Serikali ishugulikie kushamiri kwa uuzwaji wa vifaa vya nyumbani ambavyo vimekwishatumika

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,356
2,000
Ninaliona hili kwa hapa Arusha na sijajua kama Serikali inaufuatiliaji wa kujiridhisha uhalali wa kila kinachouzwa kwenye hizi yadi. Kumekuwa na masoko yanayoibuka yaliyosheheni vifaa/vyombo mbalimbali kama Majiko, Meza, Vitanda, Magodoro, TV, Feni n.k.

Ningetamani kama inawezekana kuanzishwe utaratibu ambapo vifaa/vyombo vipigwe mihuri/alama ya utambulisho kutoka kwa Mamlaka husika na kusiwe na kifaa/chombo chohote mnadani ambacho hakijathibitishwa na Wahusika/Mamlaka kujua kimepatikana vipi...badala ya kuacha tu mambo yaendeshwe kiholela.

Na Wanunuzi waelimishwe juu ya athari ya kununua kifaa/chombo kisicho na muhuri (uthibitisho).
 
tracebongo

JF-Expert Member
Nov 18, 2018
1,731
2,000
Ukiwa serious sana maisha haya utapata tabu. Yaani mimi nitake kuuza subwoofer langu nipite kwa mwenyekiti likapigwe muhuri kwa 5,000 na 18% kodi ya TRA?

Acha watu wauze vitu vyao kwa uhuru, kama unahisi kuna mali za wizi kareport polisi. Kumbuka kodi ya hivyo vitu ilishakatwa wakati vinanunuliwa na kama ni used kutoka nje ya nchi pia utaratibu umefatwa ndomana unaviona hapo.
 
May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,356
2,000
Ukiwa serious sana maisha haya utapata tabu. Yaani mimi nitake kuuza subwoofer langu nipite kwa mwenyekiti likapigwe muhuri kwa 5,000 na 18% kodi ya TRA!?
Acha watu wauze vitu vyao kwa uhuru, kama unahisi kuna mali za wizi kareport polisi. Kumbuka kodi ya hivyo vitu ilishakatwa wakati vinanunuliwa na kama ni used kutoka nje ya nchi pia utaratibu umefatwa ndomana unaviona hapo.
Sina shida sana na Vinavyotoka Nje ya Nchi.

Hofu yangu ni haya Magodoro yetu tukiyaanika uwani baada ya Mtoto kukojolea yanabebwa sana, na sababu kubwa ni kuwa tayari kuna soko la uhakika.

Kama hawa Wauzaji watatakiwa kuripoti kila wanachopokea kwenye yard zao....kwa kuthibitisha tu kuwa wameuziwa na Muuzaji/mmiliki halali, na akajitambulisha kwa Msimamizi/Kiongozi wa eneo itatosha na wala sijasema suala la risiti au kodi....lengo hapa ni ku discaurage wizi holela mitaani.
 
Maleto

Member
Jun 10, 2020
30
95
Ukiwa serious sana maisha haya utapata tabu. Yaani mimi nitake kuuza subwoofer langu nipite kwa mwenyekiti likapigwe muhuri kwa 5,000 na 18% kodi ya TRA?

Acha watu wauze vitu vyao kwa uhuru, kama unahisi kuna mali za wizi kareport polisi. Kumbuka kodi ya hivyo vitu ilishakatwa wakati vinanunuliwa na kama ni used kutoka nje ya nchi pia utaratibu umefatwa ndomana unaviona hapo.

Haaaaaa! unaipa sarekali kazi ngumu sanaa .
 
mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
6,428
2,000
Ukiwa serious sana maisha haya utapata tabu. Yaani mimi nitake kuuza subwoofer langu nipite kwa mwenyekiti likapigwe muhuri kwa 5,000 na 18% kodi ya TRA?

Acha watu wauze vitu vyao kwa uhuru, kama unahisi kuna mali za wizi kareport polisi. Kumbuka kodi ya hivyo vitu ilishakatwa wakati vinanunuliwa na kama ni used kutoka nje ya nchi pia utaratibu umefatwa ndomana unaviona hapo.
Mleta uzi ameongea jambo point sana.
Nadhani linapaswa kuangaliwa kwa makini sana suala hilo.
Mfano south yapo maduka kama hayo.
Yanaitwa pawn shops.
Huruhusiwi kuuza au kununuwa chochote bila ID yako na risiti ya kitu husika.
Ili chochote kikitokea basi ni wewe na wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
6,428
2,000
Ninaliona hili kwa hapa Arusha na sijajua kama Serikali inaufuatiliaji wa kujiridhisha uhalali wa kila kinachouzwa mtaani. Kumekuwa na masoko yanayoibuka yaliyosheheni vifaa/vyombo mbalimbali kama Majiko, Meza, Vitanda, Magodoro, TV, Feni n.k.

Ningetamani kama inawezekana kuanzishwe utaratibu ambapo vifaa/vyombo vipigwe mihuri/alama ya utambulisho kutoka kwa Mamlaka husika na kusiwe na kifaa/chombo chohote mnadani ambacho hakijathibitishwa na Wahusika/Mamlaka kujua kimepatikana vipi...badala ya kuacha tu mambo yaendeshwe kiholela.

Na Wanunuzi waelimishwe juu ya athari ya kununua kifaa/chombo kisicho na muhuri (uthibitisho).
Naunga mkono hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
miss pablo

JF-Expert Member
Jul 9, 2018
3,154
2,000
Ukiwa serious sana maisha haya utapata tabu. Yaani mimi nitake kuuza subwoofer langu nipite kwa mwenyekiti likapigwe muhuri kwa 5,000 na 18% kodi ya TRA?

Acha watu wauze vitu vyao kwa uhuru, kama unahisi kuna mali za wizi kareport polisi. Kumbuka kodi ya hivyo vitu ilishakatwa wakati vinanunuliwa na kama ni used kutoka nje ya nchi pia utaratibu umefatwa ndomana unaviona hapo.
Yaan anataka kodi itozwe twice.

Sijajua kama amejiuliza wenye bidhaa wakaamua kuzidump mazingira yatakuaje badala ya kuwa reused
 
miss pablo

JF-Expert Member
Jul 9, 2018
3,154
2,000
Sina shida sana na Vinavyotoka nje.

Hofu yangu ni haya Magodoro yetu tukiyaanika baada ya Mtoto kukojolea yanabebwa sana, na sababu kubwa ni kuwa tayari kuna soko la uhakika.

Kama hawa Wauzaji watatakiwa kuripoti kila wanachopokea kwenye yard zao....kwa kuthibitisha tu kuwa wameuziwa na Muuzaji/mmiliki halali, na akajitambulisha kwa Msimamizi/Kiongozi wa eneo itatosha na wala sijasema suala la risiti au kodi....lengo hapa ni ku discaurage wizi holela mitaani.
Ooj, for that case u have a point. Lakini unadhani ndo itakua suluhisho? Hapana.
Watu watachonga mpaka mihuri fake. Hilo la kutozwa kodi twice ni wizi aisee
 
Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
524
1,000
Mleta mada yupo sahihi, ila alisahau kueleza sababu ya kupata udhini ya mamlaka ili aeleweke kwa urahisi.

Kuna sehemu madalali walisombwa kwenye Difenda la polisi kisa, wanauza magodoro kumbe ni ya wizi.
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,541
2,000
Ninaliona hili kwa hapa Arusha na sijajua kama Serikali inaufuatiliaji wa kujiridhisha uhalali wa kila kinachouzwa mtaani. Kumekuwa na masoko yanayoibuka yaliyosheheni vifaa/vyombo mbalimbali kama Majiko, Meza, Vitanda, Magodoro, TV, Feni n.k.

Ningetamani kama inawezekana kuanzishwe utaratibu ambapo vifaa/vyombo vipigwe mihuri/alama ya utambulisho kutoka kwa Mamlaka husika na kusiwe na kifaa/chombo chohote mnadani ambacho hakijathibitishwa na Wahusika/Mamlaka kujua kimepatikana vipi...badala ya kuacha tu mambo yaendeshwe kiholela.

Na Wanunuzi waelimishwe juu ya athari ya kununua kifaa/chombo kisicho na muhuri (uthibitisho).
washauri watu waache kukopa FINCA and Co
 
May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,356
2,000
Tatizo litaanza na yule muuzaji kuthibitisha kua mali ni yake...
Kuanzia kwenye risiti ya awali.
Naifahamu hiyo changamoto lakini ni rahisi sana kwa mmiliki halali kujitambulisha ofisi ya Kata lilipo duka/yadi ya kuuzia mali hizo kuliko yule aliyeiba.

Mmiliki/Muuzaji wa kwanza akijitambulisha kwa kuacha taarifa za anapoishi, Balozi wake n.k ni taarifa tosha.

Hata kama haitosaidia kwa 100% lakini walau 70% zikipatikana ni tofauti kabisa na kuachwa mambo kwenda tu kiholela.
 
May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,356
2,000
Mleta mada yupo sahihi, ila alisahau kueleza sababu ya kupata udhini ya mamlaka ili aeleweke kwa urahisi.

Kuna sehemu madalali walisombwa kwenye Difenda la polisi kisa, wanauza magodoro kumbe ni ya wizi.
Exactly my point, uwepo wa Wizi siku zote unasababishwa na soko.

Na uwepo wa hizi yadi ni kuhalalisha masoko yasiyo rasmi yatakayovutia Wizi mitaani.
 
May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,356
2,000
washauri watu waache kukopa FINCA and Co
Watu wakope tu.

Ila tusisahau kwenye msafara wa Mamba na Kenge wanajichomekamo....basi la, mali za FINCA and Co ziwe na utambulisho wake na za Wananchi pia ziwe na utambulisho wake.
 
las Casas

JF-Expert Member
Nov 22, 2015
407
500
Mkuu naunga mkono hoja, mitaa hiyo karibu na Pinpoint niliwahikutaka kununua kitu nikasita nisije kamatwa kutokana na uhalali wa mali husika ambayo ni used
 
May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,356
2,000
Mkuu naunga mkono hoka, mitaa hiyo karibu na Pinpoint niliwahikutaka kununua kitu nikasita nisije kamatwa kutokana na uhalali wa mali husika ambayo ni used
Na pale walianza kidogokidogo lakini sasa hivi eneo limepanuka na wanaendelea kupanua eneo.

Na sasa wanaenda mpaka wanakaribia yale Mataa ya Mianzini....na wameshachukua pande zote mbili za barabara.

Wengine(kama sio hao hao) wamefungua kule maeneo ya Samunge sambamba na Vinu vya National Milling.

Sasa huu ushamiri unatambulika na Mamlaka au wamekunja nne tu maofisini kuacha mambo yaende kiholela?.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom