Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Chief, mimi naamini kwamba kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. Tusilazimishe kukomoana kwa kuwa tu mtu ana mtaji wake na tumeshajua kuwa amegomesha kutetea maslahi yetu. Kamba ya hao walivyokuwa Wakulima ilikuwa haiwaruhusu kungojea fedha za msimu, kwa maana nyingine hata wewe "Kama" una nafasi nzuri kifedha na upo kijijini bado kuna mkulima angeweza kuja kwako mkapatana na akaweka bond mavuno yake yote ya mwaka kabla ya msimu wa kununua. Ni hali duni ya Wakulima ndiyo imeruhusu wawepo wachuuzi hawa ambao mimi naona hakukuwa na ulazima wa kufanyia haya. Pesa amekula mkulima kwa hiari yake, leo tunataifisha mali ya mchuuzi, kesho tunasema tunaondoa umaskini...
Labda
Na ndiyo biashara zilivyo kila siku.Msimu wa mavuno watu wanakusanya mahindi na mpunga ndani.Bei ikichangamka wanapeleka sokoni.
 
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.

Pole Sana kwa yaliyokukuta. Inaelekea uliingia kichwa kichwa bila kuelewa kuwa biashara ya korosho haifanywi na kila mtanzania. Serikali imeshapiga marufuku kangomba na choma choma.., ungeuliza kabla ungeambiwa madhara yake. Sio kila wakati kuilaumu serikali bali unatakiwa ufuate taratibu na sheria, biashara ya korosho ni kwa wakulima tu wa korosho hatakiwi mtu kati wala dalali.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.

Aisee, is it true?

Si afadhali hata mnunuzi (serikali) angesema kuwa hanunui "za wasio na mashamba!!" kuliko kuiba (maana huo ni wizi wa mchana kweupe) wa mali halali ya mtu?

Yeah, kama siyo mali ya mtu halali, serikali ioneshe na kuthibitisha hivyo kwa kuonesha ni kosa gani kisheria na limefanywa na mtu huyu hata dola iibe mali yake?

Huyu Makufuli na watu wake na maamuzi yao ni lazima wana matatizo ya akili, siyo bure. Haya mambo hayawezekani kufanywa na watu wenye akili timamu, haiwezekani!!!

Hii ni ishara kuwa ipo siku wote tunaokula ugali ama ubwabwa ama maharage ama nyama ya ng'ombe tutaambiwa tuoneshe mashamba na mazizi ya kufugia ng'ombe...

Na tukishindwa kuonesha mashamba ama mazizi ya kufugia ng'ombe ama mbuzi tunapigwa marufuku kula vyakula hivyo na vikukutwa ndani ya nyumba zetu vinachukuliwa na serikali
na pengine kupelekwa kwenye mahakama na mahakimu na majaji wa Makufuli..!!
 
Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.
Unaichukia Tanzania?
Kwani ndiyo iliyokunyang'anya korosho zako?
Tulia umfahamu adui yako. Tanzania sio adui yako. Usipomjua adui utamshinda vipi ili ujipatie haki yako?
 
Huyu Makufuli na watu wake na maamuzi yao ni lazima wana matatizo ya akili, siyo bure. Haya mambo hayawezekani kufanywa na watu wenye akili timamu, haiwezekani!!!

Unajua Kitaturu, kuna watu wamebarikiwa na kuwa na uwezo mbalimbali. Wapo wanaoweza kukulisha matango pori bila mwenyewe kujua unakula visivyolika.
Kuna watu kazi wanayoiweza ni kujiweka tu katikati ya matatizo ya watu na kuyafanya yaonekane ni matatizo yasiyoweza kutatuliwa.
Nimemsoma vyema kabisa huyo mleta mada na kuwaza sana. Ndio, tuna utawala wa ajabu sana kwa sasa na unaweza kufanya lolote watakalo kulifanya wenyewe hata liwe baya kiasi gani. Tumekwishaona mifano halisi ya mambo wanayoweza kuyafanya.

Nakataa katakata kwamba mleta hoja kafanyiwa kama anavyodai hapa.
Watu wa aina hii ndio watakaofanya kazi ya kuuondoa udhalimu unaotukabili iwe ngumu zaidi.
 
