Serikali kupitia simu za mkononi, inaweza kukusanya fedha na kuanzisha Mfuko(Fund) wa kugharamia Bima ya Afya na Elimu ya Juu kwa Watanzania wote

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Habari wadau,

Leo nimekaa na kutafakari sana juu ya uwezekano wa laini za simu tunazotumia katika simu zetu kutumika kukusanya fedha zinazoweza kugharamia matibabu ya karibu kila mtanzania na pia kukusanya fedha zinazoweza kutumika kugharamia Elimu ya juu.

Kwanini simu ya mkononi kupitia laini ya simu iliyosajiliwa?
Kulingana na Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, hadi kufikia mwezi December mwaka 2017,watanzania wapatao milioni 40 wanatumia simu za mkononi, idadi hii ikiwa ni kutoka watumiaji milioni 27.62 mwaka 2012 hivyo tunaweza kupata fedha nyingi nazingine tukazielekeza katika maeneo mengine.Pia,tusisahau idadi ya watumiaji wa simu itaendelea kuongezeka kila mwaka.

Tunaweza kukusanya fedha kiasi gani kufanikisha jambo hili kulingana na takwimu hizo?
Ni rahisi tu. Kwa mfano,ikakubaliwa na kupitishwa kuwa kila mwananchama atapaswa kuchanga shilingi miatano tu tu(500/=) kwa mwezi kupitia line yake ya simu(simu ya mkononi)

Sasa chukua 40,000,0000 x 500=20,000,000,000(Bilioni 20) na hii ni kwa mwezi mmoja tu.

Kwa mwaka maana yake ni 20,000,000,000 x12=240,000,000,000(Biloni 240).

Sasa wadau tujiulize,kwa fedha yote hii kwa mwaka,swala la kuwa na Bima ya Afya itakayohudumia kla mtanzani litashindikana na hata kiasi kingiine cha fedha kutumika kwa mambo mengine kama kuanzisha mfuko wa kugharamia elimu ya juu au fedha hizo kutumika pia kuboresha huduma za afya kama ujenzi wa vituo vya afya na mahospitali?


https://www.google.com/url?sa=t&rct=j&q=&esrc=s&source=web&cd=&cad=rja&uact=8&ved=2ahUKEwiz4PSC-KfsAhXj1uAKHVM6ARIQFjAHegQIChAC&url=https://www.pressreader.com/tanzania/mtanzania/20190630/281603832012081&usg=AOvVaw1tWi_hNU4DeItvAHpXM6AH

Kwa maana hiyo na kulingana na ongezeko hilo,mwaka huu wa 2020, idadi hiyo ya watumiaji milioni 40 itakuwa imeongezeka zaidi ya hapo.

Nini kinaweza kufanyika kufanikisha wazo hili?
Kinachoweza kufanyia ni serikali, kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) ikishirkiana na makampuni ya simu za mkononi, kuanzisha tozo maalumu kwa asilimia ya kila muda wa maongezi mtumiaji wa simu anaponunua airtime au kuanzisha vocha maalumu zitazoingizwa kama vocha za kawaida za simu ila hela itayopatikana inaingia moja kwa moja serikalini na makampuni ya simu yanaweza kulipwa aslimia fulani kama maliupo ya kazi ya uwakala wa kukusanya mapato hayo.

Kutoza kwa asilimia kwa kila muda wa maongezi(airtime) utaonunuliwa
Kinachoweza kufanyika ni wataalamu walioko serikalini(watu wa Bima ya Afya na wadau wengineo) kukaa chini na kuangalia gharama halisi ambayomkila mwannchi anaemilki simu(kulingana na idasdi iliyopo) anaweza kuchangia kupitia manunuzi ya airtime anunuapo muda wa maongezi. Hapa namanisha wataalamu wakishakaa chini na kupiga mahesanu yao,wanaweza kuamua/kupendekeza asilimia ya makato kwa kila manunuzi ya airtime yanayofanyika.

