Mkuu Jasusi, hapa sasa ndio nimeanza angalau kukuelewa, kumbe Watanzania unaowazungumzia wewe, kuwa wamebadilika, ni hawa wenzetu wenye exposure kama hawa wengi wao waliomu humu jf!, hivyo umenishauri nami nitafute fursa ya kutoka nje ya Tanzania nami nijipatie exposure japo ya miezi miwili, hivyo nitakapo rejea nchini, mtazamo wangu, utakuwa umebadilika!.
Mimi nilimaani Watanzania wapiga kura zinazo matter, hawa ni wale wenzangu na mimi ambao watoto wao huweza kuvaa nguo mpya tena za mtumbani mara moja kwa mwaka, au siku ya Iddi, au siku ya Krismasi!. Watanzania hawa ndio wale wanaishi katika lindi la umasikini uliotopea, ambao wameaminishwa "mpaji ni Mungu", na wanaishi kwa kutegemea "riski kwa Mungu", na wameridhika na umasikini wao kwa sababu ndio walichopewa na Mungu.
Hawa ndio wapiga kura walio wengi, ni hawa ndio kura zao zinazo detetermine nani anakuwa rais wa Tanzania 2015!.
Watanzania hawa wakishagawiwa zile T-shirt na kofia, na kupewa shibe ya siku moja, huiona CCM ndie mkombozi wao waliyeletewa na Mungu awakomboe, na kwa sababu siku zote, CCM is the only party they've known tangu wengi wao wamezaliwa!, na hiki ndicho chama watakacho kipigia kura maisha yao yote!.
Kama mambo yenyewe ya kubadili mtazamo ni angalau lazima mtu kajieposure, nakuhakikishia, hizo kura za hao wote wenye hako kaji exposure, bado hazitatosha kuleta mabadiliko, unless wale wote wenye hivyo viji exposure, watashuka chini ground zero, na kuwahadithia wale wenzangu na mimi kuwa umasikini wao haijatokana na Mungu, kuna dubwana ambalo ndilo chanzo cha umasikini wao, na kama wasipoliondoa, wataendelea vivyo hivyo, kuzaliwa masikini na kufa masikini kwa kutegemea t-shirt, kofia na shibe ya siku moja dhidi ya njaa ya miaka mitano mingine!, CCM itaendelea kutawala!.