Tunajengaje "Utalii wa Michezo" kwa kupiga marufuku na kutishia mashabiki wasisapoti timu fulani?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,137
7,905
Nimekumbuka hapo katikati hasa kipindi "African Football League" inakaribia kuzinduliwa, Serikali ilikuwa inaongelea umuhimu wa kuwekeza kwenye "Sports Tourism" au "Utalii wa Michezo". Tafsiri ya haraka ya "Utalii wa Michezo" maana yake ni "kuandaa matukio ya kimichezo ambayo yatavutia watu kutoka miji au nchi nyingine kuja katika mji ambao tukio hilo la michezo linafanyika kwa nia ya kushuhudia na kuburudika."

Hivi sasa kumekuwa na fukufuku la kutishia watu na kupiga marufuku Watanzania wasisapoti timu za nje zinapokuja kucheza na timu za Tanzania. Mimi nafikiri tutoke kwenye dhana kuwa Simba au Yanga wanapocheza, basi wakifungwa goli wanaoshangilia tunakimbilia kuwalebo kuwa ni mashabiki wa mtani wake.

Ukipita mitaani hata mechi hizi za kimataifa zisipokuwepo watu wanaonyesha mapenzi na timu za nje na wanavaa jezi zao katika maisha yao ya kawaida tu. Tanzania ya leo si ajabu kukutana na mtu mtaani amevaa jezi ya TP Mazembe au Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns au Al Ahly achilia mbali timu za Ulaya na wanafuatilia kwa ukaribu mechi zao hata za ligi ya ndani. Kwa nini tunashangaa tukiona kuna watanzania wanawashangilia au kuwasapoti pale wanapokuja? Kuna Watanzania wangapi wapenzi wa Yanga au Simba lakini pia ni wapenzi wa Liverpool/Arsenal/Man City/Barcelona/Real Madrid/ Man U, nk. lakini hilo halitushangazi ila tunashangaa na kuhamaki wakiwa wapenzi wa timu zingine za Afrika?

Ili tukuze utalii wa Michezo, sehemu za michezo hazitakiwi kuwa viwanja vya vita. Vita iwepo pale kwenye pitch kati ya wachezaji 11 dhidi ya 11 ya upande wa pili ila majukwaani tuhakikishe tunatengeneza mazingira ya urafiki na upendo, hapo ndiyo kweli tunaweza kumfanya mtu asafiri umbali mrefu akijua hata avaeje, ashangilie timu gani au akae wapi jukwaani atafurahi, ataburudika na atakuwa salama.

Kuna kipindi tulikuwa tunafanya kampeni za kukuza Utalii wa Ndani. Kimsingi Utalii wa Michezo ni sehemu katika utalii wa ndani. Imekuwa ni utamaduni wetu kwa watu kusafiri kutoka mkoa mmoja hadi mwingine kushuhudia timu yake pendwa ikicheza. Sijawahi kusikia watu wakienda mikoani wakibughudhiwa na wenyeji kisa tu kujenga mazingira ya ushindi kwa timu ya nyumbani. Pamoja na kwamba hii haijawahi kutambulika rasmi kama ni Utalii lakini kimantiki ni Utalii wa Ndani na ni Utalii wa Michezo. Inakuwaje sasa tunapromote vitisho kwa wageni au wenyeji walio na mapenzi na timu ngeni?

Ningetegemea kwa nafasi hii adimu tuliyopata ya Simba na Yanga kufikia robo fainali ya mashindano ya CAF, viongozi wangekuja na mbinu za kupromote na kuibrand ligi yetu na derby yetu ya Kariakoo ili kuvutia wawekezaji, watazamaji na watalii wa michezo. Tulitakiwa sasa hivi tuwe tunaandaa matangazo makali yatakayoruka katika mechi za kwanza za Simba vs Al Ahly na ile ya Yanga vs Mamelodi, matangazo ya kupromoti na kubrand Kariakoo Derby, Simba Day na Siku ya Mwananchi. Cha kushangaza, badala yake tumekalia kuwakimbiza wale ambao tunatakiwa kuwavutia. Hizi timu zimefika hapa si kwa kutishia tishia watu wasiende viwanjani au wasivae jezi fulani (ukiachilia vitisho katika ile mechi ya Yanga vs. Medeama) bali kwa kutengeneza timu bora za ushindani.

Embu tuumize vichwa kujua tunawezaje kukuza ligi yetu iwe bora zaidi, tunawezaje kuongeza uwekezaji katika ligi na tunawezaje kuvifanya vilabu vyetu viwe na thamani zaidi. Hizi habari za vitisho vitisho tuachane nazo.
 
Mashabiki wa simba acheni umbumbumbu wenu wa kuwashabikia wageni. Wakija wale Waarabu wenu, hata aibu huwa hamna! Eti mnawashangilia!!
 
Kila mtu aishi kimpango wake. Kama kwenye mabaa tunakaa tunashangilia timu za kigeni, iweje iwe ajabu tukiwashangilia viwanjani? Wengine wanashangilia kwa sababu wametandika mikeka
 
Mashabiki wa simba acheni umbumbumbu wenu wa kuwashabikia wageni. Wakija wale Waarabu wenu, hata aibu huwa hamna! Eti mnawashangilia!!
Kama issue ni waarabu, mbona kwenye mechi ya Medeama mlitishia watu wasije uwanjani bila kuvaa jezi ya Yanga?
 
Kama utalii ni kwenda kupokea timu pinzani airport , Hersi kuvaa jezi ya Kaizer na Manara kuvaa jezi ya Orlando kisa inacheza na Simba basi ni utalii wa kijinga
 
Mashabiki wa simba acheni umbumbumbu wenu wa kuwashabikia wageni. Wakija wale Waarabu wenu, hata aibu huwa hamna! Eti mnawashangilia!!
Uto hamna aibu kwanini?
👇
images (3).jpeg
images (3).jpeg
 
Kwani na nyie Simba huwa mnapokea wageni au kuvaa jezi za timu pinzani na Yanga ? Kama ni ndio we vaa tu hakuna wakukuzuia
 
Kama utalii ni kwenda kupokea timu pinzani airport , Hersi kuvaa jezi ya Kaizer na Manara kuvaa jezi ya Orlando kisa inacheza na Simba basi ni utalii wa kijinga
Hao ni viongozi wasiojitambua na kuna jinsi ya kuwaadabisha kama wahusika watataka kufanya hivyo. Mimi naongelea hivi vitisho vinavyoelekezwa kwa mashabiki wanaoenda uwanjani.
 
Nimekumbuka hapo katikati hasa kipindi "African Football League" inakaribia kuzinduliwa, Serikali ilikuwa inaongelea umuhimu wa kuwekeza kwenye "Sports Tourism" au "Utalii wa Michezo". Tafsiri ya haraka ya "Utalii wa Michezo" maana yake ni "kuandaa matukio ya kimichezo ambayo yatavutia watu kutoka miji au nchi nyingine kuja katika mji ambao tukio hilo la michezo linafanyika kwa nia ya kushuhudia na kuburudika."

Hivi sasa kumekuwa na fukufuku la kutishia watu na kupiga marufuku Watanzania wasisapoti timu za nje zinapokuja kucheza na timu za Tanzania. Mimi nafikiri tutoke kwenye dhana kuwa Simba au Yanga wanapocheza, basi wakifungwa goli wanaoshangilia tunakimbilia kuwalebo kuwa ni mashabiki wa mtani wake.

Ukipita mitaani hata mechi hizi za kimataifa zisipokuwepo watu wanaonyesha mapenzi na timu za nje na wanavaa jezi zao katika maisha yao ya kawaida tu. Tanzania ya leo si ajabu kukutana na mtu mtaani amevaa jezi ya TP Mazembe au Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns au Al Ahly achilia mbali timu za Ulaya na wanafuatilia kwa ukaribu mechi zao hata za ligi ya ndani. Kwa nini tunashangaa tukiona kuna watanzania wanawashangilia au kuwasapoti pale wanapokuja? Kuna Watanzania wangapi wapenzi wa Yanga au Simba lakini pia ni wapenzi wa Liverpool/Arsenal/Man City/Barcelona/Real Madrid/ Man U, nk. lakini hilo halitushangazi ila tunashangaa na kuhamaki wakiwa wapenzi wa timu zingine za Afrika?