Kwa maana hiyo, gharama ya kila vocha pamoja na muda wa mangezi kwa njia ya kurusha, zinaweza kuongezwa kidogo ili kuweza kupata/kuksanya makato hayo na kuyapeleka serikalini, na asilimia fulani kubaki katka kampuni husika ya simu kama malipo ya uwakala wa kukusanya mapato hayo ya serikali.

Kuanzisha vocha maalumu kwa ajili ya kuchangia huduma hii
Hili pengine linaweza kuwa ni wazo zuri zaidi kuliko hilo hapo juu.Katika hili,serikali kwa kushirikiana na makampuni ya simu, wataandaa vocha maalumu(labda ya shilingi 100,200,300 au 500 kutokana na itavyoonekana inafaa) na mtumiaji wa simu kununua vocha hizo na kuziingiza kama anavyongiza vocha za muda wa maongezim ila fedha inayopatikana itapelekwa serkalini na kampuni huska ya simu.

Wanachoeza kufanya makampuni ya simu ni kuongeza option ya malipo haya katika "menu" zao(kama inawezeka kitaalamu kulingana na teknolojia iliyopo) ili kutenganisha malipo au manunuzi ya vocha za kawaida na hizo vocha mpya.

Namna gani fedha zinaweza kutozwa?
Kwasababu kila line ya simu imesajiliwa na bila shaka kuna database, wataalamu wanaweza kuamua ni namna gani watu watozwe(iwe ni kila anaponunua airtime kama watatozo kwa kuchaji asilimia fulani kila unaponunua airtime au atozwe mara moja kwa mwezi,mara mbili au vinginevyo).

Hapa namanisha kuwa,kwasababun kila line ya simu imesajiliwa jina moja,mtu huyo akishanunua vocha na kufikisha kiwango kilichopangwa kwa mwezi, system haitamkata tena hela anaponunua airtime nyingine ndani ya mwezi husiku(kama itakuwa ni kulipia kwa mwezi).

Kwa wenye line zaidi ya moja itakuwaje?
Kwanza lazima ieleweke kuwa,wananchi watakaoukuwa teyari kwa huduma hii ya Bima,watapaswa kusajiliwa wao pamoja na line za simu watazopendelea zitumike kwa kulipia huduma hii za simu zitakazotumika kwa huduma hii na hivyo kuondoa uwezekana wa mtu kuchajiwa kwa kila line anayomiliki.

Kwa kununua vocha maalumu, mtumiaji wa simu anaweza pia kutumia line ya simu iliyosajiliwa kutumika katika kulipia huduma hii kulipia michango yake yake ya Bima.

Namna gani watumiaji wa huduma hii watatambulika katika mahosipitali na katika vituo vya afya?
Kwasababu huduma hii itakuwa inaendeshwa kielektroniki, zinzaweza kuandaliwa kadi za kielektoniki ambazo kila mtumiaji atapewa kama kadi yake ya utambulisho, kadi ambazo zitapaswa kutambuliwa na vifaa maalumu vitavyopatikana katika hospitali na vituo husika vya afya nchi nzima.

Kadi hii, licha ya kumtambulisha mwanachama,bado inaweza pia kubeba taarifa zake zote zikiwemo taarifa za michango yake na pia kueleza kama ametimiza vigezo na mashariti yote ya kuhudumiwa na Mfuko utakaoanzishwa kulinga na sheria itayounda Mfuko huo.

Kwanini ni muhimu kuwa na Mfuko wa aina hii licha ya gharama zitazoongezeka kwa watumiaji wa simu?
Ni ukweli ulio wazi kuwa Bima ya Afya ni jambo muhimu sana kwani magonjwa huja bila kujali una fedha au huna huku magonjwa mengine gharama zake zikiwa ni juu kuliko uwezo wa watanzania walio wengi hivyo ni bora kutozwa hizo gharama ndogo ili hata unapougua usishindwe kuhudumiwa kwa kukosa fedha.

Na kama tunazotozwa fedha kila tunaponunua vitu vitu/bidhaa kama umeme kuendeshea taasisi kama EWURA au REA wanaohusika na usambazaji umeme vijijini kuna ubaya gani tukatozwa fedha kidogo kupitia simu zote za mkonono kwa ajili ya afya zetu au kugharamia elimu za watoto wetu?

