LATRA K'njaro yawezesha SACCOS kwa Bajaj na Bodaboda

Jun 20, 2023
54
51
Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini mkoani wa Kilimanjaro(LATRA)imekamilisha mchakato wa uanzishwaji wa Chama cha ushirika wa Akiba na mikopo(SACCOS)kwa ajili ya chama cha Madereva wa Bajaj na Bodaboda Katika mkoa wa kilimanjaro.
Mpango huo inatajwa kama moja ya mwarobaini wa kutafua changamoto zinazowakabili vijana hao ambao wengi wao maisha yao ni duni.
Afisa mfawidhi wa LATRA mkoa wa Kilimanjaro,Paul Nyello anasema kabla ya kuanzishwa kwa saccos hiyo vijina 65 walipelekwa Chuo kikuu cha ushirika moshi kwa ajili ya kupigwa msasa juu ya uendeshaji wa saccos huku gharama za mafunzo hayo zlkibebwa na serikali .
"Tunategemea uanzishwaji wa Saccos hiyo utaleta mapinduzi ya ya kifikra na kupitia Saccos hii wataweza kukopeshana lakini vilevile wataweza kuaminiwa na Taasisi za fedha"
"Vijana Hawa wengi wao huko nyuma walikuwa wanakopeshwa Katika mazingira yenye utata na pia walikuwa wanaingia mikataba yenye utata na wamiliki wa hivyo vyombo vya usafiri na mwisho wake kuishia kudhulumiwa haki zao",
Mbali na Saccos,LATRA kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwamo Veta,polisi wapo kwenye miakati maalumu wa kuwapatia mafunzo ya udereva vijana hao ambayo yatawawesha kupatiwa vyeti pamoja na leseni na kuachana na leseni za kununua ambazo mwsho wake siyo mzuri.
Nyello anasema mpango huo unatarajia kuleta mapinduzi makubwa Katika mkoa wa Kilimanjaro na utakuwa pia ni mwarobaini wa kupunguza matukio ya ajali ambayo mengi huchangiwa na kutokuzingatiwa kwa kanuni na sheria za usalama barabarani.
Hii ni program ambayo tunaifanya kuelekea kwenye Uzinduzi wa Saccos Yao na pia ndugu zetu wa Benki ya Azania wameonyesha nia ya kudhamini mafunzo hayo"amasema.
Hamad Bendera mwenyekiti wa chama cha Madereva wa Bajaj na Bodaboda mkoa wa Kilimanjaro na mwenyekiti mwanzilishi wa Saccos hiyo anasema kuanzishwa kwa Saccos hiyo kutawajengea wanachama wao uwezo wa kujiwekea Akiba na kuondokana na dhana ya kutokopesheka.
Moja ya manufaa makubwa ambayo vijana Hawa watayapata kupitia Saccos Yao ni kuingia mkataba na LATRA wa kusimamia zoezi la ukataji wa stika za Bodaboda na Bajaj ambako watalamba aslimia 20.
Hii ni Saccos ya kwanza kabisa kuwahi kuanzishwa kwa pamoja kwa makundi haya vijana na pengin Itafungua njia kwa Mikoa minngine,asanteni sana LATRA Kilimanjaro kwa maono hayo
 
Back
Top Bottom