Ili tukuze utalii wa Michezo, sehemu za michezo hazitakiwi kuwa viwanja vya vita. Vita iwepo pale kwenye pitch kati ya wachezaji 11 dhidi ya 11 ya upande wa pili ila majukwaani tuhakikishe tunatengeneza mazingira ya urafiki na upendo, hapo ndiyo kweli tunaweza kumfanya mtu asafiri umbali mrefu akijua hata avaeje, ashangilie timu gani au akae wapi jukwaani atafurahi, ataburudika na atakuwa salama.

Kuna kipindi tulikuwa tunafanya kampeni za kukuza Utalii wa Ndani. Kimsingi Utalii wa Michezo ni sehemu katika utalii wa ndani. Imekuwa ni utamaduni wetu kwa watu kusafiri kutoka mkoa mmoja hadi mwingine kushuhudia timu yake pendwa ikicheza. Sijawahi kusikia watu wakienda mikoani wakibughudhiwa na wenyeji kisa tu kujenga mazingira ya ushindi kwa timu ya nyumbani. Pamoja na kwamba hii haijawahi kutambulika rasmi kama ni Utalii lakini kimantiki ni Utalii wa Ndani na ni Utalii wa Michezo. Inakuwaje sasa tunapromote vitisho kwa wageni au wenyeji walio na mapenzi na timu ngeni?

Ningetegemea kwa nafasi hii adimu tuliyopata ya Simba na Yanga kufikia robo fainali ya mashindano ya CAF, viongozi wangekuja na mbinu za kupromote na kuibrand ligi yetu na derby yetu ya Kariakoo ili kuvutia wawekezaji, watazamaji na watalii wa michezo. Tulitakiwa sasa hivi tuwe tunaandaa matangazo makali yatakayoruka katika mechi za kwanza za Simba vs Al Ahly na ile ya Yanga vs Mamelodi, matangazo ya kupromoti na kubrand Kariakoo Derby, Simba Day na Siku ya Mwananchi. Cha kushangaza, badala yake tumekalia kuwakimbiza wale ambao tunatakiwa kuwavutia. Hizi timu zimefika hapa si kwa kutishia tishia watu wasiende viwanjani au wasivae jezi fulani (ukiachilia vitisho katika ile mechi ya Yanga vs. Medeama) bali kwa kutengeneza timu bora za ushindani.

Embu tuumize vichwa kujua tunawezaje kukuza ligi yetu iwe bora zaidi, tunawezaje kuongeza uwekezaji katika ligi na tunawezaje kuvifanya vilabu vyetu viwe na thamani zaidi. Hizi habari za vitisho vitisho tuachane nazo.
Thamani ya KARIAKOO DERBY ni kubwa Africa.

Haijawa kwa bahati mbaya bali ni kwa utani na upinzani wa hali ya juu, likiwemo amshaamsha ya kupokea wageni na kuwashangilia.

Hii ladha haipaswi kupotea sababu ubora wa Simba unategemea na ubora wa Yanga sababu ya upinzani na utani baina yao.
 
Utumbo, utumbo na utumbo mtupu
 
Thamani ya KARIAKOO DERBY ni kubwa Africa.

Haijawa kwa bahati mbaya bali ni kwa utani na upinzani wa hali ya juu, likiwemo amshaamsha ya kupokea wageni na kuwashangilia.

Hii ladha haipaswi kupotea sababu ubora wa Simba unategemea na ubora wa Yanga sababu ya upinzani na utani baina yao.
Ni kweli utani na kuzodoana kunawafanya watu wapambanie vyao
 
Back
Top Bottom