Vijana wanasajili Bunifu Nchi Jirani

Blender

JF-Expert Member
Mar 5, 2022
3,428
5,284
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye @Nnauye_Nape amesema baadhi ya Vijana Wabunifu wa TEHAMA imewabidi wakasajili ubunifu wao katika Nchi za jirani sababu ya kutokuwepo kwa Sera ya Kampuni changa za TEHAMA (Startups) nchini.


“Kwa muda kidogo Sekta hii imekuwa haina mfumo mzuri wa kisheria wa kuratibu ubunifu wa Ki-TEHAMA hapa nchini na matokeo yake tunao Vijana wa Kitanzania ambao wanafanya ubunifu lakini wanalazimika kwenda Nchi jirani kusajili ubunifu wao na kuufanya ubunifu wao ufanye kazi na mfano mzuri ni Kijana mmoja wa NALA alifanya ubunifu mkubwa hapa na ikabidi aende kwa majirani zetu kusajili ubunifu wake”


Waziri Nape ameyasema hayo wakati akiongea na Vyombo vya Habari baada ya kufunga Kikao na Wadau Kujadili Ushirikiano wa Maendeleo Juu ya Sera ya Kampuni Changa za TEHAMA (Startups) Tanzania, Jijini Dar es Salaam.


“Kama Serikali tukasema inabidi tuwe na mfumo mzuri utakaotambua bunifu za hawa Vijana lakini pia uweze kuzilinda bunifu hizo ili pia waweze kuvutia uwekezaji nchini, tumekaa tumekubaliana na Wadau mbalimbali kutoka ndani na nje Nchi, tumeweka msingi na sasa tuko tayari kuendelea na hatua inayofuata”
#MillardAyoUPDATES
20231031_183629.jpg

Kumbuka hiyo nchi jirani ndio wamekubali huduma ya starlink, Huku yeye akimlitea zengwe tajir #1 duniani kwamba afungue ofisi Bongo ili kuwe eti kuwe na usalama wa data Kwa watumiaji.

Na startups nyingi kama costech ni wapiganaji Tu 😂
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye @Nnauye_Nape amesema baadhi ya Vijana Wabunifu wa TEHAMA imewabidi wakasajili ubunifu wao katika Nchi za jirani sababu ya kutokuwepo kwa Sera ya Kampuni changa za TEHAMA (Startups) nchini...

Kungekuwa na mazingira wezeshi kwa vijana hapa nchini, hao vijana huko nje wangeenda kufanya nini sasa? Serikali ijitafakari sana
 
Huyu jamaa hiyo nafasi hafai kuwepo.
kuna suala la paypal hana majibu
suala la gharama Za internet hana majibu .
starlink kawakataa

Hawa jamaa wapo kunufaisha matumbo yao tu.
Yani wanaongea as if hii nchi imeongozwa na chama tofauti.

hiyo issue ilitakiwa ifanyike muda mrefu
lakini saiv ndio wanaleta hoja kwamba wapo kwenye
mchakato siku zote walikua hawaoni?
kwahiyo hapa anataka asifiwe anasaidia vijana. foolish
 
Huyu jamaa hiyo nafasi hafai kuwepo.
kuna suala la paypal hana majibu
suala la gharama Za internet hana majibu .
starlink kawakataa

Hawa jamaa wapo kunufaisha matumbo yao tu.
Yani wanaongea as if hii nchi imeongozwa na chama tofauti.

hiyo issue ilitakiwa ifanyike muda mrefu
lakini saiv ndio wanaleta hoja kwamba wapo kwenye
mchakato siku zote walikua hawaoni?
kwahiyo hapa anataka asifiwe anasaidia vijana. foolish
Huyu ni chadomo Tu 😂, Hana akili na maarifa ya kufanya mageuzi Katika wizara Zaidi ya kujitafutia 10%
 
Kuna Fisi za Costech wanavizia Idea za watu na kishika mkono utakachokuwa unapewa.
Alafu utasikia serikali ya awamu hii imetoa pesa zote , kuendesha Miradi kumbe pesa ni wafadhili wa EU,
.
Tumetumia bilioni 1. Huku madogo wamepewa mil9, SEMA Tu 😂 unakuta kuna relative's, tunaamua kuuchuna
 
Ccm roho mbaya za husda, watataka kumuwekea nani mazingira rafiki ya kutengeneza pesa? Wao ndio kila kitu, umataka uanzishe jambo lako basi, basi watapanga foleni uwape rushwa milele bila ukomo.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Alafu utasikia serikali ya awamu hii imetoa pesa zote , kuendesha Miradi kumbe pesa ni wafadhili wa EU,
.
Tumetumia bilioni 1. Huku madogo wamepewa mil9, SEMA Tu 😂 unakuta kuna relative's, tunaamua kuuchuna
Nilipata nafasi ya kwenda Sabasaba na maeneo mengine ya maonesho, kuna unafki mwingi Sana waku wahadaa wadhamini toka nje.

Kimbembe wakiondoka.
mtiti kwako mpokea fungu la uwezeshi.😂
 
Back
Top Bottom