Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,446
- 7,817
Akizungumza leo Januari 20, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi yake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Nchimbi amesema hakuna mtu asiyejua CCM ndio chama kinachoongoza Serikali, hivyo hakuna ulazima wa kutumia nguvu kudhalilisha watumishi wake.
“Hatuwezi kusimamia Serikali kwa kuwa tunawatukana tukana watu, wewe hapa, kwa nini, mshenzi sana wewe, ahaa hiyo mshenzi haipo katika Ilani ya CCM , lazima tuwaheshimu watumishi wa Serikali, tuongoze kwa weledi.”
Alisema Dkt. Nchimbi
---
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuael Nchimbi ni kama ametupa jiwe gizani akiwaonya baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaotumia mamlaka yao kudhalilisha viongozi wa Serikali.
Bila kutaja majina, Dk Nchimbi amesema kumekuwa na utamaduni wa viongozi wa chama hicho kutoa maelekezo kwa viongozi wa Serikali.
Akizungumza leo Januari 20, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi yake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Nchimbi amesema hakuna mtu asiyejua CCM ndio chama kinachoongoza Serikali, hivyo hakuna ulazima wa kutumia nguvu kudhalilisha watumishi wake.
Januari 15, mwaka huu, chama hicho kilitangaza kumteua Nchimbi aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri kushika nafasi hiyo iliyokuwa wazi baada ya Daniel Chongolo kujiuzulu kwa madai ya kuchafuliwa kwenye mitandao ya kijamii.
“Chama chetu kisikwepe wajibu wake wa kuisimamia Serikali, ni wajibu wa kikatiba na kikanuni. Sisi ndio tulichaguliwa na wananchi. Mkataba ni kati ya CCM na wananchi na mtekelezaji wa mkataba ni Serikali, lakini tusimamie bila kuwa na kiburi, tusimamie kwa weledi,’’ amesema.
Bila kutaja jina la mhusika anayetukana viongozi wa Serikali, Nchimbi alisema: “Hatuwezi kusimamia Serikali kwa kuwa tunawatukana tukana watu, wewe hapa, kwa nini, mshenzi sana wewe, ahaa hiyo mshenzi haipo katika Ilani ya CCM , lazima tuwaheshimu watumishi wa Serikali, tuongoze kwa weledi.”