Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,883
- 2,765
Hili kwa ukweli wizara husika (ya habari) ilizingatie. Saa mbili, saa tatu asubuhi unaanza kusikia habari za nani kafungwa nani kahamia club fulani, kocha kafanyaje, n.k. Muda wa asubuhi ni muda wa kupata taarifa muhimu za matukio yanayoendelea duniani kuanzia siasa, uchumi, utamaduni, sheria, sayansi na teknolojia.
Vyombo vyetu vijikite huko. Si kuanza na michezo ili kuwaosha vijana mbongo zao wawaze tu kuanza kubeti. Hii kwa kiasi kikubwa sana inaondoa ari ya udadisi kwa hayo niliyoweka hapo juu. Nini kifanyike
1. Hao hao wachambuzi wageuze vipindi vyao mwelekeo wa maeneo tajwa hapo juu.
2. Masuala ya michezo yaanze saa saba mchana baada ya taarifa za habari za kitaifa na kimataifa za redioni ta TV
3. Wizara itoe mwongozo wa namna ya kufikia huko.
4. Taasisi mbalimbali zianze kushirikiana na vyombo hivi ili kuwapa mada za kujadili
Mathalani wakati huu tunazungumzia kilimo kikiwalenga vijana. Wizara husika zittoe mwongozo wa namna ya kuandaa vipindi ambayo vitakuwa na mvuto kusikiliza na hata kutazama. kwa namna hii tutajenga kizazi chenye kudadisi na kuwa na mafanikio katika nyaja tofauti. Yafanyiwe kazi