Serikali imenunua tena mashangingi 26 mapya kimya kimya!

nadhani procurement ya haya magari ilishaanza kabla ya tamko

kinachositikitisha ni PINDA kama PM anajua kinachoendelea na amekaa kimya, sijui na yeye anapokea lile shangingi la 51?
 
Nchi wahisani wako very much concerned kuhusu exta vagant spending za serikali kwa bidhaa za anasa, vitafunwa, na posho lukuki.

Uingereza ndie biggest contributor wa General Budget Support kwa kutoa 60% na nchi nyingine kujazia hiyo 40 %!. Nilipopata fursa kumuona Mama Balozi, Diane Corner, nilimuuliza kama ni kweli mna uchungu na government spending na jinsi wanavyotapanya fedha za wahisani, kwa nini wanaendelea kuongeza mwaka hadi mwaka huku tukizidi kuzitapanya, alipiga chenga na kudai they are just generous!.

Kwenye uchaguzi mkuu wakatoa bilions, wakati huo idara ya mpiga chapa mkuu ilikuwa na uwezo wa kuchapisha karatasi za sensa, kufuatia "he who pays the piper may call the tune" Tenda ya kuchapisha karatasi za kura ilitokewa kwa Kalamoo, ni kampuni ya Uingereza, vifaa vyote vya uchaguzi ni imported from UK!, zile fedha za msaada zimerudi zilikotoka!.

Mpaka kesho Uingereza ndie biggest donor wetu na sasa ndie anaeongoza kwa DFI kwa Tanzania kupitia BG kwenye uchimbaji gesi asilia kule Mtwara, hivyo maadam serikali ya Tanzania wanapenda pipi za mashangingi, waacheni walambe utamu wa pipi na sisi tupate kilicho chetu!.

Pinda ni very genuine kwenye kupunguza matumizi ya anasa, wenzake hawataki na chini ya collective resiponsibilities, amejinyamazia!. Pinda alitaka kumwajibisha Jairo, mwenyewe akataa!. Pinda baada ya kumsimamisha Mama Nyoni na Dr. Mtasiwa, alimshauri Waziri na naibu wapigwe chini, mwenyewe alikataa, sasa mnataka afanye nini?.

Kwenye expenditure ya starehe mmeyaona mashangingi tuu?. Hamjanote fleet ya SUV za state house sasa ni BMW x5 na sio Toyota tena?!. Hamjanote zile pikipiki za kumpamba Amiri Jeshi Mkuu pale uwanja wa Taifa siku hizi ni BMW 1.100 cc kila moja ikiuzwa kwa milioni 35 badala ya zile Honda CB 750 cc ambazo zilikuwa ni milioni 15 tuu!.

Zamani computers za serikali ni Dell za wastani wa milioni 2, sasa ni Mac Books na ma I-Mac milioni 5 each!.

Hii ndio Tanzania yetu ya kisasa, kila waziri siku hizi ni mwendo wa I pad na simu ya I- phone 4gs au Samsung Galaxy Tub!.
 
Tutamlaumu Pinda kwasababu UKWELI unaufahamu lakini anatupiga kila leo CHANGA la macho. Ooh Serikali itaondokana na ununuzi wa mashangingi wakati anajua sio kweli.

BTW, kama analotetea analiamini kwanini basi bado yuko kwenye serikali ya mafiadi? naye ni yule yule hana jipya.
 
By Mkinga Mkinga | The Citizen Reporter- Dar es Salaam | Monday, 13 August 2012

The government seems to have started off on the wrong foot in its resolve to stop purchasing expensive vehicles.

Checks by The Citizen have established that recently the government received a fleet of 26 Toyota Land Cruiser V8 vehicles. Reports availed to this newspaper confirmed that the costly vehicles, also expensive to maintain, have been bought for the ministry of Justice and Constitutional Affairs for the Constitution Review Commission (CRC).

Going by the price of Sh150 million per vehicle, it means that the purchase has cost the government Sh4.2 billion.
(mhhhh! bado hatujaweka operating & maintenance cost)

Speaking exclusively to The Citizen the minister for Justice and Constitutional Affairs, Mr Mathias Chikawe, admitted that the government has bought the 28 vehicles to cater for members of the CRC to effectively discharge their responsibilities.

"Yes we have bought about 26 new vehicles after we bought two earlier for the chairman and his deputy... but the second batch consists of about 26 and will be used by commission members and supporting staff in collecting views on the new constitution," minister Chikawe said

He said his ministry was involved in buying the vehicles for the commissioners because since the last financial year the constitutional review commission had no government vote which would have allowed the purchase of facilities for the exercise.

The move comes only weeks after the Prime Minister, Mr Mizengo Pinda, told the nation that the government had resolved to do away with expensive vehicles. He said from now on it would purchase vehicles with engine capacity of 2000cc from the 3000cc which were a norm.

Tabling his office budget in august House in Dodoma, the Premier said the government plan to do away with cars which cost more for their maintenance.

Asked why his ministry had bought the vehicles against Mr Pinda's statement, Mr Chikawe said:

"The order for the vehicles was made before the Prime Minister's statement... we have decided to buy vehicles which would withstand our kind of roads because they will take the commissioners to remote areas."