Wewe unatetea wizi , dhuluma ya serikali kwa raia wake. Kwani serikali hii kudhulumu raia wake wameanza leo kwenye korosho? Si hata hela za rambirambi Bukoba walizidhulumu, ili hali rambirambi zilizotolewa kwenye msiba wa dada yake Magufuli hatukusikia zikichukuliwa na serikali kufanya kazi za jamii.
Unatete uovu wa serikali hii ya kidikteta.
hoja yako ni ipi?,nimekwambia nacho fahamu juu ya ushirika hawaruhusu mfanya biashara kule

hayo mambo ya rambirambi yafungulie uzi ntachangia
 
Mbona mahindi watu wanunua maelfu ya magunia na wanauza sehemu nyingine serikali haihoji? Kwani korosho ni haramu ? Aibu kubwa kwa Utawala huu wa kihuni na udikteta?
Hapa nilipo ukileta "u-KANGOMBA " kwenye karafuu ndiyo mwisho wa kulalia kitanda chako....acha watuondolee hawa middle man maana walikuwa wakitoka kwenye korosho hao wanakuwadia wagombea udiwani wa ccm..kama vipi wanunue chuma chakavu tu!
 
Unajua Kitaturu, kuna watu wamebarikiwa na kuwa na uwezo mbalimbali. Wapo wanaoweza kukulisha matango pori bila mwenyewe kujua unakula visivyolika.
Kuna watu kazi wanayoiweza ni kujiweka tu katikati ya matatizo ya watu na kuyafanya yaonekane ni matatizo yasiyoweza kutatuliwa.
Nimemsoma vyema kabisa huyo mleta mada na kuwaza sana. Ndio, tuna utawala wa ajabu sana kwa sasa na unaweza kufanya lolote watakalo kulifanya wenyewe hata liwe baya kiasi gani. Tumekwishaona mifano halisi ya mambo wanayoweza kuyafanya.

Nakataa katakata kwamba mleta hoja kafanyiwa kama anavyodai hapa.
Watu wa aina hii ndio watakaofanya kazi ya kuuondoa udhalimu unaotukabili iwe ngumu zaidi.

Hebu fafanua kwa nini unakataa?

Umeona viashiria vyovyote kuwa huyu mtu anajaribu kutulisha matango pori tu hapa?

Kwa upande wangu nionavyo na kwa jinsi mambo chini ya uongozi wa serikali hii yanavyokwenda, sioni shaka wala ajabu haya kutendwa na dola

Kama watu (vyombo vya usalama/dola) vinateka na kuwapoteza raia eti wanaikosoa "serikali", wanajaribu kuua ama kuua kabisa kwa risasi za vita na kila aina ya uovu hili nalo unaonaje ajabu kutendwa na hawa viumbe??
 
Hapa nilipo ukileta "u-KANGOMBA " kwenye karafuu ndiyo mwisho wa kulalia kitanda chako....acha watuondolee hawa middle man maana walikuwa wakitoka kwenye korosho hao wanakuwadia wagombea udiwani wa ccm..kama vipi wanunue chuma chakavu tu!
Biashara yoyote lazima kuwepo na mtu wa kati....
Haiwezekani wote muwe wakulima
Haiwezekani wote muwe wachimbaji madini
Etc....huo unaitwa mgawanyo wa kazi
Wote mpata riziki

Ova
 
Wasajiliwe na kupata leseni haina shida
 
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.
DUH, NIMESOMA HUU UZI, NIMENYON'GONYEA, INAUMA SANA, ILA MKUU JIKAZE TU HIO NDIO SEHEMU 1 YA LIFE
 
Wasajiliwe na kupata leseni haina shida
Mbn Wana leseni kitambo za kununulia mazao.....tatizo hapa ni kuonesha shamba
Lilipoletwa
Yaani mm broker wa madini Nna leseni ya ubroker na nailipia kila mwaka ukinikuta na madini unaniambia nioneshe leseni ya mgodi?
Kwa style hyo wnaua biashara zote.....
Kwenye koroshow serikali wao wangendelea kusimamia tu ila game la koroshow waache mkulima na mfanyabiashara walicheze
Biashara haitaki sjui jeshi etc ingilie biashara inayumbaaa na kuelekea kufa

Ova
 
Sheria ya kwamba ukiwa na bucha ya kuuzia nyama lazima uonyeshe zizi?
Wacha kuchanganya mambo ya facebook humu. Hivi unaweza kuwa na bucha halafu usiwe na leseni pamoja na kibali afya ukaachiwa???????
 
Back
Top Bottom