Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Pole sana Mkuu..ila hiyo uliyokuwa unafanya ndio KANGOMBA..yaani unanunua korosho kwa mkulima kwa shilingi 1000 ili wewe uje kuuza kwa 3300. Japo umesema hukuwa unawalazimisha ila ulitumia shida za wakulima kujinufaisha. Suala lako linafanana na utetezi wa kufanya mapenzi na binti chini ya miaka 18, hata kama ulimtongoza na kukubaliana lakini sheria itakuambia umebaka.
Umewahi kuishi kijijini na ukafuatilia kwa umakini shida za wakulima? Mimi nadhani serikali ilipaswa kutumia busara kuokoa pesa za wanunuzi wadogo wadogo, tofauti na hapo ngoja NAMBA ZIENDELEE kusomeka hadi akili zitukae vizuri.
 
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.

Hapo kosa ni lako, umefanya biashara ambayo sio halali
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Nilikuwa na mchumba wangu alinishikilia.nimpe mtaji aende kufanya biashara ya kununuwa na kuuza korosho mwaka huu. Nilimkatalia kata kata lakini alikuwa hasikii lolote mpaka uchumba ukavunjika kwa sababu hii. Sijui amefikia wapi sasa hivi na korosho zake, sitaki hata kujuwa.
 
Pole sana Mkuu..ila hiyo uliyokuwa unafanya ndio KANGOMBA..yaani unanunua korosho kwa mkulima kwa shilingi 1000 ili wewe uje kuuza kwa 3300. Japo umesema hukuwa unawalazimisha ila ulitumia shida za wakulima kujinufaisha. Suala lako linafanana na utetezi wa kufanya mapenzi na binti chini ya miaka 18, hata kama ulimtongoza na kukubaliana lakini sheria itakuambia umebaka.

Na huo ndio msingi wa Biashara. Buying at cheap price ili uuze kwa gharama kubwa kupata faida.

Ukiweka gharama za kusomba, kuhifadhi na nyingine za kuishi huko na kutafuta soko unafikiri anapata faida kiasi gani kwa Kilo?
 
Ukiwa muongo inabidi pia ujue namna ya kuandika uwongo uliokaribu ma ukweli!

Hii story yako utawaokota nyumbu wengi!
Mfuasi wa ibilisi katk ubora wako wa kijuha!!!,Aya tuambie ukweli unaojua wew sasa shenzi.Wew bila shaka utakua kidemon tupo huku tunashuhudia unyang'ananyi wew unaleta kejeli?mijitu nyie.....
 
Pole sana Mkuu..ila hiyo uliyokuwa unafanya ndio KANGOMBA..yaani unanunua korosho kwa mkulima kwa shilingi 1000 ili wewe uje kuuza kwa 3300. Japo umesema hukuwa unawalazimisha ila ulitumia shida za wakulima kujinufaisha. Suala lako linafanana na utetezi wa kufanya mapenzi na binti chini ya miaka 18, hata kama ulimtongoza na kukubaliana lakini sheria itakuambia umebaka.
Mfano wako ni senseless!!!!
 
How does the government of Tanzania think? Seems quite opposite to citizens thinking,
 
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.

Uandishi wako ni Too Political oriented. Mkulima anakulazimishje ununue? Anajuaje kama wewe una pesa? Ona majibu yako Ninahaki ya kufanya biashara mahala popte hoja c kufanya biashara popote bali namna gani unafanya hiyo biashara. Lakini uandishi wako ni wa Kusadikika style
 
Umewahi kuishi kijijini na ukafuatilia kwa umakini shida za wakulima? Mimi nadhani serikali ilipaswa kutumia busara kuokoa pesa za wanunuzi wadogo wadogo, tofauti na hapo ngoja NAMBA ZIENDELEE kusomeka hadi akili zitukae vizuri.
Mkuu sio kuwahi kuishi,ndio nipo huku. Nikuambie tu kwamba hawa 'wafanyabiashara wadogo' ndio wametufikisha hapa,kama utakumbuka mwaka jana korosho kwa kilo mnadani iliuzwa hadi 4,000/. Bei hii ikawavutia walanguzi waliokuwepo miaka ya nyuma na wapya kama huyu mtoa Uzi kuja kununua korosho kwa wakulima kwa bei ya chini ili wauze kwenye minada kwa bei ya juu.
Kilichotokea bei walionunulia kwa magendo kwa mkulima ndio hiyo ambayo ilitangazwa kwenye minada hivyo wakajikuta hamna wanachopata.Walichoamua kufanya kwa muamvuli wa wakulima wakatangaza kususa kuuza korosho kwenye minada. Utauliza kwavipi,jibu ni kwamba mwaka jana bei ya dira kwa kilo ilikuwa sh1300-1500 lakini wakulima hawakususia bei ya minada ya sh 2300 na ambayo ilipanda hadi hiyo 4000.
Hii 'biashara' ya korosho isome tu humu.
 
Najua kuna watu wamezurumika na serikali inachofanya si sahihi kwa uono wangu!...ila samahani kusema hii habari yako ni UONGO, umeitunga kwa watu tunaoweza kusoma miandiko!
 
pole Dada maisha ya sasa hivi Tanzania wengi wamepata hasara kwa mfumo unaoendana na wako kama vile walivyovamia Arusha na kuchukua hela wengine walikopa wana marejesho ila naamini utafanikisha tuu ukiona kiza ujue mwanga upo mbele yako usifikiri kujiumiza kwa lililotokea...ila inaumiza sana huko kusini wengi wameingia hasara sana...
 
Uandishi wako ni Too Political oriented. Mkulima anakulazimishje ununue? Anajuaje kama wewe una pesa? Ona majibu yako Ninahaki ya kufanya biashara mahala popte hoja c kufanya biashara popote bali namna gani unafanya hiyo biashara. Lakini uandishi wako ni wa Kusadikika style
Huyu jamaa bila shaka hata Kudini hajawahi kufika!

Anapata story na kuamua ku frame stori kama hii!

Wahanga utawajua kwa miandiko yake. Sio maswala ya dah hapo!😁😂😂😂😂
 
tapatalk_jpeg_1542131910472.jpeg
 
Back
Top Bottom