Serikali Itenge Maeneo Maalum kwa Ajili ya Wakulima na Wafugaji ili Kuondoa Migogoro ya Hifadhi za Ardhi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

SERIKALI ITENGE MAENEO MAALUM KWA AJILI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI ILI KUONDOA MIGOGORO YA HIFADHI

"Nchi zilizoendelea mfano Afrika ya Kusini, Durban ni sehemu inayohusika na viwanda tu. Johannesburg ni sehemu inayohusika na Biashara tu. Tanzania tutenge maeneo yawe ni Maalum kwa wafugaji wetu tu ili Mifugo isiingie kwenye hifadhi za Taifa na isiwaingilie wakulima" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Iko mikoa inajulikana na inategemewa nchini kwa kuzalisha chakula, mfano Songea, Iringa, Njombe, Songwe, Mbeya, Katavi, Rukwa na Morogoro. Adhma ya kuwapandia wafugaji majani sehemu moja itakuwa rahisi kutambua Mifugo na kuwasaidia Maliasili kuzuia Mifugo isiingie hifadhini" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Watu wa Jimbo la Momba, mwaka 1974 kipindi cha sogea cha Mwalimu Nyerere, babu zetu waliambiwa watoke Vijiji vya mbali wakae sehemu za karibu ili huduma za kijamii ziweze kuwapata kwa pamoja na wakaachia maeneo hayo kwa Serikali kwa nia njema na maeneo hayo yakawa ni ya hifadhi" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Mwaka 1974 watu wa Momba walikuwa wanakadiriwa chini ya watu elfu 20, sasa hivi kwa Sensa ya mwaka 2022 Momba ina zaidi ya Wananchi 270,000. Katika Vijiji 72 kuna maeneo machache wanaomba waongezewe kipande kidogo cha ardhi ili waendelee na shughuli za kilimo" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Tunaomba kwa moyo wa unyenyekevu na uadilifu mkubwa; Kitongoji cha Kanyala Kijiji cha Tontela Kata ya Chilulumo; Kitongoji cha Mbalo Kijiji cha Mlomba Kata ya Chitete; Kitongoji cha Moravian Kijiji cha Itumbula Kata ya Iguna; Kitongoji cha Mbao Nachiula Kijiji cha Ntungwa Kata ya Mkomba" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Wananchi hao wote wamezungukwa na hifadhi, wamezaliana na hawana mahali pa kwenda. Nia ya Serikali ni njema ya kutunza maeneo yetu ili vizazi na vizazi vije kurithi lakini msipotupa maeneo kidogo ambayo babu zetu walikubali kuyaachia tutaenda wapi?" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Wananchi wa Momba hawaombi Hekari 1,000 au Hekari 500, wanaomba Hekari chache tu ili waendelee kuendesha shughuli zao. Mkiendelea kutuacha tutaendelea kuwa watumwa ndani ya Ardhi yetu wenyewe" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-06-03 at 16.45.30.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-03 at 16.45.30.jpeg
    26.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Video 2023-06-03 at 00.18.46(1).mp4
    20.5 MB
Wafugaji ni wakorofi sana, mkulima yeye hawezi hamisha mazao yake wala ardhi
 
Tena kuna ufumbuzi mwepesi kabisa. Bofya chini hapo:

 
Back
Top Bottom