Serikali upande wa elimu irasimishe vituo vya watoto chekechea kufundisha hadi darasa la 3 ndipo wajiunge na shule za msingi kuendelea darasa la 4

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
Serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi;

Naomba ifikilie kurasimisha vituo vya watoto chekechea viwe (basic schools).

Ambapo Watoto watafundishwa kwa miaka mitatu katika vituo hivyo vya chekechea kwa maana ya baby class mwaka mmoja, middle class mwaka wa pili na top class mwaka wa tatu, then Mtoto ndipo atajiunga shule ya msingi kuanza darasa la nne,tano,sita na saba!

Utaratibu huu uwe ni wa hiari kwa wale watakaopenda.

SABABU YA KUFANYA HIVYO
  • Miji inapanuka kwa kasi Sana kiasi kwamba watoto wakiwa bado wadogo wanasafili umbali mlefu kufika shule ya msingi
  • Shule za msingi hazina bajeti ya uji lishe kwa watoto Jambo ambalo Ni Mhimu kwa watoto hususani hawa wa madarasa ya awali
  • Chekechea zinahitaji eneo dogo ili kusajiliwa tofauti na shule ya msingi, hivyo zitapatikana kwa wingi na karibu zaidi na makazi ili kurahisisha kupeleka watoto
  • Uwezo wa kueleweshwa na kufundishwa watoto ni mkubwa zaidi kwasababu idadi haitakuwa kubwa kulinganisha na shule za msingi
  • Kutokana na msingi Bora wa chekechea watoto wataweza kumudu masomo ya msingi kirahisi zaidi kuliko Sasa
  • Kwa miaka mitatu watoto watakuwa wamekomaa hata kwenda wenyewe kwa mguu shule za msingi zilizo umbali mlefu.
  • kupitia utaratibu huo wa hiari serikali itazalisha ajira kwa walimu.
  • Msongamano uliopo Sasa shule za msingi utapungua na nguvu itaelekezwa kuanzia darasa la nne Hadi la Saba
KUPANGA NI KUCHAGUA
 
Naunga mkono hoja tunatumia muda mwingi sana shuleni manufaa hayaonekani bora watu wamalize wakiwa wadogo wawe na uwanja mpana wa kujaribu mambo na kuwa wabunifu wasije wakayafanya makosa ya kimaamuzi wakiwa hawana muda wa kuyarekebisha kwa maana umri unakuwa umeshawaenda.
 
Wazo zuri sana.
 
Daah mkuu umenigusa, kila siku nachelewa kazini kwa kuwapeleka watoto wangu shule ilihali hapa jilani Kuna chekechea!

utaratibu huu ungekuwepo ingekuwa poa sana
 
Naunga mkono hoja tunatumia muda mwingi sana shuleni manufaa hayaonekani bora watu wamalize wakiwa wadogo wawe na uwanja mpana wa kujaribu mambo na kuwa wabunifu wasije wakayafanya makosa ya kimaamuzi wakiwa hawana muda wa kuyarekebisha kwa maana umri unakuwa umeshawaenda.
exactly inaweza saidia sana
 
Back
Top Bottom