Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) yatakiwa kuwa na mfumo madhubuti wa kuratibu utafiti utakaosomana na Taasisi nyingine

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo ameitaka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuwa na mfumo mathubuti wa kuratibu tafiti utakaosomana na Taasisi nyingine zinazofanya tafiti.

Agizo hilo limetolewa Julai 31, 2023 mjini Morogoro katika Kikao kazi cha kujadili usimamizi ya utafiti na maendeleo nchini ambapo amesema ili kutekeleza hilo kwa ufanisi Wizara itaunda kamati ndogo shirikishi ambayo itapitia maoni ya kikao kazi na kuangalia sheria mbalimbali za taasisi zinazohusu masuala ya tafiti ili kutoa mapendekezo.

"Utafiti ni muhimu kwa maendeleo ni vyema ukaratibiwa vizuri ili kupunguza milolongo ya kupatika kwa vibali vya kufanya utafiti na kuwezesha upatikanaji wa matokeo kwa urahisi," amesisitiza Prof. Nombo.

Katibu Mkuu huyo ameongezea kuwa ni muhimu kwa taasisi mbalimbali kujikita katika kufanya tafiti za pamoja ili kuleta tija, lakini pia kuhakikisha zinatenga fedha kwa ajili ya tafiti.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Prof. Maulilo Kipanyulu amesema kikao kazi hicho kinafanyika kwa kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ina jukumu la kutunga na kusimamia utekelezaji wa Sheria na Miongozi ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Utafiti

Naye Mshiriki wa Kikao hicho Makumu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka ameipongeza wizara kwa kikao hicho na kutaka kifanyike mara kwa mara ili kujadili vipaumbele, utekelezaji na matokeo ya tafiti katika maendeleo
IMG-20230731-WA0007.jpg
IMG-20230731-WA0012.jpg
IMG-20230731-WA0009.jpg
IMG-20230731-WA0011.jpg
IMG-20230731-WA0010.jpg
IMG-20230731-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom