Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,813
- 34,193
Kwa ufupi
Serikali itakosa mchango wa dawa zenye jumla ya gharama ya dola za Marekani 375 milioni sawa na Sh787 bilioni, ambazo zimekuwa zikichangiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).
Dar es Salaam. Serikali itakosa mchango wa dawa zenye jumla ya gharama ya dola za Marekani 375 milioni sawa na Sh787 bilioni, ambazo zimekuwa zikichangiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).
USAID ilitoa mchango huo chini ya mradi wa kutunza na kugawanya dawa hasa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, kwa kipindi cha miaka 10 kote nchini.
Mradi huo ambao pia umeisaidia Serikali kujenga maghala ya kuhifadhia dawa umefikika mwisho, hivyo USAID akiwa kama mchangiaji mkuu wa dawa, inaiacha ikiwa na pengo.
Hata hivyo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya amesema licha ya mradi huo kufikia ukomo na kuwa na msaada, wizara imejipanga kuhakikisha kuna uhakika wa upatikanaji wa dawa nchini.