Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
347
462
Ndege mpya ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Boeing 737-9 Max, inatarajiwa kuwasili nchini Machi 26 mwaka huu kutokea nchini Marekani, hii itakuwa ndege ya 14 kutoka ATCL.

images (99).jpeg
 
Mnakomaa kununua ndege, halafu kila mwaka mkifunga hesabu zenu mnakutana na hasara tu! Halafu bado hamkomi!

Badala ya kuziunganisha barabara zote za Mikoa nchini kwa kiwango cha lami, ili kuwarahahisishia wananchi usafiri wa uhakika na wa bidhaa zao! Mko busy kununua vitu vya kujifurahisha nyinyi wenyewe!

Hii nchi imelaaniwa aisee! Hizo ndege waachieni sekta binafsi bhana! Nyinyi wekeni nguvu kubwa kwenye kutengeneza miundombinu rafiki kote nchini kama barabara za lami ili mpate kodi kwa urahisi! Na siyo kushindana na watu binafsi kufanya biashara!
 
Gonde jako mosie.
 
Ndege mpya ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Boeing 737-9 Max, inatarajiwa kuwasili nchini Machi 26 mwaka huu kutokea nchini Marekani, hii itakuwa ndege ya 14 kutoka ATCL.

Badala ya kuendelea kuwa na mawazo au fikra potofu kila wakati za kununua ndege mpya kutoka ktk viwanda vya nchi za nje, nadhani umefika wakati sasa wa kufikiria kuwa na kiwanda au viwanda vyetu weyewe vya kuunda ndege hapa hapa nchini kwetu Tanzania. Tuwe na wazo kama hili, hata kama sisi wenyewe bado akili zetu hazijawa kubwa kuweza kuwa na viwanda vya namna hii, basi tuanze hata kwa kuwakaribisha wawekezaji kutoka nje ya nchi, tunaweza kuingia nao mikataba maalumu ya uwekezaji wa namna hii. Viongozi wa nchi hii wawe na Maono Mapana ili wayaone haya mambo mazuri kwa mustakabali mwema wa nchi hii.
 
Wazo Zuri, tena zuri sana
Lakini mkuu dah, tusikimbilie suti wakati hata nepi bado.
Hebu tuanze kwanza na Viwanda vya mbolea, Saa, Radio, earphones, viatu na nguo.
viwanda vya kuchakata vito vya thamani na mazao.

Hayo madude makubwa hata India na mchina yanamtoa jasho.
Kipindi elimu ikiwa kipaombele cha Taifa ndiyo tuweke hayo mawazo mezani, ila kwasasa ni bado sana.
 
Kwani kwao ni mwanza?
Si itakuwa inampeleka dubenga na zenj daily?
Kupatwa kwa mama Tanzania
Andika hii: kuna mazingara yanawekwa sawa. Siku si nyingi shirika na ndege atapewa ''mwekezeaji'' kwa sababu ''sisi'' hatuwezi kuendesha. Bandari, kitu kitega uchumi kinachotema fedha kama mgodi wa almasi imetushinda ije kuwa shirika la ndege?
 
Wazo Zuri, tena zuri sana
Lakini mkuu dah ,tusikimbilie suti wakati hata nepi bado.
Hebu tuanze kwanza na Viwanda vya mbolea,Saa ,Radio ,earphones ,viatu na nguo.
viwanda vya kuchakata vito vya thamani na mazao.
Hayo madude makubwa hata India na mchina yanamtoa jasho.
Kipindi elimu ikiwa kipaombele cha Taifa ndiyo tuweke hayo mawazo mezani,ila kwasasa ni bado sana.
Tunaweza fanikisha hata kwa wakati huu wa sasa. Siyo lazima tufanye sisi, kwenye comment yangu hiyo nimeshauri kwamba tunaweza kuwa na Viwanda hivyo hata kwa Kupitia Wawekezaji, ambao tayari Wana uwezo wa kujenga viwanda vya kuunda ndege.
 
Kwenye hili la ununuzi wa ndege; mimi nipo kinyume na serikali.
Hapana, ndege hapana, tuna mengi ya kujiimarisha kwa ajili kukuza uchumi wetu; ndege hazina uhusiano wa moja kwa moja katika kumkomboa mwananchi wa kijiji Nambinda kiuchumi..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom