yake Maharage Chande na wameiibia serikali jumla ya 45bn TZS kwenye ununuzi huu haramu.

January Makamba ana tuhuma za kukwapua 15bn TZS kwenye mradi wa LNG kule Mtwara na kuna ushahidi ambao CAG ameogopa kuuandika kwa madai kuwa amefanya hivyo kuinusuru serikali. Mengine ya vyura kulipiwa bila kufuata utaratibu na kuashiria ubadhilifu hayo mtayasoma wenyewe kwenye ripoti.

January Makamba ameshiriki kuficha nyaraka na kumsaidia Seth wa IPTL kuilaghai serikali na leo hataki kulipa faini ya mabilioni ya fedha kwa kuwa January Makamba kashiriki akiwa nishati kuficha nyaraka muhimu za IPTL na sasa serikali haiwezi kumdai tena Seth na IPTL chochote kinyume chake eti yeye ndiyo anaidai serikali.

January Makamba HAFAI kuendelea kukaa ndani ya baraza la mawaziri kwa sababu tuhuma zake za rushwa ni kubwa sana na wizi amefanya akiwa nishati ni wa kiwango cha UFISADI wa kutisha sana. Achilia mbali tuhuma zake za kuwauwa kwa sumu wafanyakazi wa umma akiwemo afisa wa TRA kule Tanga na wafanyakazi watatu wa ofisi ya CAG na tuhuma za kufanya jaribio la kumuuwa kwa sumu waziri mkuu ,huyu mtu anakaaje kwenye baraza mpaka leo?

January Makamba ana tuhuma na ushahidi upo wa kuwatumia maafisa wa idara ya usalama wa nchi kusaka wapinzani na wakosoaji wake nje na ndani ya Tanzania na kutaka kuwauwa, anakuwaje bado ndani ya serikali? Huyu mtu ni murderer na gaidi kabisa kwa sababu alifikia hatua ya kukodi makundi ya wahalifu wa kisomalia kufanya kazi hii akishirikiana na watu wasio waaminifu ndani ya vyombo vya usalama.

Kadogosa anahusika na upotevu wa mabilioni ya hela za SGR na alihusika kwenye kutoa tenda bila ushindani na watu wakakwapua mabilioni ya fedha za mradi na sasa SGR imekwama. Kwa hali hii tunawezaje kuwa na Kadogosa ofisini mpaka leo? Uwepo wake ni jibu kuwa analinda maslahi ya wakubwa walioshiriki kwenye huu wizi. Huyu hakupaswa kuendelea kuwapo ofisini mpaka leo kwa kuwa ananuka rushwa na yuko pale kusaidia wizi na majibu ya kazi yake mmeyaona kwenye kukwama na kusuasua kwa mradi wa ujenzi wa SGR. Kila siku ni blah blah tu

Dokta Andilile wa EWURA huyu ni mwizi kama alivyo January Makamba na wameshiriki kwa kiwango kikubwa sana kufanya wizi na kuvuruga sekta ya nishati hasa kwenye mafuta na kuendelea kumuacha madarakani ni kubariki wizi walioufanya. Na hili ndiyo eneo ambalo ma cartel ya wizi wa mafuta nchi yamefanikiwa kumnasa na kumrubuni

Biteko hawezi kuona madudu ya EWURA kwa sababu kwanza kishapofushwa macho kwa rushwa kubwa kubwa anazopewa na akina Anil Shuchak na wenzake, pili anahongwa majumba na hawa watu kiasi kwamba kasahau kuwa aliteuliwa ili kufasisha uchafu wa hii sekta. Tatu kaacha kufanya kazi kisomi sasa anategemea waganga na wachawi alioletewa na watu hawa ili kufanya kazi. Bahati mbaya sana hawezi tena kufanya hilo na amekuwa sehemu ya majambazi na majizi haya yanayoharibu sekta ya mafuta nchini toka wakati wa January Makamba kama waziri wa nishati.

Prof Mbarawa kuendelea kuwemo kwenye baraza la mawaziri ni muujiza mwingine hasa kufuatia uzembe mkubwa sana aliofanya kwenye kushughulikia suala la uwekezaji bandarini. Uzembe wake na kukosa maarifa ndiko kulikolitia taifa hili kwenye sintofahamu kubwa kiasi kile na huyu hakustahiki hata leo hii kuwa waziri.

Profesa Mbarawa ni chanzo cha rushwa na wizi ukiofanywa sana TANROADS na CAG ameweka wazi kwenye ripoti yake kitu kilichopelekea yule bosi wa wakati ule kufukuzwa na sasa anatakiwa awajibike na madudu yake na afuatwe huko aliko na kuwajibishwa.