Pia, unaweza kuona hiyo miatano(500/=) na nyingi lakini jiulize kwa mwezi unatumia kiasi gani kuweka kwenye simu yako na kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki tena sometimes kuwasalimia tu.Pia jiulize ni kiasi gani unakatwa kulipia deni la Bodi ya Mikopo kila mwezi alafu ndio uone kama hiyo 500 au 300 kwa mwezi inaweza kuwa ni nyingi, na pia jiulize ni kiasi gani unaweza kukopa mkopo wa riba kugharamia matibabu yako,ya mwanao au ya mzazi wako kule kijijini au aliekuja nyumbani kwako(mjini) kwa ajili ya matibabu.

Kuunda Mfuko(Fund) husika

Wataalamu na wadau wote wanaohusika wakiona jambo hili linawezekana, basi watapeleka mapendekezo yao serikalini kwa ajili ya utekeleazaji ambapo serikali itapaswa kuandaa sera na sheria itayotumika kuanzisha na kusimamia uendeshaji wa Mfuko huu.

Sheria inaweza kuweje?
Hii ni kazi ya wataalamu ila pamoja na mambo mengine,sheria inaweza kutamka kuwa ni lazima kila mtanzania mwenye kumliki line ya simu ajiunge na huduma hii au iwe ni hiari ya mtu(ni vizuri iwe hiari lakini itafaa zaidi fedha zitazokusaywa zitumike pia katika kuhamasisha watu wajiunge na Mfuko huu na pia zitumike kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya kupitia semina,makongamono,matangazo katika vyombo vya habari,n.k).

Kwa kila mchangiaji mwenye watoto au tegemezi,sheria itamke wazi ni watoto au ni wategemezi wangapi wanaweza kunufaika na huduma hiyo.

Pia,sheria itakayounda Mfuko huu, imtake kila mwanachama, kueleza ni i nani ataotaka wafaidike kupitia michango yake kwenye mfuko husika.

Usalama wa Mfuko
Ili kuzuia serikali kuingilia utendaji wa Mfuko huu, na pia ili kuufanya Mfuko uwe huru kwa lengo la kufanya wanasiasa wasiwe na mamlaka juu ya uendeshaji wa huu Mfuko huu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huu asiteuliwe na Raisi ,na pia sheria itamke bayana kuwa serikali hairuhusiwi kukopa kutoka katika huu Mfuko isipokuwa panapotokea dharura maalumu kama vile kukabiliana na madhara yaliyosababishwa na majanga ya asili au nchi inapoingia katika vita ,n.k.

Faida nyingine za kuanzishwa kwa Mfuko/tozo ya aina hii

Wafanyakazi/Waajiriwa, hawatalazimika tena kukatwa hela(maelfu kadhaa ya shlingi) kutoka kwenye mishahara yao kila mwezi kwa ajili ya kuchangia Bima ya Afya ya Taifa na hivyo wataokoa fedha na kupuguza wingi/mzigo wa makato katika mishahara yao.

Watanzania wengi hata wale wasio na ajira za kuelewaka/rasimi, wanaweza kupata Bima ya Afya kwa kumiliki tu simu ya mkononi.

Makusanyo haya yanaeweza pia kutumiwa kugharamia elimu ya juu na kusomesha watanzania wote bila kuwa na element za kubaguana na hata kuwezessha elimu bure mpaka vyuo vikuu.

Kuanzishwa kwa chombo kama hiki, pia kutatengeneza fursa za ajira kwa watanzania watakaojiriwa katika Mfuko huu,makampuni ya simu yataongeza faida na hivyo yatalipa kodi zaidi serkalini ,na pia uuzaji wa vocha hizi maalumu nao utatoa ajira kwa vijana wataojihusisha na biasharan hii,n.k.

Hasara zinazoweza kujitokeza

Binafsi sioni hasara yoyote katika kuanzisha Mfuko kama huu.

