Nakubali Serikali haiwezi kutuwekea pesa mifukoni lakini basi irahisishe mazingira ya kuzipata

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nisikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane!.

Bila shaka mtakubaliana na mimi ya kwamba hakuna serikali itakayokuwekea fedha mfukoni bali inapaswa kama raia uamke uende ukazitafute kwa kupambana kwa kufanya kazi,hili na mimi naliunga mkono kwa asilimia 100 kabisa,lakini swali langu ni Je,Mazingira ya upatikanaji wa pesa hiyo kwa urahisi yamewekwa na Serikali?.Kwa wale mliokaa na mnaokaa ughaibuni(Marekani,Uingereza,Ujerumani,Canada n.k)nadhani mnaelewa urahisi na ufanisi wa serikali za wenzetu uliowekwa dhidi ya watu wake namna ya upatikanaji wa pesa na hivyo hata ukusanyaji wa kodi kutoka kwa raia wao hakuna ambaye anapiga kelele.

Wenzetu wamefanya Mapinduzi ya kiuchumi katika kila secta hivyo inakuwa rahisi kwa watu wao kupata kipato kwa urahisi na kuifanya serikali kuchukua kodi kwa urahisi na ndiyo maana kila mtu kutoka katika nchi duni hutamani kukimbilia huko kwenda kutafuta na kufanya kazi kwasababu mazingira ya upatikanaji wa kazi angalau ni mepesi ukilinganisha na nchi duni.

Leo naangazia zaidi Tanzania na Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi Tangu Tumepata Uhuru wa Tanganyika.

Huwa najiuliza sana ni Mapinduzi ya aina gani ambayo yamekuwa yakinasibiwa na hiki Chama kikongwe kinachoingoza serikali na vyombo vyake vya dola,Kila mwaka Chama hiki kimekuwa kikifanya maadhimisho ya kufikisha miaka kadhaa tangu kizaliwe lakini ukiwauliza ni mapinduzi ya aina gani waliyoyafanya wakati huo wananchi wetu wanaendelea kuwa masikini huwa wanabaki kuangaliana na ikiwezekana kukushughulikia kwasababu wao hawapendi kuhojiwa na kuulizwa kuhusu umasikini wa Mtanzania.

Chama hiki kimekuwa na sera zake kadhaa ambazo moja wapo ya sera yake kujinasibu kuitwa CHAMA CHA WAKULIMA NA MASIKINI.

Pamoja na kujinasibu kwa Majigambo kedekede lakini bado hakijaweza kufanya Mapinduzi ya Kumkwamua Mkulima kuondokana na Umasikini,vilevile bado hakijaweza kumkwamua Masikini kuondokana na Umasikini wa kutupa ambao umewafanya wananchi wengi kuwa na msongo wa mawazo kila uchwao hadi kupelekea mauti na kuwaacha wengine wakiwa Vichaa!.

Baada ya miaka mingi kupita nilitegemea kuona hiki Chama kinajinasibu kuitwa CHAMA CHA WAKULIMA NA MATAJIRI,na hii ingekuwa ni baada ya wananchi wetu kuupata Utajiri kupitia Kilimo chenye tija,badala yake hata wao wanaona aibu kujiita hivyo kwasababu hakuna Mapinduzi yeyote waliyoyafanya katika nyanja tofauti tofauti za kumuwezesha mwananchi kujikwamua kutoka kwenye umasikini.

Nilitegemea kuona mnafanya yafuatayo ili kumfanya mwananchi aweze kuwa na urahisi wa kujipatia kipato kitakacho muondolea umasikini wa kutupwa ambao umekuwa sifa kuu kwenye chama chenu.

1.MAPINDUZI KATIKA VIWANDA.

Hili ni eneo ambalo kila mtanzania angekuwa proud endapo lingekuwa limewekwa vizuri na serikali,viwanda muhimu karibia vyote vimekufa kabisa na vilivyopo vinapumulia mashine.

Tatizo lenu mmejaza maviwanda ya kutengeneza maji ya kunywa kila eneo na mnajisifu ni viwanda kumbe ni uozo mtupu,viwanda ninavyoongelea hapa ni viwanda ambavyo vingechakata malighafi za shamba moja kwa moja na kuuza bidhaa nje ya nchi,kwa mfano viwanda vya pamba na katani.

Leo ukisema unafanya kazi kiwandani basi kila mtu atakucheka na kukudharau kwasababu hakuna malipo huko bali ni utumwa wa kufa mtu,kibaya zaidi serikali na Chama chake wako kimya muda ambao wananchi wanalia na kuteseka,kazi wanayoiweza ni kusifu na kuabudu huku kelele za anaupiga mwingi zikisikika kwa wingi.

2.MAPINDUZI YA KILIMO.

Nilitegemea kuona mnawezesha mabenki ya kilimo yaweze kutoa mikopo kwa riba nafuu na masharti nafuu.
Sijui hata kama ile benki ya kilimo bado iko hai au ishajifia kifo cha Mjusi kafikiri,kibaya zaidi hata wakati inafanya kazi mikopo ilikuwa inatolewa kwa rushwa na kujuana,kama ulikuwa si mwanchama wa chama cha mapinduzi ilikuwa kupata mkopo ili kuwekeza kwenye kilimo ilikuwa kosa la Jinai.

Ukienda kwenye Korosho huko ni kilio cha kusaga meno kutoka kwa wananchi.

Haya ni machache tu lakini sekta zipo nyingi mno ambazo zilihitaji Mapinduzi ya hali ya juu ili kuwaondoa wananchi wetu kwenye umasikini.

Hivi serikali inategemea kabisa wananchi wake wawe matajiri kwa kilimo cha jembe la mkono?,Hivi kweli serikali inategemea wananchi wake wawe matajiri pasipo mikopo ya kilimo yenye riba nafuu?
Serikali hii ingekuwa serious leo hii watanzania wengi wangekuwa matajjri kwa kupitia kilimo tu.

Badala yake mmeacha kuyafanya hayo ili mwananchi aweze kujikwamua kwenye umasikini ila mnachokifanya ni kujisifu kwa kuwapigia magoti wazungu mliowaita mabeberu kwa kuwapatia mikopo yenye riba kubwa huku wananchi wakiendelea kuteseka namna ya kuyalipa hayo madeni.

Nilitegemea kuwaona viongozi wengi wa Chama hiki wakiumizwa na umasikini wa mtanzania na kuishauri serikali inayoongozwa na Chama Chao namna bora ya kuyafanya hayo ili kumfanya mtanzania kuwa na wepesi wa kujipatia kipato ili serikali iweze kukusanya kodi kwa urahisi.
Hivi ni nani aliwaambia wananchi wa Tanzania hawapendi kulipa kodi?,Hakuna mwananchi ambaye ameona serikali imeweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa kipato halafu akakataa kulipa kodi,huyo atakuwa mwendawazimu tu!.

Leo Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake imewafanya wananchi wote kuwa wafanyabiashara hata kama hawakusomea biashara kwasababu huko kwenye secta muhimu hakuna cha msingi zaidi ya upumbavu.

Mtu amemaliza chuo cha kilimo pale SUA lakini kwasababu ya upumbavu wa serikali isiyojali kilimo na vipengele vyake,mtu huyo anaenda kuwa machinga ili apate kipato aendeshe maisha yake,utaalamu wake wote kuhusu kilimo unafia mfukoni kwasababu ya upumbavu na ujinga wa serikali isiyojali.

Mtu amesoma pale UDOM mambo ya hali ya hewa lakini kutokana serikali kutokuwa na dira na mifumo ya kueleweka anaona bora Afungue duka la vipodozi ili ajipatie kipato maisha yake yasonge ilihali utaalamu wake ameuweka mfukoni wakati huo nchi ikiangamia.

Mtu amesoma zake pale UDSM mambo ya Elimu lakini akimaliza anashindwa aende wapi na aanzie wapi kwasababu Serikali iko bize na masuala ya kijinga,anaondoka zake anaelekea mtaani anatafuta cheti cha ufamasia anafungua duka la madawa muhimu ili ajipatie kipato kitakachomuzesha kupata angalau mlo.

Huyu aliyempa cheti cha ufamasia yeye unakuta yuko zake pale Muhimbili au Mwananyamala na hajali chochote,anachojali yeye ni fedha tu ili familia yake iishi vema,hajui kama huyu aliyepewa cheti cha ufamasia afungue duka la dawa hana hata huo ujuzi kuhusu madawa,hatimae watu wetu wanakufa kama sisimizi kwa uzembe na upumbavu wa serikali na Chama ambao wameshindwa kuweka mazingira bora ya watu wake kupata kipato.

Mtu amesoma zake pale TIA mambo ya Mapato lakini akirudi mtaani anakuta serikali inaajiri kwa kujuana na watoto wa wakubwa hatimaye tunakosa mkusanya Mapato muaminifu ambaye anaona ni bora kwenda kuuza mitumba ili kujikwamua kiuchumi,matokeo yake walioajiriwa kwa kujuana ndio wanaotuletea matatizo kwenye Taifa kwa upigaji na Rushwa!.