Kiburi cha uzima na usomi ndicho kinachomfelisha sana Profesa Mbarawa kwa kuwa anajiona yeye ni Mungu mtu na hakuna anayeweza kumwambia kitu kwa kuwa yeye ni Profesa. Lakini kiukweli Profesa Mbarawa ni waziri wa kawaida sana kama siyo wa hovyo kuwahi kushika hii wizara kwa miaka mingi sana. Na kupitia fursa hii ya kujadili ripoti ya CAG tusaidieni kufukuza majitu kama Mbarawa.

Aweso Jumaa kule kwenye wizara yako kuna makandokando mengi ikiwemo kuibiwa hela kwenye miradi ya maji hasa ule wa kule Same. Tumeambiwa na CAG kuwa kuna mabilioni yameibwa na wewe Aweso unajua nani wahusika lakini uko bize unajibaraguza kama vile huna habari na hujaona alichokisema CAG.

Aweso uko bize na mazingaombwe na kusaidia wizi kwenye wizara yako na unashindwa kujua kuwa kuna mradi wa mabilioni ya hela umetelekezwa hapo Dar Es Salaam kule Msumi na Makabe Mbezi? Watu wameiba fedha na kutelekeza mabomba na mitaro waliyochimba kutandaza mabomba hayo. Halafu upo tu una kazi ya kupigapiga magoti wakati wa mazingaombwe yako kwenye ziara huko mikoani.

Aweso wizara yako ina maukamasi sana lakini ni vile watu hawaimuliki sana na wamezoea shida za maji ndiyo maana unatembea mabega juu kama kuna mambo ya maana sana unafanya lakini kwa kifupi wizara yako na wewe mwenyewe mnaongoza kwa wizi na bunge litusaidie kuwafukuza kwa maana hamna tija yoyote zaidi ya kufanya mazingaombwe tu na kutesa watanzania bila sababu! Huna uwezo wa kuwaondolea watanzania kero za maji ila una uwezo mkubwa sana wa kufanya mazingaombwe majukwaani.

Biteko ni vile kateuliwa juzi juzi tu kuwa waziri na naibu waziri mkuu lakini huyo naye ni tatizo vilevile. Ukitaka kuona ni sehemu ya majizi ndani ya nchi hii angalia kiwango cha matukio ya kukamatwa kwa dhababu zinazotaka kutoroshwa ndiyo utajua hakunaga mtu hapa na alikuwa anafanya matukio ya kutosha alipokuwa madini ni vile watu huwa hawanaga habari na hiyo wizara.

Kwa kuwa sasa amejiingiza kwenye kundi la majizi na yanamhonga mpaka majumba basi huyu tutamuwekea utaratibu tofauti wa kumshughulikia na siyo huu wa sasa.

Kwa kifupi ni kuwa watu hawa wanatakiwa baada ya bunge kumaliza kujadili ripoti ya CAG wanatakiwa aidha wawe jela au wawe wamefukuzwa kazi;

1. January Makamba
2.Maharage Chande
3. Dokta Andilile James
4.Jumaa Aweso
5. Profesa Makame Mbarawa
6. Masanja Kadogosa

Hawa watu hawatakiwi kuendelea kuwa kwenye utumishi wa umma hata kwa dakika moja kwa kuwa ni hatari kwa ustawi wa nchi kwa matendo yao na mambo yak kama alivyoainisha CAG kwenye ripoti yake inayojadiliwa sasa bungeni Dodoma.

MWISHO tunawakumbusha watu hawa kuwa Mheshimiwa Rais aliwateua iki kusaidia kuongoza nchi na kazi ya kutumikia watanzania na siyo kufanya wizi kama mnavyofanya sasa.

CAG endelea na moyo huu wa uzalendo na usifiche kitu kuna siku Mungu atakuja kukulipa kama hutalipwa hapa duniani.
 
Naunga mkono hoja lkn kinachonishangaza ni kwa nn kwenye orodha yako umemwacha mwigulu nchemba?!, yaani kwenye hiyo namba ya kwanza ni ya ama mwigulu ama January.woote hao ni maharamia wakubwa.na kama hawatatoka kwenye nafasi zao,basi tujue wako pamoja na mkuu wa nchi,maana yake wizi huo utakuwa na baraka za rais samia suluhu hasan.
 
Katiba katiba katiba ndio itakuwa suluhu. Kwanini hamtaki katiba iboreshwe?

Huo ndo ushahidi unaojirudia na kwa miaka sasa na mkapa alikiri.

Jamani kubarini kusuka upya katiba itakayoruhusu kila mmoja kudhibitiwa na kushitakiwa na kila mmoja kuwa mlinzi wa rasilimali.

Lakini itakayo walipa vizuri wakubwa wanaopewa dhamana na wananchi kwa kuchaguliwa kihalali
 
Back
Top Bottom