Tunaweza fanikisha hata kwa wakati huu wa sasa. Siyo lazima tufanye sisi, kwenye comment yangu hiyo nimeshauri kwamba tunaweza kuwa na Viwanda hivyo hata kwa Kupitia Wawekezaji, ambao tayari Wana uwezo wa kujenga viwanda vya kuunda ndege.
Kumbuka ili uwekezaji wa masuala ya teknolojia ufanikiwe...ni lazima-
1.Kuwepo na wasomi husika wa kutosha
-wahandisi,wanauchumi,wabunifu
-tuwe wanafiti wabobezi

2.Mifumo bora ya usafirishaji
-Reli,Barabara za kutosha, Bandari

3.Mifumo bora ya mawasiliano
-Intaneti yenye kasi,Mitandao ya simu

4.Mifumo bora ya Uchumi
-Soko la hisa
-Mabenki
-Mifuko ya uwekezaji

5.Umeme wa uhakika
-Hivyo viwanda vinakula umeme si kitoto.

Sasa hapo mkuu,hakuna hata moja ambalo tupo vizuri.Ila kwenye elimu ndiyo kabisaa.
Hakuna muwekezaji atakayetupa hela zake kama nchi haina hivyo vitu.
Yani yeye aje na kila kitu,wewe utoe ardhi tu,hiyo itakuwa biashara ya matikiti.
 
Tunaweza fanikisha hata kwa wakati huu wa sasa. Siyo lazima tufanye sisi, kwenye comment yangu hiyo nimeshauri kwamba tunaweza kuwa na Viwanda hivyo hata kwa Kupitia Wawekezaji, ambao tayari Wana uwezo wa kujenga viwanda vya kuunda ndege.
Zitauzwa wapi?

Wasichojua wengi ni kuwa hizi kampuni kubwa za uundaji ndege (Boeing, Airbus) shughuli zao kubwa ni za biashara, masoko na fedha. Wana kampuni tanzu kubwa za maeneo hayo. Huko ndiko wanakokutana na wateja wa kila aina: wanaokopa, wanaokodi, wanaoazima, wanaodunduliza, wanaonunua kwa mali kauli na wachache wanaonunua kwa cash. Kazi kubwa ndiko inakofanyika. Wateja wa cash si wa kawaida na order zao ni ndogo; hazisumbui. Zinawasilishwa viwandani chap chap. Wateja wazito ndio mijadala inafanyika kwa undani ikihusisha namna mbalimbali (complex) za manunuzi ndipo order ziwasilishwe viwandani. Ndege hazinunuliwi kama V8. Hakuna showroom kiwandani wala kwenye matawi ya kampuni.

Kwa mfano, Ethiopian Airlines mwaka huu wameweka order ya Boeing 777X ishirini (20). Mwaka jana 2023 ET waliagiza Boeing 787-10 kumi na moja (11) na Boeing 737-Max ishirini (20). Wanachofanya ni kuandaa mpango wa biashara uliohakikiwa na kuuwasilisha kwenye kampuni ya biashara, masoko na fedha ya Boeing na kujadili mahitaji ya ndege, aina zake, namna ya manunuzi na ratiba ya upatikanaji. Pesa inayotolewa cash ni kidogo sana. Marejesho makubwa yanatarajiwa kutoka kwenye mtiririko wa mapato kibiashara. Boeing wana uzoefu wa miaka mingi ya biashara na ET. Hawana tatizo na marejesho yao kibiashara.

Sisi labda kama tunataka kuwa factory mojawapo ya Boeing, Airbus, Embraer n.k. Kitu ambacho si rahisi. Hizo kampuni zinaangalia hali ya nchi na mfumo wake mzima wa kiuchumi, kibiashara, kielimu, kiteknolojia, kisiasa, n.k. Siioni Tanzania hata kufikirika katika jambo kubwa hivi.

Tupambane kwanza kuondoa aibu ya kujengewa matundu ya vyoo kwa msaada wa watu wa Marekani.
 
Hiyo ndege engineer wa boeing wenyewe hawaipandi ...ila huku kwetu sasa
 
Badala ya kuendelea kuwa na mawazo au fikra potofu kila wakati za kununua ndege mpya kutoka ktk viwanda vya nchi za nje, nadhani umefika wakati sasa wa kufikiria kuwa na kiwanda au viwanda vyetu weyewe vya kuunda ndege hapa hapa nchini kwetu Tanzania. Tuwe na wazo kama hili, hata kama sisi wenyewe bado akili zetu hazijawa kubwa kuweza kuwa na viwanda vya namna hii, basi tuanze hata kwa kuwakaribisha wawekezaji kutoka nje ya nchi, tunaweza kuingia nao mikataba maalumu ya uwekezaji wa namna hii. Viongozi wa nchi hii wawe na Maono Mapana ili wayaone haya mambo mazuri kwa mustakabali mwema wa nchi hii.
Ile helcopter yetu ya Arusha Tech iliishia wapi
 
Mama c alishasema hizi ndege zinaingiza hasara lkn bado zinaletwa ili mradi tu kuna viongozi wapige pesa hapo.
 
Kumbe pesa tunayo ya kuinunua ndege. Ila pesa ya kusaidia lishe watoto hatuna mpaka tukaombe msaada marekani wa Mchele wenye virutubisho.
 
Boeing 737 max tena? Pamoja na matatizo kibao ya hizo ndege bado tunaendelea. Kununua ndege za boeing!!
Kuna kundi la watu Inawezekana wana maslahi na manunuzi ya hizi ndege Sio biashara kama tunavyodhani
 
Badala ya kuendelea kuwa na mawazo au fikra potofu kila wakati za kununua ndege mpya kutoka ktk viwanda vya nchi za nje, nadhani umefika wakati sasa wa kufikiria kuwa na kiwanda au viwanda vyetu weyewe vya kuunda ndege hapa hapa nchini kwetu Tanzania. Tuwe na wazo kama hili, hata kama sisi wenyewe bado akili zetu hazijawa kubwa kuweza kuwa na viwanda vya namna hii, basi tuanze hata kwa kuwakaribisha wawekezaji kutoka nje ya nchi, tunaweza kuingia nao mikataba maalumu ya uwekezaji wa namna hii. Viongozi wa nchi hii wawe na Maono Mapana ili wayaone haya mambo mazuri kwa mustakabali mwema wa nchi hii.
Bajaji tu hamuwezi kutengeneza, mnawaza ndege?
 
Kisa kununua ndege JPM alisemwa ni mshamba ati wananchi hawataki maendeleo ya vitu bali ya watu. Inashangaza sana bado vitu vinanunuliwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom