#COVID19 Serikali imeanza kulazimisha watu kuchanja chanjo za COVID-19?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Inavyoonekana serikali ya Tanzania imeanza kulazimisha wananchi kuchanja chanjo za Covid bila ridhaa zao.

Tumeona mkuu wa mkoa wa Mbeya akitoa kauli za kulazimisha watu huko Mbeya kuchanja ikiwemo wafungwa

Sasa kuna kauli tena ya serikali ikiagiza wakurugenzi watendji wa Taasisi za serikali "kuhamasisha" watumishi wote wa serikali kuchanja. Hii kauli ni kama vile muendelezo wa kuamplify kidogokidogo hatua za kuwalazimisha watu kuchanja.

Binafsi ninasema, Suala la chanjo ni la Afya ya mtu binafsi, serikali haina haki ya kumlazimisha mtu kinachoingia katika mwili wake hasa kama ana wasiwasi na Matokeo ya kitu hicho

Pia rais alishasema kuwa chanjo ni hiyari, sasa sitegemei kuona tunalazimishana. Kama serikali itaanz kulazimisha watu kuchanja hii maana yake ni kuwa itakuwa imemfanya rais aonekane Muongo!

Najua serikali inataka hela kutoka kwa Mabeberu, lakini hela isiwe sababu ya kulazimishana.

WENYE KUTAKA CHANJO WACHANJE, NA WASIOTAKA TUSILAZIMISHANE!

Ila hali ngumu, maana juzi Msigwa kasema laki 4 tu ndiyo wamechanja, lakini dsm tu kuna watu karibia million 5.....bado mwamko ni mdogo sana
 
Wanachotaka kufanya ni uhuni, mambo ya tiba hayalazimishwi ni uvunjivu mkubwa wa haki za watu. kabla ya kuwalazimisha watumishi wa serikali kuchanja waanze kutoa option ya wale wasiotaka kuchanja walipwe mafao yao wasepe ili waingize kigezo cha kuchanja kama sifa ya kuwa mtumishi wa umma.
 
1632724108512.png
 
Kwenye mikataba ya ajira hakukuwa na kipengele cha kulazimishana kuchanja. Itakuwa ni kinyume cha mikataba ya kazi na sheria za utumishi muajiri kulazimisha hatua za kitabibu ambazo muajiriwa hataki

Kwa mujibu wa sheria
Unalalamikaaaaaa 🤣

Asubuhi asubuhi yote hii.
 
Na Mh Rais wa JMT kuwa kimya kuhusu matamko ya wasaidizi wake hawa sijui anatupa ujumbe gani? Kwamba ndio tuelewa anatutangazia chanjo ni hiari wakati huohuo akienda kwa wasaidizi wake kuwapa maelekezo anawaamrisha wakalazimishe wananchi kuchanjwa.
 
Inaelekea ndicho alichoambiwa huko kwa Mabeberu kuwa afanye chanjo kuwa ni lazima ili apate ushirikiano wao!
 
Tatizo hiyo chanjo imekuwa outdated maana huko ilikotoka walioichanjwa sasa hivi wanachanjwa tena booster
 
Inaelekea ndicho alichoambiwa huko kwa Mabeberu kuwa afanye chanjo kuwa ni lazima ili apate ushirikiano wao!
Nahisi hilo, maana hata hotuba yake iliegemea zaidi kujitetea kuhusu hatua tulizochukua kama nchi kuhusu covid, kuliko kueleza sera za mahusiano ya nchi yetu na mataifa mengine.......
 
Chanzo zenyewe bado mwezi mmoja ziishe muda wake...Ndio maana wa haha zisije kuwafia.
 
Inavyoonekana serikali ya Tanzania imeanza kulazimisha wananchi kuchanja chanjo za Covid bila ridhaa zao.

Tumeona mkuu wa mkoa wa Mbeya akitoa kauli za kulazimisha watu huko Mbeya kuchanja ikiwemo wafungwa

Sasa kuna kauli tena ya serikali ikiagiza wakurugenzi watendji wa Taasisi za serikali "kuhamasisha" watumishi wote wa serikali kuchanja. Hii kauli ni kama vile muendelezo wa kuamplify kidogokidogo hatua za kuwalazimisha watu kuchanja.

Binafsi ninasema, Suala la chanjo ni la Afya ya mtu binafsi, serikali haina haki ya kumlazimisha mtu kinachoingia katika mwili wake hasa kama ana wasiwasi na Matokeo ya kitu hicho

Pia rais alishasema kuwa chanjo ni hiyari, sasa sitegemei kuona tunalazimishana. Kama serikali itaanz kulazimisha watu kuchanja hii maana yake ni kuwa itakuwa imemfanya rais aonekane Muongo!

Najua serikali inataka hela kutoka kwa Mabeberu, lakini hela isiwe sababu ya kulazimishana.

WENYE KUTAKA CHANJO WACHANJE, NA WASIOTAKA TUSILAZIMISHANE!

1. Wale watu waliofanya ugaidi na mbowe, ambao tayari wameshaanza kkutumikia vifungo vyao ni akina nani?

2. Tumechanja 30% ya watanzania, ni kweli tumechanja 18,000,000?

3. Watanzania hawana matatizo na tozo za simu. Kodi juu ya kodi, kodi ya matumizi. Ni kweli hii?

4. Watanzania wameichagua ccm iwaongoze ni kweli?

5. n.k, n.k.
 
Kama mnasema magufuli alikuwa anapika data ,wapike data na hizo chanjo kuonesha watazania wamechanjwa milioni kasoro moja ila watanzania wenyewe tunajua moyoni.
 
Kwenye mikataba ya ajira hakukuwa na kipengele cha kulazimishana kuchanja. Itakuwa ni kinyume cha mikataba ya kazi na sheria za utumishi muajiri kulazimisha hatua za kitabibu ambazo muajiriwa hataki

Kwa mujibu wa sheria
Sio kwenye kipengele Cha ajira tu, Bali suala la matibabu ni hiari ya mgonjwa.
Mgonjwa ana haki ya kukataa dawa au matibabu.
 
Back
Top Bottom