JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Kongamano hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano Kati ya Taasisi ya MOI na Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha Marekani limeshirikisha ambapo ya Wataalam 120 wanashiriki kutoka Mataifa mbalimbali Duniani limefanyika Jijini Dar es Salaam.
Amesema uanzishwaji wa huduma hiyo inayotumia teknolojia ya kisasa inayotawala Dunia kwa sasa na itasaidia kuwapunguzia Wananchi gharama za kufuata matibabu ya aina hiyo nje ya nchi na kukuza tiba utalii hapa nchini.
“Hii ni kwa mara ya kwanza kwa MOI na ni mara ya kwanza kwa Taifa kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia matundu (Endoscopic Spine Surgery), kwa dhati tunakishukuru Chuo Kikuu cha Weill Cornel cha Marekani kwa ushirikiano huu muhimu na kwa niaba ya menejimenti naahidi tutauenzi,” amesema Prof. Makubi.
Prof. Abel Makubi
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu kutoka Taasisi ya MOI, Dkt. Hamisi Shabani
Upande wake Mkurugenzi wa Upasuaji wa Mgongo kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornel Marekani, Prof. Roger Hartl ameahidi kuendeleza ushirikiano na Taasisi ya MOI katika kuendelea kuwajengea uwezo wataalam, kuwezesha tafiti za kisayansi na vifaa tiba vya upasuaji ili iweze kuwa kituo mahiri cha upasaji wa mgongo barani Afrika.
“Lengo letu kuiona MOI ikiwa kituo cha umahiri kwenye kutoa tiba na mafunzo kwa mataifa mengine juu ya upasuaji wa mgongo kwa kutumia matundu, nimefurahi kuona namna ambavyo MOI inathamini ushirikiano wetu na ninaahidi kuuendeleza,” amesema Prof. Hartl
Prof. Roger Hartl