WanaJF ninaandika nikiwa na hasira zilizochanganyikana na huzuni kuhusu kinachoendelea huko Arusha. Kwanza kabisa niseme mimi ni mzaliwa wa Arusha na nimekulia huko. Kilichonitoa Arusha ni elimu ngazi ya chuo kikuu. Nitakachoandika hapa sio stori za kuhadithiwa au kuona kwenye media.
Kwa miaka ya karibuni hasa mwaka huu kumeripotiwa ajali nyingi za pikipiki zilizoondoa maisha ya vijana wengi na kuwaachia wengine ulemavu. Tofauti na sehemu zingine kwa Arusha imeonekana hii misiba ni kawaida hali inayopelekea kuwepo na masikhara mengi sana misibani. Vyombo vya habari hasa vya mitandaoni vimekuwa mstari wa mbele kuripoti masikhara yanayofanyika misibani huku msiba wenyewe ukipewa uzito mdogo. Mkipita kwa Millard Ayo na online media zingine mtaona vijana wa Arusha maarufu kama machii wa R wakifukia makaburi kwa mikono kama kuonyesha heshima kwa mwenzao. Ule ni upuuzi unaopelekea kuonekana kama ajali iliyotoa uhai ni jambo dogo.
Pamoja na ajali za pikipiki pia kuna tabia ya vijana wengi wa Arusha kufanya bidii waonekane wao ni wahuni kuanzia mavazi hadi kuongea. Wazazi na walezi wengi wanaugulia ndani kwa ndani hakuna namna. Mimi ninakataa kabisa huu USELA MAVI wa hawa vijana. Vijana wengi wameacha kusoma na kukimbilia bangi, pombe na mambo mengine ya kijinga. Media pia zimekuwa na ujinga wa kupromoti huu upuuzi wa Machalii wa R.
Pichani dada maarufu mitaa ya Kijenge aliyefariki kwa ajali ya pikipiki mwaka jana. Alijulikana kwa jina maarufu LA MAMA. Huu msiba uliniuma sana. Ndoto zangu nyingi kwa huyu hayati "La mama" zilizimika.