Serikali ipige marufuku vipindi vya michezo asubuhi redioni

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Serikali ipige marufuku vipindi vya michezo redioni asubuhi. Haiwezekani asubuhi muda wa kazi ndio watu waaanza kuchambua michezo toka saa 2 asubuhi hadi saa 5, watu watafanya kazi saa ngapi?

Muda wa kufanya shughuli za uzalishaji ndio watu wanasikilizisha watu vipindi visivyo na kichwa wala miguu na mbaya zaidi 90% ya huo uchambuzi ni mpira wa ulaya, wachezaji wa ulaya, sijui mambo gani ya hovyo hovyo, watu watafanya kazi saa ngapi?

Serikali iweke taratibu ya hizi programs za kwenye redio stations, vipindi vyote vya michezo viwe jioni au usiku, sio asubuhi.

Serikali iingilie kati radio station programs zisizo na maana.
 
Ukisikia viazi, huyu ni kiazi sasa.

Kwani wamekuwekea sheria kuwa lazima uwasikilize?

Ukiona hivyo, hauna kazi, sababu mtu mwenye kazi zake hana muda huo wa kusikiliza na kufuatilia kipindi, tena kipindi asicho kipenda.

Radio zenyewe bongo zimejaa, kwanini ung'ang'ania radio moja?
 
Serikali ipige marufuku vipindi vya michezo redioni asubuhi. Haiwezekani asubuhi muda wa kazi ndio watu waaanza kuchambua michezo toka sa 2 asubuhi hadi sa 5, watu watafanya kazi sa ngapi? Muda wa kufanya shughuli za uzalishaji ndio watu wanasikilizisha watu vipindi visivyo na kichwa wala migui na mbaya zaidi 90% ya huo uchambuzi ni mpira wa ulaya, wachezaji wa ulaya, sijui mambo gani ya hovyo hovyo, watu watafanya kazi sa ngapi?

Serikali iweke taratibu ya hizi programs za kwenye redio stations, vipindi vyote vya michezo viwe jioni au usiku, sio asubuhi.

Serikali iingilie kati radio station programs zisizo na maana.
Hii promo imepenya.
 
Ha ha ha ha Ndugu yangu mbona kama unateseka sana, Ni hii sports Arena ya leo au kuna Jengine?
 
Serikali ipige marufuku vipindi vya michezo redioni asubuhi. Haiwezekani asubuhi muda wa kazi ndio watu waaanza kuchambua michezo toka sa 2 asubuhi hadi sa 5, watu watafanya kazi sa ngapi? Muda wa kufanya shughuli za uzalishaji ndio watu wanasikilizisha watu vipindi visivyo na kichwa wala migui na mbaya zaidi 90% ya huo uchambuzi ni mpira wa ulaya, wachezaji wa ulaya, sijui mambo gani ya hovyo hovyo, watu watafanya kazi sa ngapi?

Serikali iweke taratibu ya hizi programs za kwenye redio stations, vipindi vyote vya michezo viwe jioni au usiku, sio asubuhi.

Serikali iingilie kati radio station programs zisizo na maana.
asiyeenda kazini kwasababu ya kusikiliza uchambuzi wa habari za michezo atamalizana na HR wa ofisi husika wewe endelea na shuhuli zako acha unaa.
 
Nimeandika nimefuta, nikaandika nikafuta, nikaandika tena nikafuta.

Nisamehe kwa niliyoandika na kufuta.
Yani wee jamaa hutulii. Ngoja shemeji yako akufukuze urudi kwa kaka yako uswaz choo passportsizze hamna bundle. Dada yako kaxhoka kukukingia kifua
 
Mtu anashindwa kuelewa kuwa.

1.Hata michezo ni ajira.
2. Kuna kazi nyingi unaweza kufanya huku unasikiliza redio.
3. Si kila mtu anafanya kazi asubuhi.
4. Hata yeye anaweza kuanzisha redio akatangaza anachoona cha maana.
5. Hakuna anayemlazimisha kusikiliza.
6. Serikali imesaini mikataba ya kimataifa ya kuthamini uhuru wa vyombo vya habari.
7. Haki ya kujieleza ni haki ya msingi ya kikatiba Tanzania.
8. Serikali inafurahia watu wakiongea habari za michezo kwa sababu wanakuwa hawaongelei matatizo ya uchumi na siasa ya nchi.
9. Watu wanahitaji distractions, huwezi kuongelea falsafa, uchumi na siasa muda wote.
10. Ajira zenyewe za kamba, why so serious?
 
Back
Top Bottom