Utoaji taarifa zisizohakikiwa za vifo vilivyotokana na Ajali huzua taharuki kwenye Jamii

JamiiCheck

Member
Nov 3, 2023
54
41
1000014911.jpg

Pamoja na ukweli kuwa teknolojia imeleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya habari na mawasiliano, ambapo sasa mtu yeyote(Netizen) anaweza kutoa taarifa ikawafikia watu wengi kwa haraka sana, lakini ni vyema kuhakiki na kuthibitisha taarifa yoyote ambayo unaona inaweza kuzua taharuki kabla hujaiweka mtandaoni

Pindi itokeapo ajali, wananchi wamekuwa wakisaidia kwa nia njema kusambaza taarifa za ajali hiyo kwenye mitandao ya kijamii. Kasoro hutokea pale wanapotoa taarifa za vifo ambazo zinakuwa bado hajizathibitishwa na mamlaka husika. Unakuta kuna ajali ya basi imetokea, mwananchi aliyejitolea kusambaza taarifa hizo, bila kuwa na uelewa anaweza kupotosha kwa kutaja idadi ya vifo isiyo sahihi mfano kwa kusema watu wote waliopata ajali wamefariki dunia. Taarifa kama hii inaweza kuzua taharuki kubwa sana katika jamii.

Kuhabarisha kuhusu ajali ni jambo moja, lakini kuhusu idadi ya vifo ni jambo jingine linalohitaji umakini zaidi. Huwezi kuhabarisha kuhusu idadi ya vifo vilivyotokea kwenye ajali kwa kukisia tu. Ni vyema kuwasiliana na mamlaka husika kwa uhakiki zaidi.

Pia ili kupunguza ukali wa taarifa, kama umeona kuna umuhimu wa kutoa taarifa ya idadi ya vifo kuna maneno unashauriwa kutumia mfano, INASEMEKANA, INADAIWA, INAKADIRIWA WATU KADHAA n.k

Tunawakumbusha watumiaji wa mitandao wote kuhakiki taarifa yoyote wanayopata kabla ya kuisambaza. Unapojiridhisha kwa kuhakiki taarifa yako, unapunguza uwezekano wa kuzua taharuki kwenye jamii.

Kufikia Jukwaa la JamiiCheck, bofya HAPA.
 
Back
Top Bottom