Yangu ni hayo,mnaweza kuboresha au kukosa pale ambapo nimekosea kwani naamini humu wamo watu wa fani za aina nyingi hivyo kuna wenye kuweza kuwa na mawazo bora zaidi kulingana na fani zao.

Tusisahau hata vitu kama Mpesa na tigo pesa vilibuniwa na watu, hivyo hata na sisi tunawza kubuni vya kwetu na wengine wakaiga.
 

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
622
1,000
Serikali inakusanya pesa nyingi kutoka vyanzo vingi ilivyonavyo lakini bado wazo lako halijawahi kufikiwa.. Pili katika watu milioni 40 sio wote kwao 500 ni fedha isiyo na madhara, wapo watu hawaweki hela kwenye simu mpaka line inafungiwa..
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Yan hata hii 18% ya kila vocha tunayolipa mnaona haitoshi, mnataka nyingine!!
Alafu hiyo hela nichange mm alafu apewe mwanafunzi wa chuo kikuu wakati wa kwangu shule ya msingi hana bima!?
Hiyo ni Bima kwa ajili ya Afya yako na inaweza isiwe lazima.Kumbuka watanzania wengi hawana Bima ya Afya na wako watu wanakufa kwa kukosa fedha za matibabu.Sasa kipi bora?
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Serikali inakusanya pesa nyingi kutoka vyanzo vingi ilivyonavyo lakini bado wazo lako halijawahi kufikiwa.. Pili katika watu milioni 40 sio wote kwao 500 ni fedha isiyo na madhara, wapo watu hawaweki hela kwenye simu mpaka line inafungiwa..
Soma vizuri uelewe uzi wote.
 

Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
600
1,000
Hiyo ni Bima kwa ajili ya Afya yako na inaweza isiwe lazima.Kumbuka watanzania wengi hawana Bima ya Afya na wako watu wanakufa kwa kukosa fedha za matibabu.Sasa kipi bora?
Bas isiwe kweny matumiz ya simu.
Km n jero kw mwez bas niambiwe nitoe 6000 kwa mwaka nipewe hiyo bima.
Km familia yang ina watu wanne bas nilipe 24000 tupewe hizo bima.
Lakini hujafikiria ukomo wa matumiz, yaan Je, itatumika kwa hospital zote???
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Bas isiwe kweny matumiz ya simu.
Km n jero kw mwez bas niambiwe nitoe 6000 kwa mwaka nipewe hiyo bima.
Km familia yang ina watu wanne bas nilipe 24000 tupewe hizo bima.
Lakini hujafikiria ukomo wa matumiz, yaan Je, itatumika kwa hospital zote???
kuwaambia watu watoe 6000 inaweza kuwa ni vigumu kuzikusanya hizo pesa kuliko kukusanya mia tano kwa mwezi kutoka kwenye simu yako.

Hela tunazoumia kwenye simu ni nyingi ila tuko tayari tofauti na kugharamia afya zetu.
 

Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
600
1,000
kuwaambia watu watoe 6000 inaweza kuwa ni vigumu kuzikusanya hizo pesa kuliko kukusanya mia tano kwa mwezi kutoka kwenye simu yako.
Lakini kuna jambo haliko sawa kweny hiz takwimu.
Tunaambiwa tupo kama 50mil hiv, nusu ya hiyo ni watoto chini ya miaka 15-18
Sasa wamiliki wa simu 40mil wanatoka wapi??
Ok, tusidadisi sana, lakini kwa wazo lako, bora kutoa elfu6 kwa mwaka kuliko 500 kila mwezi
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Lakini kuna jambo haliko sawa kweny hiz takwimu.
Tunaambiwa tupo kama 50mil hiv, nusu ya hiyo ni watoto chini ya miaka 15-18
Sasa wamiliki wa simu 40mil wanatoka wapi??
Ok, tusidadisi sana, lakini kwa wazo lako, bora kutoa elfu6 kwa mwaka kuliko 500 kila mwezi
Kutoa hiyo 6000 inaweza isiwe rahisi kama kukusanya kwa njia hii ya simu na pia unaweza pata fedha nyingi unazoweza kuzitumia kujenga vituo vya afya na hata kusomesha watoto wa masikini elimu ya juu na chenji ikabaki.

