Serikali kukosa mchango wa dawa toka USAID

Serikali kukosa mchango wa dawa toka USAID

Hapa ndio turejee kauli ya rais kuwa hatuhitaji misaada, ilikuwa na uhalisia? Jamaa wakitukacha tutapoteana hapa nchini. Kwa hiyo kauli ya JK jana imepata nguvu zaidi.

Ka nchi ketu bado kachanga mno tusitunishiane misuli na magiant.

Hapa ni kuomba Mungu tu huo mradi wa pili uanze mapema kabla ndugu zetu hawajaishiwa dawa na kuanza kuharisha kama ilivyokuwa zamani mtu akiwa na ngoma
 

Comrade CHUAKACHARA, you are back....jibu la swali lako ni simple...kwenye taarifa hiyo ukisoma utaona inasema mradi huo wa USAID umefikia ukomo wake yaani miaka 10 tayari imefika, lakini kichwa cha habari kinasema USAID yasimamisha misaada, sasa hii inaleta picha tofauti kabisa...ushahidi wa gazeti la MWANANCHI upo kwenye uandishi wake..nazungumzia experience...na kumbuka au fahamu kuwa hili gazeti linamilikiwa na kampuni ya Kenya...
 
wamekata posho sasa watakata na mishahara ili kua na taifa linalojitegemea lisilohitaji misaada.
 
Hii habari haijakamilika.Lakini katika kujipanga huko kwa serikali bado hiyo ni divertion ya Resources kutoka mahali maana sidhani kama walijua hawataongezewa muda.Gharama bado anabeba mwananchi wa kawaida wakati hatukua tumejipanga.Maamuzi mabovu yanayosukumwa na uroho wa madaraka Mwananchi analipia gharama
Kaka we inaonekana hadi leo unanunuliwa hata chupi na wazazi
 
Uwiiii nafwa mie jamani! MIE NATUMIA ARV sasa nitapata wapi? aiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii loooooooo!
 
Hii habari haijakamilika.Lakini katika kujipanga huko kwa serikali bado hiyo ni divertion ya Resources kutoka mahali maana sidhani kama walijua hawataongezewa muda.Gharama bado anabeba mwananchi wa kawaida wakati hatukua tumejipanga.Maamuzi mabovu yanayosukumwa na uroho wa madaraka Mwananchi analipia gharama
Mjenga nchi ni mwananchi awe maskini au Tajiri; Kila mtu mungu kampa kipawa chake.
 
Kwani hamjui kwamba mwaka jana serikali ilianzisha mfuko wa Uchangiaji kwa ajili ya kununua dawa za UKIMWI? tayari serikali ilikuwa ilishajipanga toka Mwaka jana, kwa hiyo hakuna wasiwasi wowote kuhusu hilo.
Huo mfuko umeingiza shilingi ngapi hadi sasa. Je unajua kuwa miezi miwili sasa serikali haijatangaza makusanyo ya mwezi wakati inaingia ilikuwa inatangaza kila mwezi? Unajua kuwa serikali haijapeleka fedha za maendeleo kwenye idara zake kwa miezi miwili na haijapeleka fedha za matumizi ya ofisi za OC? Unajua kuwa kwa sasa uzalishaji viwandani na biashara zinashuka yaani recession?

Kwa vile hadi sasa hatujui uelekeo wa kiuchumi wa awamu ya tano, ni ndoto ya mchana kusema utajitegemea. Hukuna uwekezaji mpya utakuja kwenye nchi ambayo itoa kauli kama "uhujumu uchumi" na "kutaifisha bidhaa". Miaka hii mitano tutalia na kusaga meno
 
Tanzania haiwezi kuendelea bila misaada.
By JK jana kwenye kongamano
 
Hapa ndio moto utaonekana unawaka Tanzania,acha zile za mcc watu walikuwa wanaongea kwa kiburi.Marekani kutokuendelea na msaada wa kutoa dawa za ARV italeta matokeo mabaya zaidi kwa mfumo mzima wa Afya.Kama madaktari watakuwa wakweli na kuacha siasa watakubaliana na mimi kwamba muda wa kulaza wagonjwa utaongezeka na gharama za dawa za kawaida zitaongezeka kutokana na kuongezeka kwa waathirika wenye magonjwa nyemelezi.
Pili usugu wa virusi unaweza kuongezeka maradufu kutokana na kununua dawa za substandard kwa vijihela vinavyompa jeuri dk kusema "tumejipanga"wakati tumeona kwa dawa tu za malaria imekuwa ni shida mno kupatikana hospitali baada ya wafadhili kujitoa.Badala yake zinaonekana madukani dawa mseto zenye ubora hafifu kutoka India na hata wakati mwingine kukosekana na kusababisha watu waendelee kutumia Fansidar na Metakelfin ambayo tuliambiwa sasa haitumiki.
 
Sikia mladi wa afya marekan inasaidi nchi nying hapa kinachotokea n kutunyima kwa njia ya nyuma .... Tatizo ni zanzibar

Swala hili lilijulikana na lilijadiliwa sana wakati wa bunge la 10. wabunge walitaka kujua serikali inajipangaje wakati huo ukifika. hivyo msidhani kuwa ni jambo lililokuja kwa kusitukizwa serikali ilishaarifiwa muda wa mradi kwisha
 
Hii habari haijakamilika.Lakini katika kujipanga huko kwa serikali bado hiyo ni divertion ya Resources kutoka mahali maana sidhani kama walijua hawataongezewa muda.Gharama bado anabeba mwananchi wa kawaida wakati hatukua tumejipanga.Maamuzi mabovu yanayosukumwa na uroho wa madaraka Mwananchi analipia gharama
Sasa wewe umeambiwa chanzo cha kusitishwa huo msaada ni nini?

Hivi bavicha mkoje
 
Serikali ya Marekani imeendelea kuikaanga serikali ya makufuri kwa kuinyima tena msaada unaokadiriwa kufika Tsh trilioni 1(Tsh 787 bilioni) ambazo zimekuwa zikichangwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) kwa ajili ya ununuzi wa dawa za ARV kwa wagonjwa wa UKIMWI.

CHANZO: Mwananchi

MAONI YANGU
Haya ndiyo matunda ya kuminya demokrasia lakini wanaoumia ni watanzania wenzetu masikini wasiokuwa na hatia. Tujiandae kuzika watanzania wengi watakaokufa kwa kukosa ARV.
 
wabongo kwa kupayuka hawajambo, mlipewa msaada kwa 10yrs! ili mjiandae kujitegemea kununua dawa. 10yrs imeisha mkataba umeisha mnasema mmenyimwa msaada!
Inamaana haujui hata msaada unamaana gani?!
 
Serikali ya Marekani imeendelea kuikaanga tena serikali ya makufuri kwa kuinyima tena msaada unaokadiriwa kufika Tsh trilioni 1(Tsh 787 bilioni) ambazo zimekuwa zikichangwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) kwa ajili ya ununuzi wa dawa za ARV kwa wagonjwa wa UKIMWI.

CHANZO: Mwananchi

MAONI YANGU
Haya ndiyo matunda ya kuminya demokrasia lakini wanaoumia ni watanzania wenzetu masikini wasiokuwa na hatia. Tujiandae kuzika watanzania wengi watakaokufa kwa kukosa ARV.
Msaada huu uliisha zamani kwa sababu yamutumizi mabaya kwa mijibu wa ufahamu wangu. Sasa wewe unaongelea leo kwa sababu za kudanganya
 
Back
Top Bottom