Mbeya: Watuhumiwa 14 wa Mtandao wa kuchepusha mapato ya Serikali wafunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,249
Jana tuliambiwa waliokamatwa wamefikia 40, lakini Taarifa mpya inaeleza kwamba 14 miongoni mwao wamepewa kesi ya Uhujumu uchumi.
---

Watu 14 wamefikishwakatika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mbeya na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 03/2023 wakituhumiwa kuendesha genge la uhalifu kinyume Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Washitakiwa wanatuhumiwa kutenda kosa hilo kwa kutengeneza mfumo haramu wa kukusanya ushuru wa mazao wilaya za Mbarali, Rungwe, Mbeya, Ileje na Momba na kufanikiwa kukusanya TZS milioni 382.8.

Pamoja na shitaka hilo, mshitakiwa wa nne hadi mshitakiwa wa 14 wameshitakiwa pia kwa kosa la kumiliki kifaa haramu kinyume na kifungu cha 10(1)(a) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao. Washitakiwa hao wameshitakiwa kwa kosa hilo baada ya kukutwa wakimiliki mashine za POS ambazo zilikuwa na mfumo haramu wa kukusanyia ushuru wa mazao.

Aidha, mshitakiwa wa kwanza, tatu na 14 wameshitakiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha kinyume na kifungu cha 12(b) na 13(1)(a) cha Sheria ya Utakatishaji Fedha. Wanatuhumiwa kutumia fedha walizozipata kutokana na kukusanya ushuru wa mazao kwa njia harumu kununulia viwanja na nyumba ili kuficha ukweli juu ya uchafu wa pesa husika.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo hawakupaswa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo bado haijapewa mamlaka ya kusikiliza shauri.

Washitakiwa wote wamerejeshwa rumande kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa shauri la jinai ambalo kiasi cha fedha inayotuhumiwa ni zaidi ya TZS milioni 300.

Kesi hiyo itatajwa Septemba 11 mwaka huu.

Swahili Times
 
Shortcut tamu sana..ila hao walinogewa na walikuwa wanalindwa, hapo wametolewa kafara tu!
 
Ndivyo alivyosema hata Rais
Ajabu watu hawa wameachwa
Ongeze Maafisa Tarafa na watendaji wa kata na kijini...Halafu naona kufumia POS si huwa wanapewa vifaa tayari vimefungwa mfumo So huenda Wamuulize IT wa wilaya ye ndo anakosa la kufumga mfumo huo hso waliotumia mfumo hawana kosa wao walifanya majukumu yao hii kazi naijua sana so naona hao wengine kuanzia wanne mpaka 14 walifamya kwa kama sehemu ya kazi walizopangiwa na wakuu wao so hawakugusa pesa yyte
 
Back
Top Bottom