May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,820
Ninaliona hili kwa hapa Arusha na sijajua kama Serikali inaufuatiliaji wa kujiridhisha uhalali wa kila kinachouzwa kwenye hizi yadi. Kumekuwa na masoko yanayoibuka yaliyosheheni vifaa/vyombo mbalimbali kama Majiko, Meza, Vitanda, Magodoro, TV, Feni n.k.
Ningetamani kama inawezekana kuanzishwe utaratibu ambapo vifaa/vyombo vipigwe mihuri/alama ya utambulisho kutoka kwa Mamlaka husika na kusiwe na kifaa/chombo chohote mnadani ambacho hakijathibitishwa na Wahusika/Mamlaka kujua kimepatikana vipi...badala ya kuacha tu mambo yaendeshwe kiholela.
Na Wanunuzi waelimishwe juu ya athari ya kununua kifaa/chombo kisicho na muhuri (uthibitisho).