Serikali Kutumia Bilioni 30 Kujenga Taasisi ya Moyo Mloganzila

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Ujenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika hospitali ya Mloganzila unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka 2023 ambapo utagharimu Sh30 bilioni, mpaka kukamilika kwake.

Kimsingi jengo hilo jipya, litafanana nan a jengo la sasa ambalo lipo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), na kwamba litakuwa na vitanda zaidi ya 300.

Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Oktoba 28, 2023; na Mkuu wa Kitengo cha Uhakiki wa Ubora, Dk Naizihijwa Majani, wakati akizungumza na wanahabari baada ya kuwa wametembelewa na ujumbe toka ubalozi wa Chini nchini.

Dk Majani amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo jipya pale Mloganzila, utafanyika kwa ushirikiano na watu wa China kama ilivyokuwa kwenye jengo mama la JKCI pale MNH.

Aidha amesema taasisi hiyo kwa siku inahudumia wagonjwa wa nje 500 na wagonjwa wa upasuaji 400 ambapo wameongezeka kutoka 100 kwa mwaka,hivyo ujenzi huo utakapokamilika utasaidia utoaji wa huduma kwa watu wengi zaidi.

"Kwa sasa hatuwezi kuongeza upasuaji wa wagonjwa zaidi ya 400 kutokana na idadi ya vitanda vilivyopo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), hivyo ujenzi utakapokamilika tutaweza kufanya upasuaji wa wagonjwa zaidi ya hapo," amesema Dk Majani.

Dk Majani amesema mpango uliopo kwa sasa ni kutoa huduma ya magonjwa ya moyo kwenye hospitali za Kanda ambazo ni pamoja na Hospitali ya Bugando Mwanza, Benjamini Mkapa Dodoma na ile ya Chato.

Amesema matarajio ya JKCI baada ya miaka mitatu ni kuona huduma ya magonjwa ya moyo inatolewa nchi nzima na wananchi wengi wataweza kupata matibabu ya moyo.

Kaimu Mkurugenzi wa JKCI, Dk Tatizo Waane amesema Serikali imekuwa na ushirikiano na China katika masuala mengi ya taifa na katika sekta ya afya kumekuwa na ushirikiano wa mabadilishano ya wataalamu baina yao na China hususani katika upasuaji wa moyo kwa watoto.
 
Back
Top Bottom