Serikali imenunua tena mashangingi 26 mapya kimya kimya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imenunua tena mashangingi 26 mapya kimya kimya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by imamu, May 27, 2012.

 1. i

  imamu Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna usemi wa kiswahili usemao sikio la kufa halisikii dawa. Usemi huu hulenga matendo (ya watu/mtu/kitu) ambayo hujirudia rudia huku yakiwa hayana faida kwa mtu husika pia kwa walengwa wake.

  Hii ni CCM na serikali yake hapa Tanzania. Pamoja na serikali kujinadi mahala pengi ikiwemo bungeni kuwa itaachana na ununuzi wa magari ya kifahari maarufu kama mashangingi a.k.a Kilimo Kwanza, inaonekana ununuzi wa magari hayo ni ugonjwa sugu na unaendelea kuitafuna CCM na serikali yake.

  Inasemekana magari hayo yamenunuliwa tena kwa fujo safari hii kwa wateule wa hivi karibuni wakuu wa mikoa, wilaya na baadhi ya mawaziri. Kama kweli serikali ilikuwa na nia ya dhati ya kutoendelea na ununuzi wa magari hayo ya kifahari, basi ingeanza na wateule wa hivi karibuni kwa kuwanunulia RAV4 za bepari Pinda anayejificha kwenye kivuli cha mtoto wa mkulima.

  Hii ni kuipa ujiko CHADEMA? Au mmetumwa kuiua CCM kwa makusudi? Au mnataka kuiua CCM ili Nyerere asahaulike?
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ngoja 2015 tuwape kubwa
   
 3. M

  Masabaja Senior Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM inaumwa ugonjwa wa matumizi labda wapate mganga
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,519
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi wameshapewa mikopo yao?
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hata Mbowe kalichukuwa lake alilojidai kulirudisha, tena kalirudia kimya kimya.
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Si limenunuliwa kwa kodi za wananchi wa nchi hii. Acha alitumie kwanini atumie gari lake binafsi.
   
 7. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Katika hayo matumizi ya kununua magari, nyuma ya pazia kuna siri nzito, ila sio muda mrefu watanzania watajua tu.
   
 8. N

  Nyuki baby Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pesa zetu izo jamani mhh!
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,334
  Trophy Points: 280
  Sio kweli kuwa imeyanunua kimya kimya, tenda ilishatangazwa zamani mara baada ya uchaguzi wa 2010 na Toyota Tanzania Ltd ndio walishinda!.

  Kila miaka 5 mitano serikali inayoondoka huondoka na magari yao na serikali mpyahuja na mapya!. Hata wabunge japo wangi wamerudi wale wale, zile milioni 100 za kununulia gari jipya kila mbunge amepata!. Mwaka mmoja kabla ya kuvunjwa bunge, Spika Sita alinunuliwa benzi mpya S Class 500 nyeusi. Mama Makinda naye kanunuliwa mpya S- Class 350!.

  Wakuu wa wilaya mpya, wale manaibu wapya na wajumbe wa Kamati ya Kukusanya Maoni ya Katiba pia nao mashangingi mapya ni stahiki zao!.
   
 10. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Balaa gani mimi sionekani, nami nipate japo Vokswageni jamani!
   
 11. Codon

  Codon JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama nikweli,I NAUMA MNO!Lakini kunasemi zababu zetu,Ukiona giza linazidi ujue asubuhi inakaribia pia Mbio zasakafuni mwisho wake kwenye ukingo!
   
 12. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu Pasco. Ishu ya msingi hapa ni ununuzi wa hayo 'mashangingi'. Serikali ya Pinda ilihaidi kupunguza ununuzi wa magari hayo, inamaana wangenunua Nissan au aina nyingine. Lkn hali halisi, magari hayo yameendelea kununuliwa, tena kwa fujo sana, sasa hapa kunakuwa na contradiction kwenye ile ahadi ya pinda. Pia, kuhusu swala la staili za viongozi, kiongozi ana staili ya gari, lakini sio lazima liwe shangingi, hata RAV4 anaweza kutumia. Hii tabia ya kununua mashangingi ni kasumba tu ya serikali ya ccm, isiyokuwa na uchungu na wananchi wake...
   
 13. Maendeleo tu

  Maendeleo tu JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kuna wilaya zinazotumia umeme wa majenereta sasa hivi ni mgao wa kufa mtu kisa hakuna hela za kununulia mafuta. huu ujasiri wa serikali kutumia kodi zetu kununua haya mashangingi unatoka wapi!!!??? anyway, time will tell...
   
 14. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  CCM CCM shika mkia., piga vita maendeleo na uadilifu ah ah ccm kufa kabisa..
  Kwa ccm, kuwaletea wananchi maendeleo siyo priority. Kwao matumbo yao, ujinga kwa wananchi na amani fake ndiyo vipaumbele
   
 15. K

  Kosmio Senior Member

  #15
  May 27, 2012
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 128
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pasco
  Mh. Lukuvi alivyokuwa anatoa taarifa kuhusu kuachana na magari ya kifahari bila shaka alijua kuwa ni stahiki yao.

  Cha msingi kama serikali iko serious na statement zinazotolowa hadharani basi ni vema hayo magari ya kifahari yauzwe na atekeleze aliyoyasema.
   
 16. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu if you still believe in Pinda political rhetorics then you are doomed. Jamani ni kwamba serikali haifanyi kazi kwa kauli za majukwaani za viongozi. Serikali inafanya kazi kwa kupitia waraka/secular. Kuna waraka wa serikali ambao unatumika hadi hivi sasa unaelekeza aina ya magari wanayotakiwa kununuliwa mawaziri, makatibu wakuu, RCs, DCs etc. Mpaka hadi Ijumaa waraka unaotumika ni ule wa zamani (Mashangingi).

  Pinda angekuwa na nia ya dhati ya kupuguza matumizi ya serikali kwa kununua magari ya bei nafuu, angepeleka hoja hiyo kwenye baraza la mawaziri. Na kama ingepita basi waraka/secular mpya ingetoka inayoelekeza ununuzi wa magari ya viongozi. But PM is weak can't do that because he knows atakutana na vipingamizi ndani ya baraza la waziri, Because the Kikwete government is addicted in SPENDING.

  Ndiyo maana hata mwaka ule alipokataa shangingi bado alinunuliwa shangingi na kuletewa. To save his face akalikataa eti wapewe wengine, lakini he coudn't do anything kwa mtu aliyenunua hilo shangingi. kwasababu anajua they guy was correct, yeye Pinda ndiye anacheza politics.

  Kenya wameweza kwasababau ni suala liliokubaliwa kwenye baraza la mawaziri na kuwekewa muongozo/secular na hakuna anayethubutu kuuvunja huo muongozo. i.e kumununulia kiongozi shangingi

  Nyinyi ambao mnaendelea ku-buy hizi political rhetorics za Pinda kalaghabaho. Jamaa hana nia kabisa anawazuga. Hizi zote ni dalili za chama kinachoelekea kufa hakisikii cha muazini!
   
 17. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu umesema kweli kabisa, wenzetu Kenya hakuna waziri wala nani anayetumia shangingi. Wabunge wote walipewa Volkswagen na maofisa wengine wa serikali wanatumia Corolla. Wanabana matumizi, sisi tunaongeza matumizi.

  Tiba
   
 18. K

  Kosmio Senior Member

  #18
  May 27, 2012
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 128
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Funny govt.
   
 19. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  CCM is like the Roman Empire....it will collapse very soon
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mbona alijidai analirudisha?
   
Loading...