Serikali inawahamisha wananchi wasahau na wasiongelee tena TOZO ya miamala ya simu. Wananchi tuendelee kuwalaani viongozi wetu waliotuletea huu wizi.

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
262
778
b6597322-1343-4aaa-be27-8f50b7e3be92.jpeg

Huo hapo juu ni wizi na hujuma za waziwazi tunaofanyiwa na serikali yetu. Cost of living imekuwa kubwa, uchumi wetu wa kusuasia unazidi kuwa hoi hasa wazazi na ndugu zetu wanaotegemea mpesa, tigopesa, airtel money
images (6).jpeg


kufanyiwa miamala yao. Fikiria ndani ya ada za miamala kuna 18% kodi inayoenda serikalini bado serikali imeona makusanyo hayo halali kutoka kwa wananchi hayatoshi wameona ni bora watanzania maskini waishi kama misukule ila Tozo mpya iendelee kuwanyonga watanzania.
Kama ni issue ya uzalendo, viongozi wetu wawe wa kwanza kuonesha uzalendo kwa kujipunguzia mishahara minono wanayolipana.
Kuna maoni hapa juu ya njia nyepesi serikali inaweza kuzitumia kujiongezea mapato bila serikali kutumia Tozo hii ya miamala ya simu.


Wananchi tuendelee kukumbuka kwamba Tozo ipo tupaze sauti kuipinga na kuwalaani viongozi wote walioleta hoja hiyo na waliohusika kuipitisha.
 
Tupunguze digital teansactions tozo kubwa sana ikiwexekana tuache kabisa
 
Back
Top Bottom