Bro thread nzuri ila wote tunafahamu hasira zote hizi ni kwa sababu Ali Kiba alimbwaga Diamond kwenye Tuzo za Watu. Nilitegemea msomi kama wewe unaelewa tuzo zinazoendeshwa kwa mfumo huu kura za mashabiki ndio zinaamua mshindi kwa 100%, tafadhali pitia kwa waanzilishi wa Marekani
People's Choice Awards: Fan Favorites in Movies, Music & TV - PeoplesChoice.com uangalie utaratibu wao kisha linganisha
Tanzania People Choice Awards hakuna tofauti, popular vote ndio inaamua mshindi. Tuzo kama Kili ndio zinahusisha majaji kwa sababu toka hatua za awali zinahusisha Academy kwa hiyo kunahitajika majaji watakaohakiki. Kitu pekee ninachoweza kukwambia umshauri rafiki yako Diamond na team yake ni kuwa waache kudharau hizi tuzo za ndani. Majina yalipotangazwa Ali Kiba alipost Instagram na Facebook kuomba kura kwa mashabiki na team yake ilikuwa mstari wa mbele kupiga kampeni Instagram ikiwatumia watu wengine maarufu kumuombea kura. Upande mwingine Diamond hakuwa na time kabisa, ndio kwanza akaanza kuziponda tuzo za Kili mara baada ya Wema na Jokate kuanza kumpigia debe Kiba. Bado wiki mbili upande wa Kili kura zifungwe na ninakuhakikishia kuna kila dalili ya Diamond kuangukia pua kwa mara nyingine kama ataendelea na kiburi cha kutegemea eti kwa kuwa ni maarufu au ndiye mwanamuziki anaetambulika kuliko wote kwa sasa kwamba basi atapewa tuzo. Akamuulize Fid Q ambaye alikuwa na mentality hiyo hadi aliposhtuka mwaka jana baada ya kina Fella na Babu Tale kuendesha kampeni ya kumuombea kura na akapata tuzo mbili.
Kuhusu website maarufu, tambua kwamba Jamii Forums walikuwa wadhamini wa tuzo na hiyo moja kwa moja ilikuwa inawaondoa katika kinyang'anyiro. Na kama ulikuwa hujui website zenye traffic kubwa kwa sasa Tanzania ni Jamii Forums, Millard Ayo, Issa Michuzi, Global Publishers na Raha Tupu (ile ya ngono). Pamoja na hayo kura ndio ilikuwa inaamua kama wapenzi wa website tajwa hapo juu ukitoa JF na Millard hawakupiga kura kwa wingi usitegemee wataingizwa kwa kuwa tu ni "mafaza".
Miss Tanzania sifahamu sana, ila ninavyoelewa inaendeshwa na kampuni iliyopewa leseni na Miss World kwa hiyo BASATA hawana uwezo wa kuwaambia jamaa wawanyang'anye leseni ni sawa na Wizara ya Michezo isivyokuwa na uwezo wa kuwaambia CAF au FIFA wamtimue Malinzi.