Kama mada inavyojieleza hapo juu
Serikali ya JMT imeanza tena lile zoezi la kuwahakiki upya watumishi wake ambapo kwa awamu hii imedhamiria kuwadaka wale wote walioleta udanganyifu katika zoezi lililofanyika hapo awali.
Aidha katika awamu hii uhakiki huo haufanywi tena na maafisa utumishi wa idara zote za Serikali kama ilivyokuwa awali, ila tuu jukumu hilo limebebwa na kikosi kazi maalumu kilichoteuliwa na Rais wa nchi hii kikiwaunganisha baadhi ya maafisa kutoka UTUMISHI ,TISS NECTA,NACTE pamoja na TCU.
Zoezi hili limeshaanza katika taasisi mbalimbali ambapo idadi kamili ya watumishi waliobanika kufoji vyeti na kuleta udanganyifu katika zoezi la awali itaekwa bayana na mamlaka zinazohusika.
MY TAKE
Wakuu kwa uhakiki huu hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe.kama ulileta ujanja ujanja mwanzoni sepa kabla hawajaja ofisini kwako.
Nitaleta idadi rasmi ya taasisi zilizokumbwa na dhoruba hili hivi punde.