Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Nn 10 je tuliobomolewa nyumba za Milioni 450 je Fanya kama umetoa sadaka,ndo serikali ya wanyonge na wanyonge ndo sisi
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.
 
Kama ulinunua kibiashara na hukukiuka taratibu za biashara basi huna haki ya kunyanga'nywa lakini kama wewe ni mmoja wa kina Kangomba ni vyema ukayapata machungu waliokuwa wanayapata wakulima.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Namuunga mkono Magufuli kwenye mengi, lakini kwa hili la korosho.
Ingawa wengi kwa namba watafaidika lakini limejaa dhulma na litamtia doa siku zote.
Hawa jamaa wajiunge wakaishtaki serikali kwa unyang'anyi.
 
Kila nikirudia kusoma humo nilipoweka Red naona sielewi kama ulienda kwa lengo la kwenda kununua korosho huko kusini au ulikuwa unapita tu ukaombwa na wakulima wa korosho ununue korosho zao?

Hivi ukimkuta teja ana msokoto akakuomba akuuzie ana kiu ya maji nawe ukanunua ukakaa na msokoto dola ikaja ikakukuta nayo utajielezea vipi?
Aliyekutwa na ngozi ndiye mwizi..! Wewe ulienda kusini kulangua korosho na ulanguzi ni kosa.
Why korosho ndo iwe haramu??? Watu pia wana mahindi, mchele, kahawa, ndizi, maharagwe n.k na wote hawana mashamba mbona hamjawakamata???

Una roho mbaya sana kama dikteta wako
 
We tatizo sio mtu wa kujiongeza, bila kuwa mbunifu huwezi kutoboa

Kuna rafiki angu naye yupo huko aliposikia tu korosho zitataifishwa kwa wasio na mashamba akapagawa

Nikamwambia tafuta mzee mwenye shamba mrithishe hizo korosho we kaa pembeni, mambo yalienda mswano anasubiria kibunda chake

Kumbuka wanyonge ndio hufa
 
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.
Anayetaka kujitoa mhanga hatangazi utasikia tu kimewaka!
 
Mzee meko kule ameenda kuchungulia fursa lengo sio kwenda kutetea wanyonge mimi toka alivyofinyia kwa ndani hela za wahanga bukoba nimemtoa thamani kabisa
 
Wakilipwa na wa rambirambi watalipwa wastay tune
Baba yangu jee ulikuwa na leseni ya biashara??????????????
Kisheria inawezekana kuwa wewe ni mlanguzi kwa sababu huna shamba wala leseni ya biashara hiyo.
Ninadhani mwisho wa siku mtalipwa ila jamani tujifunze kufuata sheria na taratibu zake.
 
Hivi story hii uongo wake na wa yule anayesema tunajenga reli na mradi wa Rufiji kwa hela zetu kumbe hazina kuko chwee mpaka waziri wake analia "wanaume" wamesitisha Misaada ni yupi muongo mwenye athari kwa nchi?
Halafu ni aibu unaaminiwa na raia kisha unakuwa mtu wa fix!
You have spoken all, I like it
 
Hivi mfano nikiwa na tani 10 nikamuuzia mtu tani tani 2 nikijua kuwa inayobaki nitalipa deni kwenye hivyo vyama vya ushirika nitakuwa nimefanya kosa? Hivi wakulima wote hukopa pembejeo? Hivi mkulima anawezaje kukwepa deni la pembejeo huku akijua mwakani atazihitaji, kwenye tumbaku middle men wapo sana kinachofanyika ni kwamba mkulima anabakiza kiasi ambacho atawalipa hao wa ushirika.
Sijawahi kusikia vyama vya ushirika vikilalamika kudhulumiwa na wakulima.
iko hivi hawa wakulima wana vikundi kama utalaza deni basi linagawiwa kwa kukundi kuzima kilishindwa kulipa linagawiwa kwa kijiji kikishindwa lipa libabebwa na chama (mara nyingi ni ngumu kufika huku) ndo maana ujawah sikia chama kikipata hasara

II. unajuaje izo korosho zinalipa deni ikiwa weww hujui ubora wake na zitauzwa vp? aya hata ukijua unauza kimakosa kwa kuwa inafaa upeleke zote maana ndo makubaliano yenu.
a
kwenye tumbaku hakuna mtu wa kati na haruhusiwi sema tumeishi hivyo kimazoea

maana iyo tumbaku tu kuchukua pembejeo chache na kuja ma mzigo mkubwa unao zidi maradufu makisio ni makosa. pia mkulima A kuchukua pembejeo na tumbaku kuuzia kwa mkulima B ni makosa maana anakwepa deni na kuwabambikia wanakikundi wake.

unashangaa mkulima kukwepa deni la pembejeo (wanakikundi hulilipa deni hilo maana wamedhaminiana) na mwakani atapewa na ile hela (deni alilokopa) atakatwa na litaenda kwa walio mlipia (wanakikundi)

mkuu hayo mambo kifupi ni ulanguzi hakuna haki kwa wafanyayo hayo ila huruma tu
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Mkuu pole sana ila naomba urekebishe hapo unasema unaichukia Tanzania pasomeke unamchukia jiwe.... Jiwe ndiye chanzo cha haya yote piga moyo konde 2020 sio mbali
Yeye pia sio chanzo chanzo ni katiba chakavu ya nyerere ndio imetufikisha hapa,tunataka katiba mpya ya kizazi cha sasa ili yakitoka madarakani yaozee jela.
 
Kwani mkuu hakuna pakwenda kushtaki?????
Jalibu kushtaki au tafuta au sambaza taarifa hizi kwenye tv watanzania wengine wasikie.
Hana pa kushtaki mkuu, hii nchi unaijua. Watoa haki wamewambia madiwani wa chadema uko Magu kuwa ni marufuku majengo ya serikali kutumiwa na vya vya siasa.
Hivi wajua kinacheoendelea ikulu jana na leo.....
You better shut up your chicken mouth... BICK
 
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.
Pole mkuu,nahisi vile unavyojisikia! Pole Sana Mtanzania mwenzetu
 
Mimi Kuna Jamaa alinipanga nimkopeshe million mbili Roho ilisita Sana hadi Jamaa alinikasirikia Sana ila niliposikia haya mambo ya utaifishaji nilimuendea faster nikamwambia bora aukununua korosho zingepotea.... Jamaa anashukuru Sana mm kumnyima pesa anasea angechanyikiwa kama ingekuwa ni yeye. Ili swala ni hatari kwa ustawi wa maisha ya mtu mmoja mmoja
 
Back
Top Bottom