We kaa na ujiulize kwa mwaka unatumia shilingi ngapi kununua airtime ndio utajua kama hiyo 6000 ni hela nyingi au laa.
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
39,784
2,000
kuwaambia watu watoe 6000 inaweza kuwa ni vigumu kuzikusanya hizo pesa kuliko kukusanya mia tano kwa mwezi kutoka kwenye simu yako.

Hela tunazoumia kwenye simu ni nyingi ila tuko tayari tofauti na kugharamia afya zetu.
Tunatumia hela nyingi bila kujua sababu ni kiasi kidogo tu unatumia. Ingekuwa kama zama za kununua Dola kama vocha ununue vocha ya dola 5 ingekuwa ni sawa na 11k+ kwa sasa.

Ila ukiweka 500 unajionea unafuu sana imagine unatakiwa utie 10k kila siku si kipengele hicho
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Tunatumia hela nyingi bila kujua sababu ni kiasi kidogo tu unatumia. Ingekuwa kama zama za kununua Dola kama vocha ununue vocha ya dola 5 ingekuwa ni sawa na 11k+ kwa sasa.

Ila ukiweka 500 unajionea unafuu sana imagine unatakiwa utie 10k kila siku si kipengele hicho
Ndio maana napendekeza njia hiyo kugharamia Bima ya Afya,kwani licha ya swala la Bima kuwa ni muhimu,ila watu watalipa pasipo kuhisi maumivu, na zaidi zitapatkana hela nyingi zaidi zinazoweza kuelekezwa kwenye maeneo mengne ya kugharamia huduma za kijamii kama elimu.
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,136
2,000
Hayo ndiyo mawazo ya saccos ya chama cha wanayemuita Mwamba. Serikali haiendeshwi ki saccos. Inaendeshwa kwa fedha zinazokusanywa na mamlaka ya TRA kutoka kwa wananchi kama kodi zilizopitishwa na bunge la bajeti kwa mjibu wa sheria. Matumizi ya kodi hizo hupitishwa na bunge la bajeti ikiwamo pamoja na hilo la elimu ya juu na bima ya afya. Yaani hawa jamaa wakipewa uongozi wa nchi wataifanya nchi yetu kuwa saccos yao! God forbid!
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,517
2,000
Hayo ndiyo mawazo ya saccos ya chama cha wanayemuita Mwamba. Serikali haiendeshwi ki saccos. Inaendeshwa kwa fedha zinazokusanywa na mamlaka ya TRA kutoka kwa wananchi kama kodi zilizopitishwa na bunge la bajeti kwa mjibu wa sheria. Matumizi ya kodi hizo hupitishwa na bunge la bajeti ikiwamo pamoja na hilo la elimu ya juu na bima ya afya. Yaani hawa jamaa wakipewa uongozi wa nchi wataifanya nchi yetu kuwa saccos yao! God forbid!
Bonge la kilaza katika ubora wake!
 

residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,068
2,000
Hayo ndiyo mawazo ya saccos ya chama cha wanayemuita Mwamba. Serikali haiendeshwi ki saccos. Inaendeshwa kwa fedha zinazokusanywa na mamlaka ya TRA kutoka kwa wananchi kama kodi zilizopitishwa na bunge la bajeti kwa mjibu wa sheria. Matumizi ya kodi hizo hupitishwa na bunge la bajeti ikiwamo pamoja na hilo la elimu ya juu na bima ya afya. Yaani hawa jamaa wakipewa uongozi wa nchi wataifanya nchi yetu kuwa saccos yao! God forbid!
Hivi wewe jamaa,naona ungetoa hiyo "Dr" ukabakiza Akili pekee.
Wewe kweli ni binadamu kamili kama sisi!!?
Wewe kweli una ubongo!? Kama ubongo unao,unafanya kazi gani?
 

Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
4,006
2,000
Wazo zuri likiwekewa utaratibu mzuri wenye kuzingatia Sheria na kanuni.Ila kwa mazingira ya sasa hili linanipa shaka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom