Momba: Anayepinga Madai ya Shida ya Maji Momba Akapimwe Akili?

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MOMBA: "ANAYEPINGA MADAI YA SHIDA YA MAJI MOMBA AKAPIMWE AKILI"?

BAANDA ya February 2. 2024 Mbunge wa Jimbo la Momba kwenda na ushahidi wa video ikionyesha Wananchi wa Kijiji cha Lwatwe kata ya Ivuna wakifukua Maji chini ya ardhi, baadhi ya watu wameandika mitandaoni kwa kichwa kinachosema " WANA-MOMBA WAKATAA UZUSHI WA MBUNGE WAO" huu nao unaweza kuwa wendawazimu.

Tarehe 03.12.2023 Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe Mundy alifanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Lwatwe kitongoji cha Michese.

Akiwa hapa Mheshimiwa Mbunge, alikutana kero na hali isiyolidhisha ya upatikanaji wa maji baada ya kushuhudia msululu mkubwa wa akina mama wakigombea maji kwenye visima vya kufukua chini ya ardhi ambavyo vipo kandokando mwa Ziwa Rukwa.

Kitendo hicho kilimhudhunisha sana Mbunge huyo, mpaka kufika hatua ya kutoa machozi mbele ya wananchi hao kutokana na adha ambayo wapiga kura wake wanapitia, huku isitoshe kuwa na taarifa za watendaji wa maji kwamba eneo hilo kuna mradi wa visima unatekelezwa kumbe ni taarifa za kupikwa.

"Wananchi hapa niliambiwa kuna mradi wa visima vya maji unatekelezwa, na nimetoka kuzungumza na meneja wa Maji wa Wilaya na Mkoa wakasema huo mradi upo mbioni kukamilika, lakini cha kushangaza hakuna kinachoendelea hapa, huu siyo ujuma kweli, mimi nikisema kuna watu wananihujumu nitakuwa nimekosea kweli"? Mhe. Condester Sichalwe

Akiwa eneo la tukio Mheshimiwa Condester Sichalwe alimpigia simu meneja wa Ruwasa mkoa wa Songwe Mhandisi Charles Pambe, akimuomba kufika eneo hilo ili kujionea uhalisia, ndipo meneja huyo alituma wawakilishi wake wawili, ambao walimkuta Mbunge eneo la tukio na kukri kwamba hakika hali ni Mbaya na kuahidi kwamba baada ya siku saba watachimba visima vya dharura lakini mpaka sasa imepita miezi miwili hakuna kinacho endelea.

Baada ya Mbunge Sichalwe kupigiwa simu nyingi na wananchi kufuatia shida hiyo, ndipo akalazimika kwenda na ushahidi wa video hiyo bungeni, ili kuonyesha umma kwamba kwenye Jimbo lake Bado kuna shida kubwa sana ya Maji.

Kumekuwa na takwimu nyingi za kwenye makaratasi zikionyesha kwamba Momba imepokea fedha nyingi za maji, lakini haziendani na uhalisia, inawezekana kweli Serikali imetoa fedha hizo lakini huenda zinaishia kwenye mikono ya watu wachache, maana kama kweli zingekuwa zinafanya kazi iliyokusudiwa Momba isingekuwa na hali mbaya ya maji kiasi kile.

Dulu za habari zinaeleza kuwa kuna mkakati "ovu" wa baadhi ya watendaji wa idara ya RUWASA ndani ya Mkoa wa Songwe kutumiwa kisiasa ili kuzolotesha jitihada za Mbunge wa Jimbo la Momba Mheshimiwa Condester Sichalwe Mundy, ili aonekane hafanyi kazi vizuri, na ndiyo maana wanakwamisha miradi mingi ya Maji kwa makusudi. Imebainika.

Jimbo la Momba lenye vijiji 72 na kata 14 ni vijiji 20 tu ambavyo vinapata maji safi na salama anghalau kwa sehemu, lakini vyote 52 bado havina maji safi na salama, hizo zote ni mbinu za kumkwamisha Mbunge huyo.

Kwamfano mpaka sasa mradi huu wa Maji wa Msangano utakaonufaisha wananchi 34,162 wa Vijiji vya Naming‘ongo, Msangano, Ipata, Ntinga, Chindi, Nkala, Makamba na Yala wenye tahamani ya
Tshs 6,132,891,450.00 Ujenzi ulipaswa kukamilika mwezi wa saba mwaka huu 2024, lakini mpaka sasa utekelezaji wake haujaanza.

"Hii ni aimbu kubwa sana kuwalisha mameno ya uongo Wana Momba, hali ya upatikanaji wa maji safi na salama Momba kwa mkoa wa Songwe bado sana ukilinganisha na wilaya zingine, na hizi ni hujuma tu zinazoendelea"

"Wana-Momba wanaimani kubwa sana na chama cha Mapinduzi CCM, na Serikali ya awamu ya sita chini ya Daktari Samia Hassan Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini changamoto ipo kwa watendaji wachache waliopewa dhamana kufanya kazi kwa mazoea".

Mwisho
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-04 at 19.18.55.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-04 at 19.18.55.jpeg
    91 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-04 at 22.33.59.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-04 at 22.33.59.jpeg
    83.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-05 at 00.34.24.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-05 at 00.34.24.jpeg
    82.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom