Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Baba yangu jee ulikuwa na leseni ya biashara??????????????
Kisheria inawezekana kuwa wewe ni mlanguzi kwa sababu huna shamba wala leseni ya biashara hiyo.
Ninadhani mwisho wa siku mtalipwa ila jamani tujifunze kufuata sheria na taratibu zake.
Ngoja yakikukukuta ndio utajua km kunasheria au laa.
 
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.
pole kijana.
wewe sasa unga mkono "Azimio la Zenji" lilitolewa jana ili yule "nduli mla korosho" anyolewe bila maji!
 
Ngoja yakikukukuta ndio utajua km kunasheria au laa.
Suala siyo kunikuta au kutonikuta. Hapa kuna mtu amelalamika kuwa kama mjasiriamali alikwenda kusini kununua korosha na wakati wa kuuza anaulizwa kama ana shamba au la.
Nilichosema mimi ni kwamba kama hana leseni wala kibali cha kununua zao hilo basi kisheria yeye ni mlanguzi. Nilimuasa pia kabla ya kufanya biashara yoyote ile azingatie sheria na kanuni zinazohusiana na biashara tarajiwa.
 
Nilikuwa mtwara (masasi) hali ni mbaya kwa wakulima wa korosho. Mungu aingilie kati
 
Hebu fafanua kwa nini unakataa?

Umeona viashiria vyovyote kuwa huyu mtu anajaribu kutulisha matango pori tu hapa?

Kwa upande wangu nionavyo na kwa jinsi mambo chini ya uongozi wa serikali hii yanavyokwenda, sioni shaka wala ajabu haya kutendwa na dola

Kama watu (vyombo vya usalama/dola) vinateka na kuwapoteza raia eti wanaikosoa "serikali", wanajaribu kuua ama kuua kabisa kwa risasi za vita na kila aina ya uovu hili nalo unaonaje ajabu kutendwa na hawa viumbe??
Bora umumuambia
 
Pole sana. Hiyo ndio serikali ya wanyonge na masikini wa nchi hii. Wanasisitiza vijana kuwa wajasiria mali ukianza tu kabla hata hujapata faida yoyote TRA hawa hapa! Umeenda kufanya biashara ya mazao kwa mtaji wa kukopa matokeo yake ndiyo hayo. Pole sana kiongozi
 
hoja yako ni ipi?,nimekwambia nacho fahamu juu ya ushirika hawaruhusu mfanya biashara kule

hayo mambo ya rambirambi yafungulie uzi ntachangia
Hoja yangu ni kwamba serikali ina tabia ya kudhulumu raia wake kama ilivyofanya kwemye musiba ya ajali ya tetemeko kule Bukoba na sasa kwa wakulima wakulima na wafanya biashara ya korosho.
 
Baba yangu jee ulikuwa na leseni ya biashara??????????????
Kisheria inawezekana kuwa wewe ni mlanguzi kwa sababu huna shamba wala leseni ya biashara hiyo.
Ninadhani mwisho wa siku mtalipwa ila jamani tujifunze kufuata sheria na taratibu zake.
Mnunuzi mdogo wa kawaida huwa hana leseni kwakuwa yeye anadunduliza na hii wengi huwa tunafanya. Uko mjini unatuma hela kijijini au unakwenda nyakati za mavuno wakulima huwa wanakuwa wameishiwa kabisa wanatafuta hela ya matumizi hivyo huuza kidogo kidogo mazao yao. Kwahiyo wewe unakusanya taratibu kisha uje uuze baadaye.

Hayo ni maelezo ya ziada lakini ukisoma na kufuatilia yanayyotokea kusini ni kuwa wao wanataka shamba siyo leseni
 
Hoja yangu ni kwamba serikali ina tabia ya kudhulumu raia wake kama ilivyofanya kwemye musiba ya ajali ya tetemeko kule Bukoba na sasa kwa wakulima wakulima na wafanya biashara ya korosho.
Vyama vya ushirika na mazao yake haviruhusu wafanya biashara mkuu. usitake kuhalalisha madai yako kwa kuchomekea kwamba wafanya biashara wamedhurumiwa hilo sitakubaliana na ww hata usemeje

serikali kutaifisha korosho za wasio wakulima iko sahihi 100%
 
Na serikali kutaifisha fedha za rambirambi misiba ya maafa ya tetemeko kule Bukoba ni 100/% sawa pia? Tabia ya serikali kudhulumu mali za watu imekuwa order of the day. Huo ni ukweli taka usitake. But mind you, nothing is permanent, Magufuli will eventual go, and his crimes left behind will be wiped away.
 
Mnunuzi mdogo wa kawaida huwa hana leseni kwakuwa yeye anadunduliza na hii wengi huwa tunafanya. Uko mjini unatuma hela kijijini au unakwenda nyakati za mavuno wakulima huwa wanakuwa wameishiwa kabisa wanatafuta hela ya matumizi hivyo huuza kidogo kidogo mazao yao. Kwahiyo wewe unakusanya taratibu kisha uje uuze baadaye.

Hayo ni maelezo ya ziada lakini ukisoma na kufuatilia yanayyotokea kusini ni kuwa wao wanataka shamba siyo leseni
.You are missing a point.
Serikali ilisema kuwa itanunua korosho za wakulima. Sasa kama wewe ni mlanguzi, by definition hustahili kuwemo kwenye kundi.
 
Baba yangu jee ulikuwa na leseni ya biashara??????????????
Kisheria inawezekana kuwa wewe ni mlanguzi kwa sababu huna shamba wala leseni ya biashara hiyo.
Ninadhani mwisho wa siku mtalipwa ila jamani tujifunze kufuata sheria na taratibu zake.
Wanunuzi wengi wa mazao ni wavumilivu sana. Bei za mazao Tz hii zinayumba yumba sana. Hivyo biashara ya mazao ni bahati nasibu. Unaweza nunua mpunga gunia debe saba kwa sh 90000 halafu ukaenda sokoni ukakutana na mafuriko ukauta unakoboa na kupata sh 60000 kwa gunia. Hivyo wengi hawakati leseni kwani biashara yenyewe ni pasua kichwa sometime. Warudishe korosho za watu huu ni wizi wa mchana kweupe very shem.
 
Baba yangu jee ulikuwa na leseni ya biashara??????????????
Kisheria inawezekana kuwa wewe ni mlanguzi kwa sababu huna shamba wala leseni ya biashara hiyo.
Ninadhani mwisho wa siku mtalipwa ila jamani tujifunze kufuata sheria na taratibu zake.

Kama hana leseni basi atakuwa amevunja tu sheria na stahili yake ni limepelekwa mahakamani na kushtakiwa; siyo kunyang'anywa korosho zake. Kama wamachinga hawana leseni na wanafanya biashara kwanini huyu wa korosho awe ametenda dhambi kubwa kiasi cha kunyang'anywa mali yake? Kuna tatizo kubwa.
 
Kama yeye siyo mkulima na hana leseni wala kibali, amezipata wapi? Hapa inapigwa vita 'Kangomba'
 
Pole sana ndugu,haya yanamwisho.Lakini afadhari ya wewe umenyang'anywa korosho lakini bado upo hai,wapo ambao wamenyang'anywa uhai wao na kitengo maarufu kijulikanacho wasiojulikana.
 
Hebu tuacheni ungese watanzania wenzangu, hakuna asiyejua sekeseke la korosho mwaka huu lilivyotikisa vyombo vya habari. Mie mwenyewe ilibaki kidogo niwe muhanga wa hilo sakata ila kilichonisaidia ni subira...sikuweka hela mpaka mnada wa kwanza ulipopita nikaona mambo hayaeleweki nikavunga!
Hebu acha kujifanya wazimu kwamba hujui biashara nyingi za vilimo zinaendeshwa kienyeji hapa nchini, unaropoka tu kama vile babu yako alikuwa na TIN namba na leseni ya kulimia kahawa na maharage.
Ebu pata kuelewa. Hawa Kangomba hawanunui Korosho mnadani hata siku moja. Wana njia zao za kupata korosho nawewe unajua hilo.
 
Back
Top Bottom