Serikali kununua ndege nyingine ya Boeing 787

Wanasahau kilimo wako busy kununua ndege wanasahau hiyo ni biashara kama biashara zingine hivyo inapaswa kwenda nayo taratibu na kwa uangalifu.

Hizi Bomberdier mbili zilizopo hata hatujui perfomance ikoje maana hata utoaji wa taarifa zake haueleweki.
Hata utoaji taarifa ungeeleweka bado usingekufurahisha
 
Serikali ya Tanzania ipo katika hatua za mwisho kununua ndege nyingine ya Boeing 787.

Itakumbukwa ya kwamba serikali washa-order ndege nne, ambazo ni Boeing787, CS300 na Bombardier q400, ndege zote Zitawasili July mwaka huu.

Source: Aviation Tanzania
Hongera JPM, ila naomba turekebishe mambo ili ile Bombardier Q400 iliyokamatwa iachiliwe, halafu hizi mpya tunazonunua zisikamatwe.Otherwise tutakuwa tunapiga mbio za sakafuni.
 
Hili ni jambo zuri kwa serikali kwenye dhamira yake ya kufufua shirika letu la ndege, lakini vilevile lazima ijitahidi kugusa sehemu kubwa ya uchumi ambao unagusa(unamilikiwa) wengi hasa kwenye sekta ya kilimo na viwanda ingependeza sana kama serikali ingejikita intensively kusaidia kuinua kilimo hasa wakulima wadogowado na kuwatafutia masoko ndani na nje ya nchi.

Japo hili linalofanywa na serikali nalo lina mchango wake kwenye ufufuaji Wa uchumi hongera mh.raisi kwa kufufua hili shirika ambalo lilishafariki.
Hilo unalosema ni sahihi. Lakini kwa miaka 50 approach yetu ilikuwa hiyo na tumeshindwa kuinua uchumi. Sekta hizi za kibiashara na zinazochochea uchumu kukua ni mhimu kuudumiwa ili tupige hatua. Tuhakikishe tu kuna usimamizi sahihi na mipango bora. Tusikurupuke
 
Hi Sharif muogope mungu kutumia neno ukafiri kwenye chombo cha habari si vizuri watu wanaona wametukanwa japo kidini umemaanisha MTU asieamini lakini kwa Kiswahili ni tusi kama matusi mengine Na kisheria unafungwa Na kivingine pia kidini ni dhambi ni sawa Na kwenda kwa jirani yako ukaanza kutukana wakikupeleka mahakani huponi Na hadithi ya mtume i nasema yeyote anaemuudhi MTU jirani au hata njiani kwa makusudi hata kama si muislamu anapata dhambi
 
siyo kwa ukosoaji wa kilofa kama wenu!
Sikuzote kinachouma ni lazima kionekane cha kilofa. Kama tungewasifia hizo blanda zenu mnazozifanya, hizo sifa msingeziona kuwa ni za kilofa, bali mngeziona ni za maana sana maana kusifiwa sikuzote ni kutamu kama asali, bali kukosolewa ni kuchungu kama muarubaini. Sasa kubalini uchungu unaowazindua na kuwawezesha kujirekebisha kuliko sifa zinazowapumbaza na kuwadumisha kwenye blanda zenu.
 
Ni mpaka hapo tutakapoiona. Awamu hii inajua rusha roho sana!
 
Wanasahau kilimo wako busy kununua ndege wanasahau hiyo ni biashara kama biashara zingine hivyo inapaswa kwenda nayo taratibu na kwa uangalifu.

Hizi Bomberdier mbili zilizopo hata hatujui perfomance ikoje maana hata utoaji wa taarifa zake haueleweki.
Unawaza kama Mimi vile. Kama Tanzania Tunataka kupiga hatua, basi kilimo ndiyo kingepewa kipaumbele cha kwanza.

Serikali kupitia wawekezaji, aidha kutoka Uchina au Israeli, ingeanzisha kilimo cha umwagiliaji nchi nzima. Na hii inawezekana kwa 7bu Nchi yetu imejaaliwa kuwa na vyanzo mbalimbali vya maji kama vile maziwa (ziwa vikitoria, Nyasa, Tanganyika, Rukwa), bahari ya Hindi na mito kama vile mto Ruaha, n.k.

Kupitia kilimo, Tanzania ingepata manufaa makubwa zaidi kuliko inayoyapata sasa kupitia vipaumbele vyake, mfano uwekezaji ktk safari za anga, ujenzi wa reli (standard geji), ukusanyaji wa mapato, n.k.

Faida kubwa ambazo Tanzania ingezipata kama ingewekeza kwenye kilimo ni pamoja na kuongeza ajira kwa vijana, uzalishaji wa Mali ghafi za kutosha kwa ajili viwanda ambavyo inavianzisha na kuvifufua sasa, kuongezeka kwa mapato ya serikali kutoka kwa wawekezaji, kuinua kipato cha wananchi wa hali chini, n.k.

