Serikali kurekebisha Sheria ya Watoto ili kudhibiti ukatili mitandaoni

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
FUAD-wzWIAEWrw_.jpg

Katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto mitandao Serikali imeunda kikosi kazi cha taifa cha ulinzi na usalama mitandaoni pamoja na kuifanyia marekebisho sheria ya mtoto ili iakisi mazingira ya sasa.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Dkt. Dorothy Gwajima amesema: “Malezi bora katika familia imekuwa mtihani tena mtihani kwelikweli. Wazazi wa Tanzania tuache kuwakatili watoto, ukiona ana utukutu mpeleke ustawi wa jamii, ukimpiga ukamuumiza utakutana na sheria ya mtoto, vinginevyo mzazi ajiandae kupambana na sheria ya mtoto.”

Ameyasema hayo Bungeni leo Jijini Dodoma, Mei 30, 2022 wakati akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
 
Back
Top Bottom