Mwamba 777
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 1,924
- 3,247
mkuu hapa umesema ukweli, tatizo hili yabidi kuwepo mwakilishi wa kuliwasilisha bungeni haraka sana.Serikali mara kwa mara imekuwa ikiwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kufaulu lakini jambo la kusikitisha unapofika wakati wa ajira serikali hiyo hiyo inawabagua tena.
Tumeona kwenye ajira za polisi wanaotakiwa ni wale ambao hawakufanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne. Yaani waliopata divisheni Four ila waliofaulu vizuri kwa kupata divisheni one na Two hawatakiwi.
Sanjari na hilo, kuna ubaguzi mkubwa unafanywa na serikali kwenye utoaji wa ajira hasa kwa wahitimu wenye elimu ya juu i.e bachelor degree holders kulinganisha na level zingine za kielimu kama vile diploma na certificate.
Mfano mimi nimehitimu kidato cha nne mwaka 2011. Kwakuwa nilikuwa na ndoto ya kufika mbali kielimu kama serikali inavyosisitiza, nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita.
Sikuishia hapo, niliendelea kukazana kwa nguvu zote na maarifa yote na hatimaye nikafanikiwa kuendelea na elimu ya juu na sasa ni mhitimu wa moja ya chuo kikubwa hapa nchini
Lakini katika yote, wenzangu niliomaliza nao kidato cha nne wakapata ufaulu wa divisheni Four kisha kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti leo hii ni waajiriwa wa serikali wanakula keki ya Taifa.
Niliomaliza nao kidato cha sita wakakosa sifa (qualifications) za kujiunga chuo kikuu wakaenda kusomea ualimu ngazi ya diploma tayari wote wameajiriwa serikalini
Lakini mimi niliyefuata ushauri wa serikali wa kusoma kwa bidii na kufaulu kwa kufikia kiwango cha elimu ya juu leo naonekana sina thamani kwani serikali ile ile iliyonihamasisha kusoma kwa bidii ndio ile ile imeniweka mtaani kwa takribani miaka minne sasa. Kwa maana nyingine kiherehere changu cha kusoma kwa bidii na kufaulu leo hii ndio kinaniponza kwa sababu kama ningefeli kidato cha nne au sita leo ningekuwa ni miongoni mwa wanaofaidi keki ya Taifa.
Mwisho wa yote kama serikali haina mpango wa kuajiri wahitimu wenye bachelor degree tunaomba itamke hadharani ilikusudi vijana tujue moja kwani hata ajira zinapotangazwa wenye bachelor degree wanaoajiriwa ni wachache sana tena nafikiri ni katika jitihada za serikali kuficha dhambi ya ubaguzi wanayoifanya isijulikane kirahisi.
Viongozi wengi ktk ngazi za juu ni mbulula na vilaza waliorisiti na kuunga elimu. Elimu zao ni za kuungia/ Kuungaunga. Unakuta kiongozi ana PhD, ila PhD yake ameipata kwa rushwa na kwa kujuana kisa tuu ni mbunge.
Hawahawa viongozi wamezaa mbulula na vilaza kama wao. Watoto wao ni form four failure, watu wa div four na zero. Hii ni kwaajili ya ugumu wa vichwa vyao kama vya baba zao na mama zao, then wanaungishwa certificate na diploma.
Hivyo basi ndo maana ajira na kazi nyingi wanapewa form four failure, div four, certificate na diploma maana wengi wao ni watoto wa viongozi.
Pia viongozi wanawakomoa wenye akili waliosoma moja kwa moja bila kuungia, kisa wao na watoto wao ni vilaza wanasoma kwa kuungia.
Hili swala ni la kusikitisha sana, wanaharakati na wabunge wenye akili timamu, ambao hawakuungia elimu walipeleke bungeni likadiskasiwe.