Kama ni kweli Serikali imeamua kufundisha somo la Uchambuzi wa Michezo, Kuna watu wamerogwa kule juu

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,745
Yaani kweli hii ndo wanaona issue ya msingi kwa Watanzania? Hawa watu wanalipwaje hizi kodi kufanya mambo ya hovyo kama haya?

📍Bungeni,Dodoma

▪️SERIKALI KUANZISHA SOMO LA UCHAMBUZI WA MICHEZO VYUONI

Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inakusudia kuanza kufundisha somo la Uchambuzi wa Michezo katika Chuo Cha Maendeleo ya Michezo-Malya na Vyuo vingine kwa kuzingatia uhitaji wa somo hilo nchini ili kuongeza ajira na utaalamu katika eneo hilo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma Februari 1, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa jimbo la Mlalo, Lushoto Mhe. Rashid Abdallah Shangazi aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuendeleza wachambuzi wa soka nchini ili wawe na utaalamu wa kutosha katika kazi hiyo.

"Uchambuzi katika michezo ni sehemu ya mada zinazohusiana na michezo husika ambazo zipo katika sheria zinazotawala michezo. Serikali itaangalia mahitaji ya soko katika kipindi cha kuhuisha mitaala na kuzingatia eneo la uchambuzi ambalo sasa limeiletea heshima michezo kupitia wachambuzi nguli na mahiri waliopo" amesisitiza Mhe. Mwinjuma.

Ameongeza kuwa somo hilo la uchambuzi halitahusisha soka pekee bali pia michezo mingine ikiwemo Ngumi ambayo ni miongoni mwa michezo inayotangaza vyema Taifa la Tanzania na kutoa ajira.

Aidha, Mhe. Mwinjuma ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau wa Michezo wapate elimu ya michezo katika Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya ambacho kinatoa elimu ya ufundishaji michezo, uongozi na utawala katika michezo, elimu ya viungo vya mwili katika michezo pamoja na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, netiboli, mpira wa kikapu, riadha na mpira wa wavu.
GFQEfOrXcAA270_.jpg

📸: Shamimu Nyaki
 
Wachambuzi wa Tanzania ni kama bendera fata upepo.

Timu inayoshinda ndiyo inasifiwa, na iliyoshindwa inapondwa.

Ninaunga mkono hoja ya kuirasimisha hii taaluma.
 
Kiasili watz wanakipaji cha kuongea, wape heading tu... sioni vibaya kipaji kikafanywa profession, kuliko kujidanganya kuanzisha academy na diet yetu ya pasi ndefu za makande na ugali, ukashindane na muarabu alieshiba maziwa ya ngamia from childhood to present time.
 
SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inakusudia kuanza kufundisha somo la Uchambuzi wa Michezo katika Chuo Cha Maendeleo ya Michezo-Malya na Vyuo vingine kwa kuzingatia uhitaji wa somo hilo nchini ili kuongeza ajira na utaalamu katika eneo hilo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma Februari 1, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa jimbo la Mlalo, Lushoto Mhe. Rashid Abdallah Shangazi aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuendeleza wachambuzi wa soka nchini ili wawe na utaalamu wa kutosha katika kazi hiyo.

"Uchambuzi katika michezo ni sehemu ya mada zinazohusiana na michezo husika ambazo zipo katika sheria zinazotawala michezo. Serikali itaangalia mahitaji ya soko katika kipindi cha kuhuisha mitaala na kuzingatia eneo la uchambuzi ambalo sasa limeiletea heshima michezo kupitia wachambuzi nguli na mahiri waliopo" amesisitiza Mhe. Mwinjuma.

Ameongeza kuwa somo hilo la uchambuzi halitahusisha soka pekee bali pia michezo mingine ikiwemo Ngumi ambayo ni miongoni mwa michezo inayotangaza vyema Taifa la Tanzania na kutoa ajira.

Aidha, Mhe. Mwinjuma ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau wa Michezo wapate elimu ya michezo katika Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya ambacho kinatoa elimu ya ufundishaji michezo, uongozi na utawala katika michezo, elimu ya viungo vya mwili katika michezo pamoja na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, netiboli, mpira wa kikapu, riadha na mpira wa wavu.

#KitengeUpdates
 
Kiasili watz wanakipaji cha kuongea, wape heading tu... sioni vibaya kipaji kikafanywa profession, kuliko kujidanganya kuanzisha academy na diet yetu ya pasi ndefu za makande na ugali, ukashindane na muarabu alieshiba maziwa ya ngamia from childhood to present time.
Pasi ndefu ziko mikoa yenu hiyo yenye dhiki na taabu. Huko ndiko mnashindia makande na ugali.

Nenda usukumani ambako watoto wanakuzwa kwa maziwa na viazi....Wana siha kinyama.

Nenda mikoa ya Mbeya, Kagera na Kilimanjaro ambako watoto wanakuzwa kwa ndizi na nyama....watoto wana siha siyo ya kawaida.

Acha kusambaza dhiki ya nyumbani kwenu kwenye taifa zima.
 
Kibuyu tu ...

Wekezeni michezo huko shule za msingi na sekondari....miundo mbinu ya michezo mafunzo nk

Tunashida na VIBUYU
 
Pasi ndefu ziko mikoa yenu hiyo yenye dhiki na taabu. Huko ndiko mnashindia makande na ugali.

Nenda usukumani ambako watoto wanakuzwa kwa maziwa na viazi....Wana siha kinyama.

Nenda mikoa ya Mbeya, Kagera na Kilimanjaro ambako watoto wanakuzwa kwa ndizi na nyama....watoto wana siha siyo ya kawaida.

Acha kusambaza dhiki ya nyumbani kwenu kwenye taifa zima.

Mkuu kwanza punguza hasira. Umeandika kwa hisia kama vile jambo limeelekezwa kwenye familia yako. Pasi ndefu zipo hadi kwa wanafunzi wa chuo wenye boom, unakataa kwa watoto wanaotegemea wazazi??

Wewe unapajua nilipo mimi?

Una data au unaongea tu?

Inawezekana chakula kinazalishwa kwa wingi kweli, ila kinauzwa na wakulima ikipita tu sabasaba wanaanza kuwa na upungufu wa chakula kidogo kidogo, ikifika December-Januari hali ni ngumu. Pasi ndefu zipo, wapo wagonjwa wanakatisha dawa kwa sababu ya ukosefu wa chakula.

Pia chakula kinaweza kuwepo, ila ratiba za wamama wapambanaji zikawafanya watoto wawe na lishe duni, sio kila mwenye utapiamlo hana chakula.

Mimi swezi kusemea kuhusu usukumani kwa sababu sijawahi kufika huko wala sijui takwimu zao.

Ila nakumbuka vyema Mwendazake alivyokua akipambana watu wasiuze mazao akidai kwamba kila mwaka wakulima wanakua na njaa kwa sababu ya kuuza mazao yote huko kwao usukumani.
 
Back
Top Bottom