Serikali hii isiyojali inaendelea kusomesha watu wake wakati huo huo ikiwa inajua kabisa haiweki mazingira wezeshi ya watu wake kupata kipato,nilitegema kuona elimu yetu inaendana na mapinduzi katika VIWANDA na KILIMO ili iwe rahisi kuwezesha watu wetu kupata kipato,nilitegemea kuona hizo secta mbili ndizo ziwe zinaongoza kwa kuajiri watu wetu na siyo kuajiri tu,ziwe zinaongoza kwa pesa ili kila mwananchi aone fahari kujiita mkulima kwasababu kina fedha nyingi,nilitegemea kuona mwananchi anakuwa proud kufanya kazi kiwandani kwasababu analipwa kwa siku fedha nzuri ambayo inamfanya na yeye kufurahi kulipa kodi kwa serikali.

Leo hii ukisema unafanya kazi kiwandani ni aibu kubwa mno kwasababu hakuna maslahi zaidi ya kumenyeka kama punda na kuwanufaisha wamiliki na wawekezaji,leo mwananchi anafanya kazi kutwa nzima kiwandani analipwa elfu 5 -7,huu ni uonevu wa hali ya juu mno,wakati huo mwananchi akiumia hakuna kiongozi wa chama anayepigia kelele mambo kama haya,wizara ya viwanda ipo kama haipo,wizara ya kazi ipo kama haipo huku wananchi wetu wanaendelea kuwa masikini wa kutupwa.

Leo ukisema wewe ni mkulima kila mtu anabaki anakupa mgongo na kisogo(Dharau) kwasababu kwenye fikra zetu tunaamini mkulima ni mtu ambaye ameshindwa na maisha na anaye menyeka kisawa sawa na jembe la mkono,fikra hizi ambazo Chama kimeshindwa kabisa kuzifuta ni kwasababu bado wanaendelea kuamini UMASIKINI ni sifa moja wapo ya mwanadamu wa Tanzania.

Serikali hii na Chama Chake imewafanya watanzania wengi kukikimbia kilimo na kuwa wafanyabiashara ingawa hatukusomea hizo biashara kwasababu kilimo hakilipi.

Hatuhitaji mtuletee fedha mifukoni ila tengenezi mazingira mazuri ya upatikanaji wa fedha kwa urahisi,siyo sisi mtuite wakulima na masikini wakati huo nyie mkiendelea kula kuku na watoto wenu mkiwatafutia kazi za maana nje ya nchi na kwenye taasisi kubwa za serikali na sekta binafisi.

Kila mtu anapenda maisha mazuri,kila mtu anapenda kuishi kwenye nyumba bora na nzuri iliyoezekwa kwa mabati bora,kila mtu anapenda kuwa na usafiri wake,kila mtu anapenda kula raha!.

Siyo raha mzile nyie tu na watoto wenu wakati huo sisi na watoto wetu tukipitia msoto ambao mmeusababisha nyie.


Ni hayo tu kwa leo.
 
Kila mtu akiwekewa mazingira mazuri basi pesa itapatikana kwa urahisi na pesa itashuka thaman, NB: sipingani na wewe kwenye kuweka mazingira mazuri 😂 , lakini pesa haizunguki hivo
 
Termites-in-Your-Home.png
Tatizo ni hawa Mchwa waliopo Serikalini
 
Mimi nikinyonga wakianza kuiba naiba. wakiacha naacha.

nikiiona hapa hapafai.
naenda pale.pale hapa fai naenda pale". Bongo kubwa bwana

Nina kadi ya ccm na chadema"
vikao vya chadema nipo"ccm nipo posho nachukua!

Ofisini nimeweka bendera ya chama tawala ili nisi sumbuliwe na t.r.a'
Nina namba za wakuu wavituo vya polisi japo sio afisa wa serikali.
pia
Nina madem zangu watatu wakalii ma poti Ila hawajuani Hawa nikwa ajiri ya mishe zangu ziki buma Mambo yasonge.

Getto nnajezi ya ccm na chadema" nikienda tunduma navaa chadema. nikienda rungwe navaa ccm.
Chamsingi Mambo yasibume"

Nikikutana na business partner anapenda Simba siku ya kukutana nae navaa jezi ya Simba, tuna fanya biashara fresh Mambo Yana enda

Hivyohivyo kwa yanga business partner.sikosei

Ukinikuta nonde utanikuta nimeshusha pensi mlege

bega moja chini juu

njoo uhindini utanikuta nimepiga suti Safi na tai

Sjawai kuona Maisha magumu.

mdawote pochi imejaa sjawai kutegemea raisi kwani kwangu kilra raisi namtafutia mpigo wake

Ila hakuna kipindi kilikuwa Ni kigumu kidogo kwangu Kama kipindi Cha Kaka mkubwa

Mimi nilikuwa namwita
IRON GATE
R.I.P MWIBA
 
Back
Top Bottom