Serikali yazifunga akaunti 191 za wakulima wa korosho.

Serikali yazifunga akaunti 191 za wakulima wa korosho.

Bhikalamba

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2015
Posts
2,341
Reaction score
3,367
Hatua hiyo ya serikali imetangazwa na waziri wa kilimo mh. Japhet Hasunga alipokuwa akihojiwa na gazeti la citizen.

Waziri Hasunga kasema hatua hiyo ya kufunga akaunti hizo ni kwa lengo la kupisha uhakiki. Akitoa ufafanuzi alisema kuna baadhi waliuza kilo zaidi ya 1500 na kwa utaratibu mkulima anapaswa kuonyesha umiliki wa shamba la korosho.

My take:
Kwa utaratibu huu tutegemee baadhi kugeuka ombaomba kwa muda maana ndani ya akaunti kuna fedha za akiba kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na ada.

Wito wangu kwa waziri atengenze utaratibu ambao hauta athiri MTU kudraw fedha za matumizi kutoka akiba yake wakati wakiendelea na uhakiki.

======

Dar es Salaam. Serikali imefunga kwa muda akaunti 191 za benki zinazomilikiwa na wakulima wa korosho kupisha uhakiki wa kina wa umiliki wa korosho walizouza.

Uamuzi huo unakuja wakati ikiwa imeshaingiza Sh3.8 bilioni kwenye akaunti hizo katika mfululizo wa uhakiki na ulipaji wakulima wa zao hilo unaoendelea nchini.

Akizungunza na gazeti la The Citizen, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema wakulima wenye akaunti hizo wameuza zaidi ya kilo 1,500 kwenye vyama tofauti vya msingi, hivyo ni lazima umiliki wa korosho walizouza uhakikiwe.

“Hatua hii ni muhimu (ya kufunga akaunti hizi kwa muda) ili kupisha uhakiki kwa sababu utaratibu unataka mkulima aliyeuza zaidi ya kilo 1,500 za korosho aonyeshe shamba lake lilipo kwa timu yetu ya uhakiki,” alisema Hasunga

“Lakini uchunguzi wa awali umeonyesha kuna baadhi ya wakulima wameuza kiasi kinachofikia kilo 3,000 za korosho kwenye vyama vya msingi tofauti.”

Hata hivyo, waziri huyo alisema Serikali bado haijapata kiasi halisi cha korosho ambacho wamiliki wake wameshindwa kuonyesha mashamba yao, lakini alisisitiza kuwa tatizo hilo bado ni kubwa. Akizungumzia uhakiki na malipo kwa wakulima, alisema tayari Sh206.092 bilioni zimeshalipwa kufikia Disemba 27 kati ya hizo, Sh188.378 bilioni zilikuwa zimewafikia wakulima kabla ya sikukuu ya Krismasi.

“Wakulima 100,534 wameshalipwa bila kujali ni mara ngapi walipeleka korosho kwenye chama cha ushirika cha msingi. Wakulima hawa wanatoka katika vyama vya msingi 398 kati ya vyama 617 vilivyosajiliwa nchini na vyama 504 vinavyopatikana katika mikoa mitatu ya Mtwara, Lindi na Ruvuma,” alisema.

Alisema tani 188,799. 4 za zao hilo zimeshakusanywa katika maghala mbalimbali na kwamba tani 30,226.25 zimehamishiwa kwenye maghala mengine ili kutengeneza nafasi korosho zilizo mikononi mwa wakulima kupokewa. Takwimu za Serikali zinamaanisha kuwa Sh206.092 bilioni zilizotolewa ni malipo kwa tani 62,452.333 kati ya tani 188,799 zilizokusanywa na tani 126, 347.07 zinasubiri mchakato wa malipo. “Mchakato hautakamilika mwisho wa mwezi huu kama tulivyotarajia kutokana na changamoto zilizojitokeza, matumaini yetu ni kwamba uhakiki na malipo yatakamilika mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.”

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wilayani Tandahimba (Tafa), Faraji Njapuka alisema licha ya wahalifu kuingilia biashara ya korosho, wapo wakulima wanaovuna tani tano hadi 10 kwa mwaka.

“Tunachanganywa na takwimu za Serikali kuhusu malipo yaliyofanyika hadi sasa kwani kinachoelezwa hakiakisi ukweli uliopo miongoni mwa wakulima. Baadhi ya Amcos zetu hazijapokea fedha yoyote hadi sasa,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (Tanecu), Shaibu Aifai alisema mpaka sasa hali ya wakulima ni mbaya.

Meneja wa Chama cha Ushirika cha Masasi na Mtwara (Mamcu), Protence Rwiza alisema malipo yanayotolewa hayaakisi jumla ya tani 61,000 zilizohakikiwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Watu wameuza korosho sio madawa ya kulevya au vitu haramu mnawasumbua utadhani wameuza nini sijui...Mnyaazi Mungu awasaidie mpate busara na hekima katika maamuzi yenu naona Elimu zenu haziwasaidii hata kidogo...
Yaani haya ni mambo ya ajabu kabisa, hivi hakuna utaratibu mwingine? ambao hautamuathiri mkulima?na huo uhakiki utachukua muda gani?ili aweze kulima msimu unaofuata, je akionekana hana hatia mtamlipa hasara?
 
Hatua hiyo ya serikali imetangazwa na waziri wa kilimo mh. Japhet Hasunga alipokuwa akihojiwa na gazeti la citizen.

Waziri Hasunga kasema hatua hiyo ya kufunga akaunti hizo ni kwa lengo la kupisha uhakiki. Akitoa ufafanuzi alisema kuna baadhi waliuza kilo zaidi ya 1500 na kwa utaratibu mkulima anapaswa kuonyesha umiliki wa shamba la korosho.

My take:
Kwa utaratibu huu tutegemee baadhi kugeuka ombaomba kwa muda maana ndani ya akaunti kuna fedha za akiba kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na ada.

Wito wangu kwa waziri atengenze utaratibu ambao hauta athiri MTU kudraw fedha za matumizi kutoka akiba yake wakati wakiendelea na uhakiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
2020 hawa jamaa wanajikaanga wenyewe kwa mafuta yao
 
Watu wameuza korosho sio madawa ya kulevya au vitu haramu mnawasumbua utadhani wameuza nini sijui...Mnyaazi Mungu awasaidie mpate busara na hekima katika maamuzi yenu naona Elimu zenu haziwasaidii hata kidogo...
Mkulima alikipwa chake na mtu wa kati lakini mkulima bila aibu anadai alipwe tena huo ni wizi na pia ipo Rushwa mpya imeibuka kwenye uhakiki mashamba, ukiwa na pesa wanakuandikia kuwa wamehakiki shamba lako na ukilipwa wanakula 10% Serikali inafanya vioja pesa inayotumika kutengeneza Sinema ni kubwa kuliko biashara ilivyokuwa hapo Awali
 
Yaani haya ni mambo ya ajabu kabisa, hivi hakuna utaratibu mwingine? ambao hautamuathiri mkulima?na huo uhakiki utachukua muda gani?ili aweze kulima msimu unaofuata, je akionekana hana hatia mtamlipa hasara?
MTU amekuuzia mzigo ukachukua, halafu linapokuja suala la kumlipa unaleta hoja ya kuhakiki eti kama aliyekuuzia anashamba!! This is absurd.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom