Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Kwani aliwalazimisha?

Amefanya kosa lolote kwa uamuzi wake huo wakununua kuhifadhi ili baadae aje kuuza kwa bei kubwa zaidi?
Pole sana Mkuu..ila hiyo uliyokuwa unafanya ndio KANGOMBA..yaani unanunua korosho kwa mkulima kwa shilingi 1000 ili wewe uje kuuza kwa 3300. Japo umesema hukuwa unawalazimisha ila ulitumia shida za wakulima kujinufaisha. Suala lako linafanana na utetezi wa kufanya mapenzi na binti chini ya miaka 18, hata kama ulimtongoza na kukubaliana lakini sheria itakuambia umebaka.
 
Katika yote aliyoandika Mwanasheria wewe umeguswa na hayo tuu??

Yaani hauna hata ushauri wa kisheria kwa middlemen Huyu anaewakilisha wenzake wengi tu wahanga wa uamuzi wa serikali hii.??!

Sad
Kwani ameomba ushauri wa kisheria Mkuu katika mada yake?
 
Hapo ndio umeona pa maana?? QUOTE="Petro E. Mselewa, post: 29659204, member: 116264"]Bihashara=biashara; gafra=ghafla. No further comments[/QUOTE]
po
 
Najua Umeandika Ikiwa Kila Asomaye Akiumia
Kuna Neno Hili Ndiyo Utakaloitwa Kangomba
 
Habari yenyewe inaonekana ya kutunga na ya uchochezi. Eti mstaafu kanionea huruma kanikopesha million 10? Nani anaweza kukukopesha million 10 bila dhamana! Acha uongo hii story yako ya uongo
 
Pole sana, ila kwenye para ya mwisho naomba neno Tanzania lisomeke 'serikali', usiichukie nchi yako bali unaweza kuichukia serikali iliyopo. Asante.
Na atambue kuwa kuichukia serikali iliyo madarakani sio kosa bali kosa ni kuichukia nchi yako. Kuna sababu gani za kuipenda serikali kama imeingia madarakani kwa ulaghai, inaendesha dhuluma, mauaji na kuminya uhuru wa raia?
Hata mkoloni tuliyekuwa tunamchukia na kujiunga pamoja kumtoa kuna mambo alikuwa na nafuukuliko utawala huu haramu
 
Pole sana Mkuu..ila hiyo uliyokuwa unafanya ndio KANGOMBA..yaani unanunua korosho kwa mkulima kwa shilingi 1000 ili wewe uje kuuza kwa 3300. Japo umesema hukuwa unawalazimisha ila ulitumia shida za wakulima kujinufaisha. Suala lako linafanana na utetezi wa kufanya mapenzi na binti chini ya miaka 18, hata kama ulimtongoza na kukubaliana lakini sheria itakuambia umebaka.
Serikali haina tofati na kangomba, inatumia shida za wafanyakazi kujinufaisha na mafao yao, niichangie kwa miaka 35 inakaa na pesa zangu bila riba leo nimezeeka inaniona wa nini kama siyo wizi ni nini.
 
Bihashara=biashara; gafra=ghafla. No further comments

Msomi unaargue semantics sasa badala ya substance.

Umewahi kupata huduma kwa wenyeviti wa vijiji jinsi wanavyoandika?

Tatizo mkishasoma na kufika vyuoni huwa mnadhani kila mtanzania ni elite kama nyinyi kwa hiyo anaweza kujieleza ipasavyo kwa maandishi

Mleta mada anawakilisha kundi la watanzania wengi wa hali ya chini wewe umeshindwa kuling'amua hili
 
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.
Kila nikirudia kusoma humo nilipoweka Red naona sielewi kama ulienda kwa lengo la kwenda kununua korosho huko kusini au ulikuwa unapita tu ukaombwa na wakulima wa korosho ununue korosho zao?

Hivi ukimkuta teja ana msokoto akakuomba akuuzie ana kiu ya maji nawe ukanunua ukakaa na msokoto dola ikaja ikakukuta nayo utajielezea vipi?
Aliyekutwa na ngozi ndiye mwizi..! Wewe ulienda kusini kulangua korosho na ulanguzi ni kosa.
 
Pole sana Mkuu..ila hiyo uliyokuwa unafanya ndio KANGOMBA..yaani unanunua korosho kwa mkulima kwa shilingi 1000 ili wewe uje kuuza kwa 3300. Japo umesema hukuwa unawalazimisha ila ulitumia shida za wakulima kujinufaisha. Suala lako linafanana na utetezi wa kufanya mapenzi na binti chini ya miaka 18, hata kama ulimtongoza na kukubaliana lakini sheria itakuambia umebaka.

Mkuu hivi nikinunua mchele kyela na kuuleta Dar nitaulizwa nimelima wapi?
 
Back
Top Bottom