He said after the CRC finishes its work, the government might decide to auction the vehicles.
(Watauziana mafisadi wenyewe)
 
Madaktari na Walimu waliambiwa na hii Serikali dhalimu, "Serikali haina uwezo." wa kuongeza ujira na posho zenu wakati huo huo wamemwaga mabilioni ya pesa kununua magari ya kifahari.
 
Niliacha kuamini yanayosemwa na serikali hii long time ago. Naangalia tu yanayotendwa.

Inasikitisha kusema kweli halafu bado watakuwa madarakani kwa miaka mingine mitatu wakiendeleza udhalimu wao wa kuliangamiza Taifa.
 
Halafu Warioba bado ana usafiri mwingine wa serikali kama Waziri Mkuu mstaafu.

Asilimia zaidi ya 90% ya wajumbe wa hiyo tume wana usafiri wao. Na utaratibu ungeweza kuwekwa ili watumie magari ya wakuu wa mikoa na wilaya ili kuepuka gharama kubwa kama hizi lakini hii Serikali fujaji haikuliona hilo.
 
Na CDM nao wanataka kununua magar zaidi ya 100 brand new kuzunguka nchi nzima. Sample za magar yenyewe yote yana CC zaidi ya 3000, meaning hata consumption ya mafuta na general maintainence inakuwa juu.

Hawa wapinzani nilifikiri wangeonyesha njia kwa chama tawala, but nao wameenda mle mle! Hamna wa kumnyooshea kidole mwenzake.
 
You are the biggest damn liar I have ever come across. Shame on you.
 
Kwa vile Watanzania huwa wanawachagua watu kutokana na kuwatazama usoni na kuyasikiliza maneno yao matamu, majaaliwa ya CCM kuendelea kutawala ile miaka 50 mingine tuliyoelezwa humu, yanategemea atajayesimamishwa na sio sio matendo ya CCM na serikali yake katika miaka 50 iliyotangulia!.

Japo matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno, Watanzania walio wengi huridhika na maneno matamu ya uwongo na hadaa za CCM mwaka hadi mwaka, ukijumlisha na ile hali ya umasikini uliotopea wa Watanzania walio wengi, zile zile T.shirt na kofia, na ile shibe ya siku moja ya kuamkia siku ya election ave, inatosha kutuletea matokeo yale yale nasi tukiendelea na nyimbo zetu zile zile huku miaka ikizidi kukatika!.

Huu ni sehemu ndogo tuu ya ukweli mchungu tunaousubiria 2015!.

"Mark my words"!.

God Bless Tanzania.

Pasco.
 
Na CDM nao wanataka kununua magar zaidi ya 100 brand new kuzunguka nchi nzima. Sample za magar yenyewe yote yana CC zaidi ya 3000, meaning hata consumption ya mafuta na general maintainence inakuwa juu.

Hawa wapinzani nilifikiri wangeonyesha njia kwa chama tawala, but nao wameenda mle mle! Hamna wa kumnyooshea kidole mwenzake.
Ni aina gani?
 
Matatizo ya wananchi utayajua kwa kukaa ofisini? Ndio maana CDM haijengi ofisi kwasababu haina muda wa kukaa humo Kama nyinyi magamba
 
Badala ya kukemea haya madudu ya magamba ambayo yameshatendeka unakuja na usanii ambao huna ushahidi wowote ule wa kuthibitisha kile ulichoandika...ali mradi tu uwanyooshee kidole CHADEMA badala ya magamba!!!!

Na CDM nao wanataka kununua magar zaidi ya 100 brand new kuzunguka nchi nzima. Sample za magar yenyewe yote yana CC zaidi ya 3000, meaning hata consumption ya mafuta na general maintainence inakuwa juu.

Hawa wapinzani nilifikiri wangeonyesha njia kwa chama tawala, but nao wameenda mle mle! Hamna wa kumnyooshea kidole mwenzake.
 
Na CDM nao wanataka kununua magar zaidi ya 100 brand new kuzunguka nchi nzima. Sample za magar yenyewe yote yana CC zaidi ya 3000, meaning hata consumption ya mafuta na general maintainence inakuwa juu.

Hawa wapinzani nilifikiri wangeonyesha njia kwa chama tawala, but nao wameenda mle mle! Hamna wa kumnyooshea kidole mwenzake.

KWani wapinzani wanatumia pesa za serikali kununua magari hayo?
Nadhani issue hapa ni nani analipia hayo magari.
Kama ni pesa ya kutoka CDM, kuna tatizo gani?
Usipoteze mada ya hapo juu.
Warioba na wenzake hawahitaji V8 kwenda vijinini.
Kwani wananchi wa huko vijijini wakihitaji kwenda kwao wanatumia V8?
 
Badala ya kukemea haya madudu ya magamba ambayo yameshatendeka unakuja na usanii ambao huna ushahidi wowote ule wa kuthibitisha kile ulichoandika...ali mradi tu uwanyooshee kidole CHADEMA badala ya magamba!!!!

Mshikaji yupo kazini, anapoteza mada...
 
Back
Top Bottom