Serikali iweke vipaombele, sekta kubwa inayoingizia taifa mapato mengi na kuajiri watu wengi ni kilimo, fedha zote hizo za hizo ndege kama Mungu angewafungulia fikira hawa viongozi wetu wakawekeza kwny kilimo hasa pembejeo na umwagiliaji, leo hii wanyonge wengi sana wangepata neema kubwa na uhitaji wa viwanda ungekua kwa kasi ya ajabu. Lakini wapi bhana, mtu mweusi hata asome vp fahari yake ipo kwny vitu, yaani magari, nguo, majumba nk.
Nchi hii hv sasa hatujui hasa dira yetu ni ipi kwny uchumi, Rwanda nawaelewa sana wamejikita kwenye ICT na conference facilities kutokana na mazingira ya nchi yao ndogo, na wanayo haki ya kukuza shirika lao la ndege kutokana na hiyo dira ya pili kuwa centre ya mikutano mikubwa Africa mashariki na kati. Sasa hapa kwetu safari tunayo, huyu akiondoka yule atakaye kuja ataturudisha pia sehemu tofauti na hayo mandege yaani hakuna muendelezo. Aliyetoka alisema Kilimo kwanza, huyu kaja anasema kazi tu, ipi hasa haijulikani ni fully mseto