Serikali kuwahakiki upya watumishi wake

Serikali kuwahakiki upya watumishi wake

Hili jambo linachosha hapa nchini.Kwanini wasiwatumbue waliosababisha wa kwepe kwenye uhakiki wa kwanza.
 
Kama TISS nao wameunganishwa katika ' Team ' ya wakakuaji na uhakiki wa Vyeti tayari safari yangu ya kupewa sana ' Ofa ' ya Bia na Washikaji zangu wawili naiona inaenda kufikia tamati kwani kwa ninavyowajua kuwa wote wawili wana Vyeti Feki halafu ile ya mara ya Kwanza walipona kwakuwa niliwapeleka kwa Mganga mmoja hatari sana huko Tanga ambaye sasa amefariki / amekufa. Nawaonea sana huruma Wake zao ambao walikuwa wakiwatambia sana Wanawake wenzao katika Mitaa yao wanayoishi huku wakiwa na Nyodo / Maringo kibao.
ujiandae kunywa balimi ama viroba vya kupima 500 au 1000 utaridhika mkuu.Hali hii itakuwa ni ya hatari na itaitingisha nchii maana mzee mwenye mjengo wake tayariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Aisee udanganyifu mkubwa ulifanywa pale kwa mtumishi "kujiendeleza"....yaan mtu alienda kujiendeleza kwa cheti kisicho chake......Akapata cheo.

Ukaguzin wakwanza ,akakificha icho cheti kilichomfanya akajiendeleze[emoji23][emoji23]......kuna watu kaguzi zote zaawali walipona , ila hii sasa hamna chakupona!!!.

Wapo walotumia vyeti vyao, ila wakaenda kuvichezea kwa ma IT , chet kikasoma A A B B B......hawa nao hawaponi.

Wapo walonunua vya watu ,alafu wakavichezea kwa ma IT wakaweka majina yao..hao pia kwaheriii.

Ivi navyozungumza, Hospital moja ya mkoa mmoja hapa hapa tanzia.... Madaktar kadhaa na manesi kwa aina zao wapatao wanne ,wametemeshwa mzigo ijumaa ilopita!!!.


Aiseee Jamaa kaamua kuhusisha TISS na NECTA ,NACTE ,na TCU .... Kwasababu hiyo ......... Namim nahisi kabisa Kilichotokea Hospital hii, ndio kimefanya Zoezi lianzwe upya kwa kushirikisha Izo Taasisi nyeti.

Hata ivo ,usumbufu ni usumbufu tuuu..kufukua fukua makaburi yann bana.
Nyumba za serikali zilizouzwa mbona hazihakikiwi kama ziliuzwa wa watu sahihi?
 
Kama vyeti vyako vina utata wa aina yoyote na umefanya kazi zaidi ya miaka mitano na hujajitengenezea utaratibu mwingine wa kuishi pasipo hiyo kazi, Tafakari uwezo wako wa kufikiri.
 
Hii ni agenda ya serikali kukimbia kuongeza mishahara..yaani awaam yote ya 5 inaishia kwenye kuhakiki wafanyakazi

Bila hata kufanya ongezeko la mishahara
Ndio ninachoona. Kuna group la qatu wanatafutwa.
 
Ni hivi kweli kuna zoezi la vyeti fake, lakini ukweli halisi ni redundancy kutokana na hali mbaya ya kifedha ya serekali. Kama ni vyeti fake kweli tutaona nafasi zao zikijazwa. Uchumi uko hoi sera mbovu ndio matunda yake haya.
Hili hawataki kuweka wazi. Kuna watu watabambikiwa kesi hapa za vyeti feki ili tu wapunguze watu.
 
Pia Mwenye Nchi nashauri kusiwepo na 'double standards' ktk hili
Au kuacha vyombo vya ulinzi na usalama
Kagueni Watumishi wote tu to be fair
 
Wakitaka zoezi liende vizuri waanzie kwa DAB
 
Na hasa ukionekana una vielementi vya ukawa huko kazini kwako.
Ndio wanakuzika kabisa. Kuna mchiz wangu anafanya kaz ofic ya RC alaf ni kada maaruf wa chadema.. namuona kama vile akiwa amenasa kwenye mtego..
 
Serikali imeanza tena kuwa frustrate wafanyakazi wa umma. This is amazing
Yaani hiki kisingizio cha kuhakiki ndio kila mahali. ni kichaka ambacho serikali inatumia ili kukwepa majukumu yake. lakini kijamii wala siyo zoezi zuri. UDSM kuna maprofesa wameondolewa kisa cheti cha form iv!! hii ina utata mkubwa. suala la cheti cha form iv kuwa na utata haliondoi uwezo wa mtu kwamba amewezakufikia ngazi aliyofikia. kisosholojia, ilitakiwa hili zoezi lisiwepo kabisa. lakini kwa kuwa wanaosimamia hawana DNA ya ubinadamu, matokeo yake ndiyo hayo
 
Back
Top Bottom