Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,861
Serikali itoe taarifa kwa umma kama utenguzi wa Balozi wa Tanzania nchini Misri ulifutwa ama laa.
Tarehe 15 August 2023 Rais Samia alifanya mabadiliko ya vituo vya kazi na utenguzi wa mabalozi na kumrejesha nyumbani Balozi wa Misri Nchini Tanzania Ndugu Emmanuel Nchimbi, na nafasi yake ikachululiwa na Balozi Meja General Makazo.
Taarifa hiyo ilitolewa kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Tangu hapo hakukuwepo na taarifa yoyote ya mabadiliko juu ya nafasi hiyo.
Lakini siku 42 baadae yaani juzi baada ya Tanzania kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa AFCON 2027, Msafara wa Tanzania uliongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri ambae ni Dr Emmanuel Nchimbi ambae taifa linajua alitenguliwa na kurejeshwa Tanzania. Taifa linatakiwa kutangaziwa mabadiliko mengine kama yalifanywa na lifahamishwe Meja Jenerali Makanzo kapelekwa kituo gani cha kazi ikiwa Nchimbi bado anahudumu kama balozi nchini Misri.
Ni takwa la kikatiba na kisheria umma kutangaziwa mabadiliko ya nafasi yoyote ya uteule wa kirais na sio vinginevyo. Kama kuna Mabadiliko ya kimyakimya basi yanaleta mkanganyiko kwa umma.