Serikali na CCM wawaeleze Watanzania bara/ Watanganyika sababu na faida za muungano kwa hoja nzito

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
38,098
47,095
Raia wengi wa Tanzania bara au kama wengine wanavypenda kujiita Watanganyika ni kama vile hawaelewi faida za muungano, hawafahamu wananufaika vipi na huu muungano. Kila mara ambapo hoja za muungano zinaibuliwa wanachama wengi wa chama tawala huwa wanapenda kusema tutaulinda muungano na kurudia rudia kauli ya Nyerere kwamba " ...... nje ya Muungano hakuna Wazanzibari. Nje ya Muungano kuna wao Wapemba sisi Waunguja..."

Hii misemo na nukuu bado haikidhi au kutoa majibu kuhusu faida za muungano kwa Watanganyika/Watanzania bara kwa sababu wao hawajali kama Wanzanzibar watabaguana. Pia kuna mifano ya nchi nyingi ambazo hazikuwahi kuungana kabisana hizo nchi hazina ubaguzi.

Yapo mambo mengi yasiyo rasmi yanasemwa kuwa ni sababu za Nyerere na Karume kuunganisha hizi nchi mbili, sasa ni wakati sahihi na muafaka wa serikali na chama tawala ambacho kiliuasisi huu muungano wajitokeze hadharani waseme hasa sababu na manufaa ya huu muungano wakati huo na wakati wa sasa. Vinginevyo wakiendelea kukaa kimya au kuja na hoja dhaifu za ubaguzi basi kelele za kuuhoji huu muungano zitazidi kuwa kubwa kadri muda unavyokwenda mbele hasa kwa vijana ambao hawakuzaliwa wakati wa huu muungano.
 
Sasa ndo lile zombie pale magogoni na chama chake lituambie faida za muungano kwa tanganyika maana tunaona vitu vinapigwa mnada tu na kujazana wazanzibar hata kwenye vitu sio vya muungano
 
Back
Top Bottom