Serikali waambieni vijana kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa na kwao kama wananchi

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,556
2,996
Tabu laaaa tabu leeeee!!!!

Bandiko langu litakuwa fupi lenye lengo na madhumuni ya kuikumbusha serikali faida na umuhimu wa kilimo katika taifa na hivyo kutilia mkazo wa nguvu kwa vijana kuacha kushinda kwenye mitandao na kwenye majumba ya kamari kama mbadala wa ajira kwao.

Mwanzo nianze kwa kusema kilimo ni kiini cha maendeo pia kilimo ni chachu ukuwaji wa maendeleo,tunapoongelea kilimo tunaongelea uwekezaji na suala la uwekezaji linahitaji akili na maarifa katika mirija ya kile unachowekeza, Vijana wengi tunashindwa kuzifanya akili zetu kufikiria kuhusu kilimo kwa sababu wengi wetu ni tunahitaji matokeo ya haraka(Rapid profit) na hatima yake kuangukia kwenye uwekezaji wa bahati nasibu ambao ni hasara kubwa kwa Taifa.

Kwako serikali muhimili wa kilimo ni sera na ubora wa sera ni mipango na uzuri wa mipango inahitakiwa kuwa yenye kueleweka na kutelezwa kwa kiasi kikubwa,serikali inatakiwa kujenga sera madhubuti yamikopo, kodi na ruzuku kwa vijana ambao wamejitolea kufanya kilimo ili kutoa motisha kwa ukuwaji wa ndani wa soko na kupunguza kupanda kiholela kwa bei ya bidhaa pamoja na kulinda thamani ya shilingi dhidi ya dola.

Umuhimu wa kilimo

1. Kongezeka kwa chakula katika taifa
2. Kulinda ardhi kutokana na majanga ya asili
3. Fursa kwa kwa vijana
4. Kupungua kwa gharama za maisha
5. Kuongezeka kwa uchumi wa Taifa na watu wake.
6. Kujitangaza kimataifa kwa biashara au utalii wa kilimo,kulinda mazingira .n.k

Bado tunalalamika maisha ni magumu ila tunazo nafasi kama taifa kupiga hatua kwenye kilimo na kurithisha ukwasi kwa jamii ijayo.
 
Katika vijana/watoto 10

8 kati ya hapo wanataka kuwa wasanii

Wakata mauno,mambo ya kulima

Hawakuelewi

Ova
 
Naungana na wewe mkuu.
 
Back
Top Bottom