Yaleyale ya awamu ileeee yamerudi

Holly Star

JF-Expert Member
Aug 25, 2018
4,316
8,013
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imekanusha taarifa zilizoandikwa mitandaoni kwamba iliuziwa ndege hii ya Q300 Bombardier ikiwa tayari ‘imechoka’ ikiwa pia ni Ndege ya zamani ambayo ilishakosa vigezo vya kuendelea kuruka.

Baada ya kuandikwa mitandaoni kuwa pia Ndege hiyo imekwama Nchini Malta kwa miaka mitatu kutokana na kukosa spea, Kampuni hiyo imetoa taarifa yake leo na kusema kwanza Ndege hiyo sio miongoni mwa ndege mpya zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania katika kipindi cha Mpango wa Ufufuaji wa ATCL ulioanza mwaka 2016.

“Ndege hii haikununuliwa na Serikali bali ni miongoni mwa ndege mbili zilizopatikana kupitia Mbia aliyefanya uwekezaji kwa kuleta ndege mbili za aina ya Dash 8 - Q300 mwaka 2008 na kupewa usajili wa namba 5H-MWG na 5H-MWF kwa kufuatana, ndege hizo za Q300 ziliundwa mwezi Mei 1997 na kabla ya kuwasili nchini zilikuwa zimetumika kwa takribani miaka 11, hata hivyo Kampuni ya Bombadier (Manufacturer) ilisitisha uundwaji wake tangu Mei 2009” ——— imeeleza Taarifa hiyo.

“Ndege zilizonunuliwa na Serikali kuanzia mwaka 2016 ni ndege 13 ambazo ni Q400 – Bombadier (5), Airbus A220-300 (4), Boeing 787-8 (2), Boeing 767-300F (1) na Boeing 737 MAX – 9 (1), ATCL ilibakiwa na ndege ya Q300 moja yenye usajili wa namba 5H-MWF baada ya ndege yenye usajili wa namba 5H-MWG kupata ajali mwaka 2012 na kushindikana kutengenezeka kutokana na ukubwa wa uharibifu wa ndege hiyo”

“Ndege iliyobakia iliendelea na safari zake hadi mnamo Mei 2017 baada ya waundaji (Manufacturer) wa ndege hizi kuagiza kuwa ndege zote za aina hii duniani zisiendelee na safari hadi zitakapofanyiwa matengenezo ya lazima ya matenki ya mafuta kwa ajili ya usalama, sanjari na agizo hilo, ndege hii pia ilihitaji kufanyiwa matengenezo makubwa yanayojulikana kitaalamu kama “6C-Check” ambapo ilifika nchini Malta mwezi Novemba 2020 kwa ajili ya matengenezo hayo.

“Kutokana na changamoto ya upatikanaji wa vipuri iliyosababishwa na athari za UVIKO 19 ambapo wazalishaji wa vipuri walipunguza na wengine kuacha utengenezaji wa vipuri kumesababisha matengenezo hayo kutokamilika kwa muda uliotarajiwa, ndege hii inatarajiwa kurejea nchini baada ya kukamilika kwa matengenezo hayo, ATCL inawaomba Wadau wake kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa mitandaoni zenye lengo la upotoshaji” ——— imemalizia taarifa hiyo. #MillardAyoUPDATES
 
Afisa aliyetoa haya Maelezo amejibu mmaswali mengi sana. Hongera nyingi sana kwake. Maafisa habari wa TANESCO, TRA nk ambao mmewahi kujibu hoja za Umma nendeni ATCL mkajifunze namna ya kujibu vitu kama hivi.
Hongera sana kwa Idara ya Mawasiliano kwa Umma ATCL maelezo yana Viwango vya Weledi na Umahiri.
 
Hiya TanzaniaLeaks inakosesha watt usingizi sana. Huo mtandao nadhani ni watu wa NDANI ya serikali maana taarifa zao zinaogopesha na so deep
 
Kwahiyo upotoshaji ni upi? Mbona wamecomfirm kila kilichotuhumiwa
Upotoshaji ni kusema hiyo ndege ni miongoni mwa zile zilizo nunuliwa na serikali kupitia TGF kwa niaba ya ATCL wakati wa awamu ya raisi Magufuli.

Wakasema kwanini Magufuli alisema ndege mpya wakati ni mtumba?

Huo ufafanuzi umeeleza ndege ni mtumba kweli lakini siyo miongoni mwa ndege zile mpya. Pia hazikununuliwa wakati wa mpango wa kulifufua shirika enzi za Magufuli.

Soma aina (model) namba ya ndege pamoja na usajiri wa ndege na tarehe ya kununuliwa hizo ndege utaelewa upotoshaji ulikuwa wapi.
 
Upotoshaji ni kusema hiyo ndege ni miongoni mwa zile zilizo nunuliwa na serikali kupitia TGF kwa niaba ya ATCL wakati wa awamu ya raisi Magufuli.

Wakasema kwanini Magufuli alisema ndege mpya wakati ni mtumba?

Huo ufafanuzi umeeleza ndege ni mtumba kweli lakini siyo miongoni mwa ndege zile mpya. Pia hazikununuliwa wakati wa mpango kulifufuashirika enzi za Magufuli.

Soma aina (model) namba ya ndege pamoja na usajiri wa ndege na tarehe ya kununuliwa hizo ndege utaelewa upotoshaji ulikuwa wapi.
Aah, kumbe walisema hivyo, hapo wamepotosha
 
Back
Top Bottom