Serikali kununua ndege nyingine ya Boeing 787

Serikali kununua ndege nyingine ya Boeing 787

Shirika la ndege sio tu ni muhimu ni lazima, kilimo sio tu ni muhimmu ni lazima pia, tunaweza tukafanya vyote kwa wakati mmoja. Kila mwaka kuna budget inatengwa kwa ajiri ya kilimo, suala ni je wizara husika watuambie wanapata kiasi gani na wanaifanyia nini, tunaweza tukasema kilimo kimesahaulika kumbe pesa zinakwenda wizarani kufanya kazi ambazo hazieleweki, wizara waje na mpango mzuri wa kilimo na watueleze jinsi watakayvotekeleza kwa kipindi fulani, hii ni wizara ambayo haifanyi vizuri kwa kisingizio cha pesa, hata hao ATCL walikuwa na mchakato wa muda mrefu kufufua shirika hilo ,wakaja na mpango wa nini kifanyike na jinsi watakavyofanya biashara hiyo na kurudisha pesa kwa wakati, sasa huwezi chukua pesa nyingi ukaziweka sehemu ambapo hakuna plan, mfano kilimo kwanza baada ya kuinua kilimo ilikuwa kichaka cha watu kuiba pembejeo, wajanja wakafaidika at the same time mkulima akaendelea kuumia ,at the end of the day kilimo kwanza tukaizika.
 
Umeongea logic na point Sana mkuu.Ila tambua pia ya kwamba serikali haifanyi kwa mtu mmoja mmoja ila majority.Unapowekeza kwenye airline sio mbaya at all coz inaboost sekta ya utalii Sana kwasababu huwezi kufanikiwa kwenye utalii without a stable airline company ambayo itaitangaza nchi ughaibuni.Mind you utalii utaongeza fedha za kigeni ambazo Zita boost uchumi pia in one way or another.So kenya,Rwanda Ethiopia sio wajinga kuinvest kwenye airlines companies mkuu.
Halafu jingine, mi natamani watu wajifunze ama wajue tu juu ya mifumo ya kiutawala nchini. Kwamba kuna mamlaka ya serikali kuu na mamlaka ya serikali za mitaa. Wakiujua huu mfumo, hatutakuja kusikia tena mtu wa levo ya kijiji akimwambia Rais juu ya barabara, pembejeo, maji nknk ataishia tu kwa diwani wake.
 
Jambo jema sana, ila naiomba serikali isilipe cash hata kama fedha inazo

Serikali iwalipe watengenezaji mara tu zitakapo wasili Tanzania

Huwa nina hisia kuwa malipo ya cash kwa ndege zilizopita nayo yamechangia kukamatwa kwa moja ya Bombadier yetu

Niko tayari kurekebishwa kama ninakosea
Hivi nyie mnafikiri process ya kununua ndege ni kama kununua vitumbua kwa mama Chausiku?
 
Hii Habari asiisikie Tundu Lissu vinginevyo watamrudisha ICU, kwa chuki aliyonayo dhidi ya nchi yetu!
Mkuu Barbarosa nimeipenda sana hii comment yako, hata mimi nilitaka kuandika hivyo hivyo. Jamaa ana chuki sana na nchi hii, kwake yeye hakuna jema linalofanyika.

Tundu Lissu huwa anajifanya anajua sana kila kitu lakini ukitembelea jimbo lake hakuna chochote cha maana alichokifanya.
 
Sawa nakubaliana na wewe chief ila awamu iliyopita c iliweka mkazo kwenye kilimo kwa kauli mbiu ya kilimo kwanza?lakini what happened?hebu tujaribu na huku kdgo mkuu tuone.

Toka awamu ya kwanza i.e. post-Nyerere Tanzania, serikali haijawahi KUWEKEZA kwenye kilimo. Usidanganyike na kauli mbiu za kilimo kwanza na BRN. Ule ulikuwa usanii. Uwekezaji, nimesema haujawahi kufikia asilimia 10 ya national budget.

Maendeleo hayajaribiwi chief. Ni kufanya tu kwa mipango na vitendo. Yaani ninachokisema ni no brainer.

Umaskini kuisha itakuwa ni ndoto kama hakuna UWEKEZAJI kwenye kilimo.

Unasema ‘tujaribu’ kwenye uwekezaji kwenye usafiri wa ndege. Kwenye taifa ambalo walio kwenye mfumo rasmi wa ajira na kodi ni wachache, hizo ndege zitazalishaje faida sasa? Maana wapandaji wapo wapi zaidi ya waajira baadhi (senior officials) wa serikali, waajiriwa wa sekta binafsi na wafanyabiashara?!?

Hakuna uchawi katika kumaliza umaskini endapo serikali inatenga bilioni 500 kununua ndege, huku ikiweka bilioni 24 kwenye kilimo (15B ikiwa fedha ya wafadhili)!!!

Uwekezaji uliofanyika so far umezalisha nini? Maana financial reports za mashirika ya umma ni siri ati!!
 
Sekta ya kilimo
Sawa mkuu.nakubali ila kumbuka tulishakijaribu hiko na kauli mbiu kilimo kwanza.kinachohitajika kwasasa ili kilimo kiibuke ni lazma kuwe na mkakati madhubuti ambao ukiwa implemented utakua na positive impact to our economy mkuu.Ila sio kukurupuka kwa kuweka mahela ambayo yataliwa na wajanja wachache kwenye sekta hiyo ya kilimo Kama ilivyotokea awamu iliyopita kwa sera ya kilimo kwanza ambayo hundred percent ili fail.
 
Tundu Lissu huwa anajifanya anajua sana kila kitu lakini ukitembelea jimbo lake hakuna chochote cha maana alichokifanya.

Sasa Lissu yeye ndiye mkusanya kodi? Yaani umaskini na kutokuwepo maendeleo kwenye majimbo ni sababu ya wabunge ama serikali?

Kama budget disbursement haifiki hata asilimia 40 ya kile kilichotengwa, mbunge analaumiwaje hapo?

Kikwete amekuwa Rais kwa miaka 10, lakini Bagamoyo na Chalinze bado umaskini umetopea!! Magufuli kawa waziri na mbunge kwa miaka 20+ lakini hadi kesho watu wanateseka na umaskini na uduni wa huduma za kijamii hapo Chato.
 
Toka awamu ya kwanza i.e. post-Nyerere Tanzania, serikali haijawahi KUWEKEZA kwenye kilimo. Usidanganyike na kauli mbiu za kilimo kwanza na BRN. Ule ulikuwa usanii. Uwekezaji, nimesema haujawahi kufikia asilimia 10 ya national budget.

Maendeleo hayajaribiwi chief. Ni kufanya tu kwa mipango na vitendo. Yaani ninachokisema ni no brainer.

Umaskini kuisha itakuwa ni ndoto kama hakuna UWEKEZAJI kwenye kilimo.

Unasema ‘tujaribu’ kwenye uwekezaji kwenye usafiri wa ndege. Kwenye taifa ambalo walio kwenye mfumo rasmi wa ajira na kodi ni wachache, hizo ndege zitazalishaje faida sasa? Maana wapandaji wapo wapi zaidi ya waajira baadhi (senior officials) wa serikali, waajiriwa wa sekta binafsi na wafanyabiashara?!?

Hakuna uchawi katika kumaliza umaskini endapo serikali inatenga bilioni 500 kununua ndege, huku ikiweka bilioni 24 kwenye kilimo (15B ikiwa fedha ya wafadhili)!!!

Uwekezaji uliofanyika so far umezalisha nini? Maana financial reports za mashirika ya umma ni siri ati!!
Upo sahihi blaza asilimia 100% ila sasa kinachotakiwa hapa ni seriousness tu ili kuibua kilimo.Nachomaanisha mkuu kuwe sasa na mpango mkakati kwa ajili ya kuibua kilimo ili mpango uje kua na positive impact to our economy
 
Badala yakuongeza mishahara na kuboresha masirahi ya watumishi wa umma ili kuimprove work moral mnanunua mindege,ndio manainakamatwa nakuachwa inapgwa na jua,laana ya watumishi ya manung'uniko ya watumishi wa umma haitawaacha sarama.
Nahisi wew ni mtumishi shukulu unalipwa kwa mwezi je na sisi tusio watumishi je kama acheni pisheni wengine
 
Upo sahihi blaza asilimia 100% ila sasa kinachotakiwa hapa ni seriousness tu ili kuibua kilimo.Nachomaanisha mkuu kuwe sasa na mpango mkakati kwa ajili ya kuibua kilimo ili mpango uje kua na positive impact to our economy
Serikali ya Magufuli ndiyo haina huo mpango mkakati! Kilimo kimetelekezwa ili nchi iwe na ndege!!
 
Ni yaleyale tuliyodanganywa canada kuwa ni ndege kumbe mafeni!??
 
Hizi ndege zinazokuja zote wanapanda mbuzi? Emirates,FlyDubai,Ethiopian,Kenyan,Qatar,KLM,SwissAir hizi zote zikija hapa wanapanda mbuzi au?
Watu akili zao zimeishia Moshi na Morogoro. Wanadhani China watu wanaenda na Dar express hahahahahaa
 
Back
Top Bottom