Tungejifunza kutoka kwenye Nchi ambazo zimeendelea kutokana na Kilimo, mfano Uchina. Kwa uelewa wangu mdogo tu, zaidi ya 85% ya Watanzania wanaishi kijijini ambako ajira yao kubwa ni Kilimo. Kwa hiyo unapozungumzia uwekezaji ktk sekta ya kilimo unazungumzia ajira ya uhakika kwa waTanzania zaidi ya 85%.

Nashauri, Serikali iiangalie upya sekta hii ya Kilimo kama inataka kutekeleza Sera yake ya "Nchi ya Viwanda" na "Uchumi wa kati" kwa vitendo.
 
Serikali ya Tanzania ipo katika hatua za mwisho kununua ndege nyingine ya Boeing 787.

Itakumbukwa ya kwamba serikali washa-order ndege nne, ambazo ni Boeing787, CS300 na Bombardier q400, ndege zote Zitawasili July mwaka huu.

Source: Aviation Tanzania
Ile ingine iko wapi??? Mbona haifiki
 
Wanasahau kilimo wako busy kununua ndege wanasahau hiyo ni biashara kama biashara zingine hivyo inapaswa kwenda nayo taratibu na kwa uangalifu.

Hizi Bomberdier mbili zilizopo hata hatujui perfomance ikoje maana hata utoaji wa taarifa zake haueleweki.
Unapanda ndege mara ngapi kwa mwezi, kwa safari za ndani?
 
Unawaza kama Mimi vile. Kama Tanzania Tunataka kupiga hatua, basi kilimo ndiyo kingepewa kipaumbele cha kwanza.

Serikali kupitia wawekezaji, aidha kutoka Uchina au Israeli, ingeanzisha kilimo cha umwagiliaji nchi nzima. Na hii inawezekana kwa 7bu Nchi yetu imejaaliwa kuwa na vyanzo mbalimbali vya maji kama vile maziwa (ziwa vikitoria, Nyasa, Tanganyika, Rukwa), bahari ya Hindi na mito kama vile mto Ruaha, n.k.

Kupitia kilimo, Tanzania ingepata manufaa makubwa zaidi kuliko inayoyapata sasa kupitia vipaumbele vyake, mfano uwekezaji ktk safari za anga, ujenzi wa reli (standard geji), ukusanyaji wa mapato, n.k.

Faida kubwa ambazo Tanzania ingezipata kama ingewekeza kwenye kilimo ni pamoja na kuongeza ajira kwa vijana, uzalishaji wa Mali ghafi za kutosha kwa ajili viwanda ambavyo inavianzisha na kuvifufua sasa, kuongezeka kwa mapato ya serikali kutoka kwa wawekezaji, kuinua kipato cha wananchi wa hali chini, n.k.

Tungejifunza kutoka kwenye Nchi ambazo zimeendelea kutokana na Kilimo, mfano Uchina. Kwa uelewa wangu mdogo tu, zaidi ya 85% ya Watanzania wanaishi kijijini ambako ajira yao kubwa ni Kilimo. Kwa hiyo unapozungumzia uwekezaji ktk sekta ya kilimo unazungumzia ajira ya uhakika kwa waTanzania zaidi ya 85%.

Nashauri, Serikali iiangalie upya sekta hii ya Kilimo kama inataka kutekeleza Sera yake ya "Nchi ya Viwanda" na "Uchumi wa kati" kwa vitendo.

Kilimo bila ya usafiri mazao yataozea shamba. Magufuli yuko sawa. Jiulize kwanini mashamba mengi yapo karibu na barabara. Na kuna ndege za mizigo pia. Masaa matatu nyanya zimeruka Bukoba-Dar.
 
Hakuna Aliyesema hayuko sawa kama umesoma neno kwa neno ktk maoni yangu.
 
Ukiangalia comments nyingi humu jamiiforum siku hizi unagundua wale wajinga wa instagram na facebook ndo wamevamia ila the great thinkers hawamo tena.
Tusubiri week ijao shule zitafunguliwa watuachie jukwaa letu
 
Serikali ya Tanzania ipo katika hatua za mwisho kununua ndege nyingine ya Boeing 787.

Itakumbukwa ya kwamba serikali washa-order ndege nne, ambazo ni Boeing787, CS300 na Bombardier q400, ndege zote Zitawasili July mwaka huu.

Source: Aviation Tanzania
Labda ndege za kuchezea watoto
 
Kwa mtazamo wangu mimi ndege, treni, magorofa na vingine vinavyofanana na hayo ni vitu vidogo sana na visivyo na thamani kuliko utu, heshima, haki, usawa na vinavyofanana na hayo. Utu wetu unathamani kubwa sana kuliko kuliko magari ya kifahari na ndege. Hivyo utu kwanza mengine yote chini ya uongozi wa makini yatawezekana tu.
 
Back
Top Bottom